Je, Kutumia Bilioni 800 Kujenga Barabara Za Mitaa ya Dar Wakati Kuna Mikoa Haijaunganishwa na Lami Haiwezi Kuwa Ni Upendeleo?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,779
Nimejaribu Kujiuliza na kufikiria pengine Kwa akili yangu finyu kwamba inawezekanaje Kutenga zaidi ya Bilioni 800 Kwa Ajili ya kujenga Barabara za Mitaa za Jiji la Dar wakati Kuna Barabara Kuu za Kuunganisha Mikoa na Mikoa na Nchi na Nchi jirani Bado Zina mavumbi,Hii ni sawa? Haiwezi Kuwa ni Upendeleo?

Nafahamu Jiji la Dar linahitaji Barabara za mitaa lakini Kwa nini hatuna Vipaombele?

Swali la Kujiuliza ,Kipi kina impacts kubwa kwenye uchumi wa Nchi na Wananchi kati ya Barabara za mitaa za Dar na Barabara kuu baina ya Mikoa Kwa Mikoa na Nchi Kwa Nchi?

Bil.800 inaweza kujenga km 700 za Barabara za Lami za Mikoa na Kufungua uchumi mkubwa sana kuliko kutumia hizo pesa kuweka lami mitaa ya Dsm.

Screenshot_20230605-103142.jpg

Mikoa Ifuatayo Haina Lami zinazounganisha Mkoa Kwa Mkoa licha ya

Morogoro -Songea/Ruvuma
Morogoro -Njombe
Mbeya -Tabora
Mbeya -Singida
Katavi-Rukwa
Mpanda/Katavi- Kigoma
Tabora-Kigoma
Kigoma -Kagera
Arusha-Mara
Singida-Simiyu
Tabora-Rukwa
Morogoro -Lindi
Tanga -Singida

My Take: Hivi kweli Watunga sera Wetu wako serious na Vipaombele vyenye maslahi Kwa Nchi?
 
Muelewe jamani huo ni mradi wa world bank kwa ajili ya kuboresha majiji makubwa africa kama dar es salaam , Nairobi, Kinshasa, kampala na n.k hapo serikali ichague iombe pesa za kuboresha dar au iache mradi upite kwa wengine.

serikali imefanya jambo jema sana na hongera zao..
 
95% mapato yanayoendesha nchi yapo Dar ....hilo Usisahau
Nilijua itakuja na huu ujinga..

Sasa ni hivi,kwanza aliyekudanganya kwamba ni Asili 95 ni nani?
Pili Hadi inafikia Dar inazalisha zaidi ni Kwa sababu kama.hizi za kujaza na kupendelea Kwa miundombinu na Huduma so hakuna muujiza..

Mwisho wewe Kwa akili Yako unaona hiyo pesa ilijenga Barabara za mitaa Dar zitazalisha kushinda kama ingejenga barabara kubwa za Kuunga Mikoa na Mikoa?
 
Barabara zinafungua uchumi na mazingira bora ya biashara na uchumi ukifunguka mapato yanaongezeka na mapato yakiongezeka miundombinu inajengwa.

Dar es salaam ni kitovu Cha biashara na uchumi wa Taifa letu na kama nilivyosema barabara zinafungua fursa za biashara basi kuna uwezekano mkubwa mapato yakaongezeka kwa kujenga barabara Dar es aalaam na kusaidia kupata mapato ya kujenga sehemu nyingine.

Kwa hiyo kulingana na swali lako, kwa kuzingatia nadharia usawa na haki naweza kusema sio sawa ila kwa kuzingatia nadharia za uchumi ni sawa, kwa maslahi mapana ya Taifa nasimama na nadharia za kiuchumi.
 
Huo siyo upendeleo tu! Bali pia ni mgawanyo wa hovyo sana wa raslimali. Maana kuna barabara nyingi tu muhimu zinazo ongoza kwa uzalishaji wa malighafi/mazao mbalimbali ya biashara na chakula, hazina barabara za kupitika msimu wote ndani ya mwaka.

Mfano mzuri ni barabara ya Kilombero Ifakara Mlimba, Mahenge, Malinyi, nk. Zinazalisha mpunga kwa wingi! Lakini barabara ni za vumbi.

Kuna barabara ya Mafinga Sawala Mgololo! Nyololo Igowole Mtwango Mgololo; kuna malighafi za mbao, kunalimwa chai, kuna viwanda vya chai, mbao, karatasi, nk. Lakini barabara zake ni za vumbi!
 
muel

muelewe jamani huo ni mradi wa world bank kwa ajili ya kuboresha majiji makubwa africa kama dar es salaam , Nairobi, Kinshasa, kampala na n.k hapo serikali ichague iombe pesa za kuboresha dar au iache mradi upite kwa wengine..

serikali imefanya jambo jema sana na hongera zao..
Toa utoto hapa,WB walikuja kuwapa Msaada au Watunga sera ndio walipeleka Hilo andiko Kwa WB?

Kwa.nini hawakupeleka proposal kwenye hizo Barabara kuu za Mikoa Ili iwe na Tija zaidi?
 
Ndio maana tunataka serikali za majimbo huo ni uhuni wa CCM yaani mkoa unaozalisha mahindi ndio mkoa wenye njaa that is nosense
Na hapo Bado Kuna BRT,Tarura, TanRoads na Mapato ya ndani ya Halmashauri wote hao wanajenga Barabara Dar tuu..

Hii sio sawa,lazima tujue tunachokifanya.
 
Toa utoto hapa,WB walikuja kuwapa Msaada au Watunga sera ndio walipeleka Hilo andiko Kwa WB?

Kwa.nini hawakupeleka proposal kwenye hizo Barabara kuu za Mikoa Ili iwe na Tija zaidi?
eeh mkuu aya basi peleka wewe hizo sera huko WB za kuomba pesa za barabara za mikoani..
 
Barabara zinafungua uchumi na mazingira bora ya biashara na uchumi ukifunguka mapato yanaongezeka na mapato yakiongezeka miundombinu inajengwa.

Dar es salaam ni kitovu Cha biashara na uchumi wa Taifa letu na kama nilivyosema barabara zinafungua fursa za biashara basi kuna uwezekano mkubwa mapato yakaongezeka kwa kujenga barabara Dar es aalaam na kusaidia kupata mapato ya kujenga sehemu nyingine.

Kwa hiyo kulingana na swali lako, kwa kuzingatia nadharia usawa na haki naweza kusema sio sawa ila kwa kuzingatia nadharia za uchumi ni sawa, kwa maslahi mapana ya Taifa nasimama na nadharia za kiuchumi.
Ujinga huu ndio naukataa,Kwa Bajeti za TanRoads,Tarura,BRT na Own Source hazitoshi Kwa Dar Hadi kutoa upendeleo Kwa kiasi hicho?

Pili Kwa akili Yako ipi itakuwa na impacts kubwa kwenye uchumi kama kutumia hizo pesa kufungua uchumi wa Mikoa au kujenga lami za mitaa ya huko kisemvule?

Tumieni akili basi,Dar haikushushwa ikawa kitovu Cha uchumi Bali upendeleo wa hivi ndio unasababisha inakuwa kitovu,huko Mikoani Kuna uchumi mkubwa kuliko hata Dar ila hakuna miundombinu wezeshi .
 
Nimejaribu Kujiuliza na kufikiria pengine Kwa akili yangu finyu kwamba inawezekanaje Kutenga zaidi ya Bilioni 800 Kwa Ajili ya kujenga Barabara za Mitaa za Jiji la Dar wakati Kuna Barabara Kuu za Kuunganisha Mikoa na Mikoa na Nchi na Nchi jirani Bado Zina mavumbi,Hii ni sawa? Haiwezi Kuwa ni Upendeleo?

Nafahamu Jiji la Dar linahitaji Barabara za mitaa lakini Kwa nini hatuna Vipaombele?

Swali la Kujiuliza ,Kipi kina impacts kubwa kwenye uchumi wa Nchi na Wananchi kati ya Barabara za mitaa za Dar na Barabara kuu baina ya Mikoa Kwa Mikoa na Nchi Kwa Nchi?

Bil.800 inaweza kujenga km 700 za Barabara za Lami za Mikoa na Kufungua uchumi mkubwa sana kuliko kutumia hizo pesa kuweka lami mitaa ya Dsm.
View attachment 2646608

Mikoa Ifuatayo Haina Lami zinazounganisha Mkoa Kwa Mkoa licha ya

Morogoro -Songea/Ruvuma
Morogoro -Njombe
Mbeya -Tabora
Mbeya -Singida
Katavi-Rukwa
Mpanda/Katavi- Kigoma
Tabora-Kigoma
Kigoma -Kagera
Arusha-Mara
Singida-Simiyu
Tabora-Rukwa
Morogoro -Lindi
Tanga -Singida

My Take
Hivi kweli Watunga sera Wetu wako serious na Vipaombele vyenye maslahi Kwa Nchi?
 
Attachments

  • E6965110-38F7-4F20-AA72-FB6D902DF4C2.jpeg
    E6965110-38F7-4F20-AA72-FB6D902DF4C2.jpeg
    23 KB · Views: 8
Barabara zinafungua uchumi na mazingira bora ya biashara na uchumi ukifunguka mapato yanaongezeka na mapato yakiongezeka miundombinu inajengwa.

Dar es salaam ni kitovu Cha biashara na uchumi wa Taifa letu na kama nilivyosema barabara zinafungua fursa za biashara basi kuna uwezekano mkubwa mapato yakaongezeka kwa kujenga barabara Dar es aalaam na kusaidia kupata mapato ya kujenga sehemu nyingine.

Kwa hiyo kulingana na swali lako, kwa kuzingatia nadharia usawa na haki naweza kusema sio sawa ila kwa kuzingatia nadharia za uchumi ni sawa, kwa maslahi mapana ya Taifa nasimama na nadharia za kiuchumi.
Ujinga huu ndio naukataa,Kwa Bajeti za TanRoads,Tarura,BRT na Own Source hazitoshi Kwa Dar Hadi kutoa upendeleo Kwa kiasi hicho?

Pili Kwa akili Yako ipi itakuwa na impacts kubwa kwenye uchumi kama kutumia hizo pesa kufungua uchumi wa Mikoa au kujenga lami za mitaa ya huko kisemvule?

Tumieni akili basi,Dar haikushushwa ikawa kitovu Cha uchumi Bali upendeleo wa hivi ndio unasababisha inakuwa kitovu,huko Mikoani Kuna uchumi mkubwa kuliko hata Dar ila hakuna miundombinu wezeshi .
 
eeh mkuu aya basi peleka wewe hizo sera huko WB za kuomba pesa za barabara za mikoani..
Sina maamuzi Mimi siwezi kufanya huo ujinga Mzee..

Impacts ya hiyo pesa kwenye uchumi ingekuwa kubwa kama zingetumika Kuunganisha Barabara kuu badala ya kujenga Barabara za mitaa hapo Dar..

Lazima tuwe na Vipaombele vyenye Tija na pia tusimame na kuikamilisha sera ya kuunganisha Mikoa Kwa Mikoa ,Nchi na Nchi na Wilaya Kwa Wilaya ndio tuhamie huko kwenye mitaa..
 
Ujinga huu ndio naukataa,Kwa Bajeti za TanRoads,Tarura,BRT na Own Source hazitoshi Kwa Dar Hadi kutoa upendeleo Kwa kiasi hicho?

Pili Kwa akili Yako ipi itakuwa na impacts kubwa kwenye uchumi kama kutumia hizo pesa kufungua uchumi wa Mikoa au kujenga lami za mitaa ya huko kisemvule?

Tumieni akili basi,Dar haikushushwa ikawa kitovu Cha uchumi Bali upendeleo wa hivi ndio unasababisha inakuwa kitovu,huko Mikoani Kuna uchumi mkubwa kuliko hata Dar ila hakuna miundombinu wezeshi .
Uwepo wa bandari kubwa Dar es salaam nio sababu kuu ya kuwa kitovu Cha uchumi, fuatilia umuhimu wa bandari kwa uchumi. Kwa sifa hii ya uwepo wa bandari ni ukweli isiopingika dar ni zaidi ya mikoa mingine.

Kisemvule sio Dar es salaam lakini umuhimu wa umuhimu wa barabara za mitaa ni mkubwa kwa sababu ya uzalishaji unaotegemea barabara hizo. Kujenga barabara za mikoa Tena katikati ya mapori na pengine huo mkoa consumption ya watu ni ndogo sana sometimes in non economical
 
Back
Top Bottom