Je, kutumia sh.50,000/= kulipa TRA kodi Nyumba ya sh.10,000/= ni akili au matope?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,063
40,724
Vitu vingine vinatia aibu, maana vinareflect IQ vya yule anaevifanya, je, ndio tuseme watunga sera wa TRA wana IQ ndogo?

Kodi ya majengo kwa nyumba ya chini ni shs.10,000/= tu, lakini gharama ya pesa + muda + usumbufu + phychological stress ya kuilipa hiyo shs.10k si chini ya sh.50k; sasa je, hii ni akili au matope?

Kwa mtu ambae akili yake inafanya kazi sawa sawa lazima angetafuta njia nzuri na rahisi ya kukusanya hii kodi; mfano, kwani haiwezekani hii kodi ya majengi ikaunganishwa kwenye luku za umeme?waweke hata 0.000000000001/= shs kwa kila unit ya umeme, hivyi jinsi nyumba ilivyokubwa zaidi au ya kibishara zaidi (mfano bar/kiwanda etc.) ndio jinsi umeme utatumika kwa wingi na ndio jinsi atalipa kodi zaidi ya majengo, maana sio nyumba haishi mtu miaka bado ailipie. Na kama mtu hana umeme nyumbani kwake basi huyo ni wale ambao serikali haina haki ya kudai kwa sababu bado haijatimiza wajibu wake wa kumpelekea huduna hii muhimu, au la, ni wa hali ya chini sana na anatakiwa awe exempt na hii kodi. Kodi ni muhimu, tuwekeeni mifumo rafiki tulipe kodi.

Pia italeta ufanisi wa rasilimali watu, zike gharama za matangazo, kampeni, maafisa wa kufuatilia na wale wa kukaa kwenye zike desk watatumika mahala pengine penye uhutaji.
 
Hakika kunapoint humu ndani yake.. ila hapo kwenye kusema usipotumia nyumba basi usilipe ni pumba.. kwani hiyo nyumba inatoweka pia??
Pia huo mfumo utajigawa tu..vipi kwa wale wasio na huduma za umeme au maji kwa ajili ya umasikini..wasilipie hiyo ADA kisa hawana huduma??
Nimetengua kauli yangu yakusema una Point.
Kifupi hii ni porojo
Haina mantiki
Nimejifunza jambo kupitia uzi huu....umefikiria mbali sana...mkuu ungekuwa karibu ungepata hata soda upoze koo

huyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika kunapoint humu ndani yake.. ila hapo kwenye kusema usipotumia nyumba basi usilipe ni pumba.. kwani hiyo nyumba inatoweka pia??
Pia huo mfumo utajigawa tu..vipi kwa wale wasio na huduma za umeme au maji kwa ajili ya umasikini..wasilipie hiyo ADA kisa hawana huduma??
Nimetengua kauli yangu yakusema una Point.
Kifupi hii ni porojo
Haina mantiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani nyumba isiyotumika inazalisha nini hadi ilipiwe kodi? Maana inakuwa haina tofauti na kichuguu kinachoishi wadudu tu; nilishwahi kuleta hoja humu miaka ya nyuma kuhusu road license iunganishwe kwenye mafuta, na gari ambayo haitumiki imepaki tu nyumbani kwa sababu mbali mbali isilipiwe road license, wapo waliopinga lakini baadae wazo langu lilifikishwa bungeni na mbunge Kessy, na hatimae lilitekelezwa.
Pia kama mtu hamjampelekea huduma ya umeme nadhani iwe ni chachu sasa kwa serikali kufanya hivyo ili iweze kukinga kodi yake ya majengo kwenye luku, au kama mtu hana uwezo basi aunganishiwe bure kisha alipe kidogo kidogo kwenye luku kadri anavyonunua hadi deni la awali litakapoisha, na serikali itakusanya kiulaini kodi ya majengo na kuokoa rasilimali watu inayotumika kukusanya hii kodi.
 
Nisaidie wewe kushangaa ... taasisi za serikali zimefilisika mawazo "... imagine .umeme .maji .etc unalipia kwa mfumo wa ki-electronic lakini mamlaka ya mapato tanzania .. imeshindwa kuiga huo mfumo ili waweze kupunguza foleni katika kazi zao pia wameshindwa kubuni njia kama hiyo ili waweze kulisaidia taifa liweze kupiga hatua kubwa katika suala la uchumi..

Watu wanapokwenda kulipia hiyo kodi",wanaacha masuala yao ya msingi ya kujiingizia kipato .. so kwa namna moja ama nyingine .. kuna pesa nyingi ambazo serikali inakosa kuziingiza "toka kwa wale watu ambao wanakuwa wapo TRA muda huo kwaajili ya kwenda kulipa hiyo kodi ...
.

Ccm oyee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vingine vinatia aibu, maana vinareflect IQ vya yule anaevifanya, je, ndio tuseme watunga sera wa TRA wana IQ ndogo?
Kodi ya majengo kwa nyumba ya chini ni shs.10,000/= tu, lakini gharama ya pesa + muda + usumbufu + phychological stress ya kuilipa hiyo shs.10k si chini ya sh.50k; sasa je, hii ni akili au matope?
Kwa mtu ambae akili yake inafanya kazi sawa sawa lazima angetafuta njia nzuri na rahisi ya kukusanya hii kodi; mfano, kwani haiwezekani hii kodi ya majengi ikaunganishwa kwenye luku za umeme?waweke hata 0.000000000001/= shs kwa kila unit ya umeme, hivyi jinsi nyumba ilivyokubwa zaidi au ya kibishara zaidi (mfano bar/kiwanda etc.) ndio jinsi umeme utatumika kwa wingi na ndio jinsi atalipa kodi zaidi ya majengo, maana sio nyumba haishi mtu miaka bado ailipie. Na kama mtu hana umeme nyumbani kwake basi huyo ni wale ambao serikali haina haki ya kudai kwa sababu bado haijatimiza wajibu wake wa kumpelekea huduna hii muhimu, au la, ni wa hali ya chini sana na anatakiwa awe exempt na hii kodi. Kodi ni muhimu, tuwekeeni mifumo rafiki tulipe kodi.
Pia italeta ufanisi wa rasilimali watu, zike gharama za matangazo, kampeni, maafisa wa kufuatilia na wale wa kukaa kwenye zike desk watatumika mahala pengine penye uhutaji.
Mada yako haina mashiko kumbuka hizohizo kodi zanyumba zimetofautiana kunawatu wanalipa zaidi ya 500000 kwa mwaka
 
Na ndio maana kama jengo ni kubwa la ghorofa maana yake litatumia umeme mwingi zaidi na hivyo bado wataendelea kulioa kodi kubwa zaidi, accordingly, na pia nyumba za ghorofa ni chache sana kwa uwiano ukilinganisha na zile za chini za sh.10,000/= kwa mwaka!
 
Hapa umeamua kutatua tatizo dogo kwa kuongeza tatizo lingine. Nadhani hoj ni namna gani TRA wanaweza kuboresha mifumo iwezeshe kukusanya kodi hii kirahisi, ungetolea mfano polisi wa barabarani mbona wameweza kuwa na mfumo wa kulipa adhabu ambao ni rafiki. Kwa hyo ufumbuzi ni kuwa na mifumo rafiki kama hiyo na sio kuongeza kwenye umeme,, viwanda vitakua vinalipa kodi kubwa kiasi gani?

Hilo la trafiki tambua mimi ndie niliependekeza miaka ya nyuma kwamba " Trafiki wafungiwe mashine za EFD" na serikali ikalifanyia kazi. Sasa hapa jikite kwenye hoja, hebu nieleweshe,natengeneza vipi tatizo kubwa?, karibu tujadili. Na usifikiri wahusika hawapo humu, maana nilishawahi kuoendekeza ndege za rais wapewe ATCL na kweli rais akawapa, so be free. Na hicho unachosema juu ya viwanda ni sawa na wale waliolalamika gharama za usafirishaji zitakuwa juu kisa road license zitalipiwa kwenye mafuta, kwani hata sasa wenye viwanda si wanalipia kodi ya majengo yao au? Tofauti ni kwamba watailipa kwenye umeme, basi!
 
Hakika kunapoint humu ndani yake.. ila hapo kwenye kusema usipotumia nyumba basi usilipe ni pumba.. kwani hiyo nyumba inatoweka pia??
Pia huo mfumo utajigawa tu..vipi kwa wale wasio na huduma za umeme au maji kwa ajili ya umasikini..wasilipie hiyo ADA kisa hawana huduma??
Nimetengua kauli yangu yakusema una Point.
Kifupi hii ni porojo
Haina mantiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hii ndiyo JF
 
Mda umefika sasa, tusiwe watu wa kupanga foleni, nadhani hii kodi ilipiwe peke yake isiunganishwe kupitia luku za umeme, ila kila nyumba isajiliwe kupitia luku za umeme kupunguza gharama, TRA waweke namba zao za kumbukumbu kisha tulipie kama tunavyolipa sasa umeme, maji, luku na traffic...imenichosha sana leo nimepanga foleni lisaa lizima benki kisa ninalipia hela ya form ya kumuandikisha mwanafunzi
 
Hilo la trafiki tambua mimi ndie niliependekeza miaka ya nyuma kwamba " Trafiki wafungiwe mashine za EFD" na serikali ikalifanyia kazi. Sasa hapa jikite kwenye hoja, hebu nieleweshe,natengeneza vipi tatizo kubwa?, karibu tujadili. Na usifikiri wahusika hawapo humu, maana nilishawahi kuoendekeza ndege za rais wapewe ATCL na kweli rais akawapa, so be free. Na hicho unachosema juu ya viwanda ni sawa na wale waliolalamika gharama za usafirishaji zitakuwa juu kisa road license zitalipiwa kwenye mafuta, kwani hata sasa wenye viwanda si wanalipia kodi ya majengo yao au? Tofauti ni kwamba watailipa kwenye umeme, basi!
Ni muhimu kodi ya ardhi na majengo ikabaki hivyo, kuiweka kwenye umeme sio sahihi kwa sababu umeme huo unatumika kwa matumizi mbalimbali tofauti na majengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwani lazima uende ukapenge foleni kuilipa hiyo kodi? Naona Mkuu wewe ambaye hutumii umeme unataka kukwepa kodi! Je, kwa yule anayetumia solar unataka kusemaje? yeye silipe kodi?
Kama mtu anatumia solar maana yake serikali haijatimiza wajibu wake wa kumpelekea umeme, hivyo iwe chachu kwa serikali kuhakikisha kila mwanachi anafikiwa na huduma ya umeme. Pia hilo la kupanga foleni sio hoja, hoja ni ile gharama ya ujumla anayoingia mwananchi na wanayoingia TRA kwa kuajiri wafanyakazi lukuki ili kuipokea hiyo shs.10,000/=, ni gharama kubwa sana kwa uwiano!
 
naona kama umeandika kwa hasira au sijui kwa jaziba
Mimi nafikiri kikubwa ni kuelimisha watu ili wawe tayari kulipa bila kulazimishwa na pia kuunganisha huu mfumo wa kodi za nyumba uwe wa kielekronic
na hii itawezekana tu baada ya kuzisajili nyumba/makazi na kupatiwa namba
 
Sidhani kama ni sahihi sana iwe kwenye mfumo huo.
TRA wangerahisisha maisha kwa kuweka mfumo wa watu kulipa bila kwenda kupanga foleni.
Halafu kupanga foleni kizamani sana. Huduma zote za malipo wangeziweka tulipe kama wenzao TANESCO na DAWASA.
Au wangeweka mawakala kama bank zinavyofanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu asie na uwezo na mwenye uwezo unampima kwa mizani Gani..

Back
Top Bottom