Je, kutokuwepo kwa rabsha za tumbuatumbua ndio ishara kuwa Rais Magufuli amemaliza kero zote za wananchi? Mbona kama mambo ndivyo sivyo?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,553
2,000
Ndugu wana JF humu ndio mahala pa kuhoji kila jambo linalotuhusu. Je, serikali awamu ya tano imekamilisha kutatua kero zetu?

Alipoingia madarakani rais Magufuli alianza kwa kasi ya kutumbua wote ambao walionekana ni wabadhirifu, wasiowaadirifu ambao walionekana kuwaletea kero wananchi kisha kusababisha wananchi kutokupata maendeleo.

Tulishuhudia watu wakitumbuliwa na wananchi wakishangalia mithili ya mhalifu akisurubishwa.

Leo hii Rais Magufuli ameanza ngwe yake ya pili ili amalize utawala wake. Je, ameshaiweka sawa Tanzania aliyoikuta imechafuka? Kwamba hakuna ufisadi, kero za wananchi zimetatuliwa zote,shule hazina upungufu wa madarasa, wananchi hawana kero ya maji. Pia ufisadi uliosababisha haya kutokea ameufuta.

Kama ndio hivi mbona Chato watu wamepiga Bil 3.6? Kama serikali yake ipo makini mbona hata kijijini kwao kumepigwa bil 3.6?

Je, huko Mwanza? Dar es Salaam? Iringa?

Kwa ufupi bado kuna tatizo kubwa na mzee baba hajafanikiwa.

IMG_20210302_114417_7.jpg
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,378
2,000
Amedhibiti vyombo vya habari ili asiwajibike, bali atekeleze yale tu ayatakayo. Sehemu kubwa ya aliowatumbua ni wale aliokuwa hawapendi, na vidagaa. Lakini ufisadi bado upo, bali hakuna chombo cha habari kinaweza kureport maana kitachukuliwa kama ni kukosa uzalendo, na kinaweza kufungiwa muda wowote.
 
Kama ni kweli, basi hatupo salama.
 
Wewe huwa ni mhafidhina. Kuhusu ukweli kuwa ufisadi upo nakuunga mkono.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom