Je! Kuvuta Sigara ni Dhambi?

Mtume (s.a.w) amesema; kila kinacholevya ni haramu kukitumia,
naomba kuwasilisha kwa kujibia hoja.
 


Mkuu, kwanza yakupasa uelewe dhambi ni kitu gani, dhambi ni sumu inayoangamiza roho, kuna kuangamiza roho (kutenda dhambi) kwa njia mbalimbali, kama ulivyo ainisha mwenyewe aina ya dhambi kama uzinifu nk, hizo ni dhambi za moja kwa moja. kuna aina ya dhambi ambazo sio za moja kwa moja ambazo huandaliwa mazingira ili zitokee, mfano kudhuru mwili kwa makusudi ukizingatia kuwa mwili na roho zina mahusiano, yaani mwili wenye Afya na roho yenye afya na vice versa, sasa roho ikiwa haina afya matokeo yake utakuwa na roho itakayo tekeleza maasi.

Kifupi kuvuta sigara au kufanya jambo linalodhuru afya ya mwili ni makosa mbele ya Mungu. Ndiyo maana hatuoni katika historia manabiii Mungu walivuta sigara wala kutumia vyovyote vinavyodhuru afya za mwili si Muhammad (saw) wala nabii Isa (as), nabii Muhammad (saw) alisema "kuleni vilivyo halali na vizuri".
 
Cha kushangaza ni moshi ya kuni haina shida kwa binadamu. Zaidi zaidi inafanya macho yawe nyekundu, na pengine kuitwa mchawi! Lakini moshi ya sigara imejaa sumu ya kila aina - nicotine na toxic chemicals tele.
kwahiyo moshi wa kuni hauna sumu yoyote! ?
 

Chochote utakachotumia na kikakudhuru hali yakuwa unajua hiki kina madhara basi utaandikiwa umefanya uovu hivyo utapata dhambi.
Na hapa vitaingia vitu vingi sana.
 
Chochote utakachotumia na kikakudhuru hali yakuwa unajua hiki kina madhara basi utaandikiwa umefanya uovu hivyo utapata dhambi.
Na hapa vitaingia vitu vingi sana.
Kama Sigara
Aliyetengeneza kaandika kabisa,

" Ni hatari kwa afya yako"

Bado unajitoa ufahamu na kuendelea kuitumia.

Hivi Sigara ni bora kuliko afya yako ?
Wale wanaotumia wajitahidi kuanza hatua za kuachana nayo ili kulinda afya zao.
Wale wanaotaka kujifunza uvutaji sigara waache kufanya hivyo.

Sigara ni kama tendo la kujiua, na kujiua ni dhambi pia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…