Elections 2010 Je kupata kura baada ya kampeni (CCM au vyama vingine) na kuingia bungeni ni nini?

venividivici

Member
Dec 30, 2006
19
0
Nina anadika kama Mtanzania ninayeipenda sana nchi yangu na ambaye nimekuwa na kiu sana ya kuona matokeo ya kuwa na vyama vingi vya siasa. Kwasababu vyama vingi vya siasa vinawezesha kuwa na mchakato (badala ya kuwa na ya aina moja) wa mawazo ambao utaiwezesha nchi kuwa na maendeleo.

Kwa maana hii. Napendelea sana vyama vya upinzani vichukuwe madaraka ili kuiweka sawa CCM. Lakini sioni kama vyama vya upinzani vipo tayari kuiweka sawa CCM.

Kilichotokea kwenye uchaguzi huu wa 2010 ni kwamba kwasababu ya kero wanazoziona toka chama tawala cha CCM, wananchi wengi walio pigia kura vyama vya upinzani, wamefanya hivyo kwasababu tu ya jazba na kutopendezeshwa na CCM. Hakuna wapinzani ambao wana mkakati tofauti na wa CCM ambao utaleta maendeleo kwa mwananchi wa kawaida - Jamani vijijini kuna tabu.

Wabunge wengi wa upinzani wameshinda katika majimbo yao kwa vile wamekuwa mahiri wa ku-ishambulia CCM "attack politics". Lakini ukiwakaisha chini hao wabunge walio zoea hayo mashambulizi ukawaambia haya hebu tupange mipango lukuki ya maendeleo nakwambia hakuna hata mmoja.

Kushinda kwa wapinzani hasa CHADEMA hakuna maana kuwa hawa CHADEMA AU CUF wapo tayari kuiweka sawa CCM kwa maana ya mipango mipya (utendaji vitendo mbali ya malumbano yasiyo na maana na kunyoosheana vidole.

Simaanishi kwamba kukosoana kusiwepo kwenye politics za Tanzania lakini in terms of percentage kukosoana kuwe 20% na utaendaji kazi utakao leta maendeleo 80%. Tatizo nilionalo ni kwamba wabunge wachache sana kote upinzani na CCM wana kaliba ya na moyo wa kutenda kazi. Inasikitisha sana kuwa hata wale kwenye chama tawala waliokuwa mawaziri walikuwa mawaziri jina tu.

Tanzania ina kila kitu sio tu extractive resources, but its location (near the sea, climate, scenary and landforms, fertile soil) lakini bado ni masikini, hasa huku vijijini. Yote hii ni kwasababu viongozi sidhani wanajua kuongoza ni nini au kutatua matatizo ni nini. Maneno ni mengi. Utendaji mchache na sehemu nyingine hakuna hata utendaji.

Furaha kubwa toka upande wa upinzani ni kwavile wameishinda CCM lakini sio kwamba wana ari na taadhima ya kutenda na kuleta mabadiliko. Ndio kuingia bungeni ni hatua ya kwanza, lakini jiulize je wabunge wetu wa CCM na wa vyama vingine wana muda na uwezo wa kuisoma miswaada, kuielewa na kuifanyia kazi au wanafungua midomo yao kupokea na kusubiri marupu rupu yanayoendana na cheo hicho cha ubunge au pengine uwaziri?.

Uzuri ni kwamba wananchi wa Tanzania wameanza kupata mwamko. Kama tunavyoona ambavyo mawaziri wa serikali ya CCM walivyo galagazwa kwasababu wamejisahau. Kwahiyo ujumbe mkubwa nioao utoa kwa washindi wa ubunge ni kwamba adhaniaye amesimama aangalie asianguke. Tena kuanguka kubaya kweli baada ya kuzoea marupurupu kwasababu yataondoka.

Ahsante.

Veni Vidi Vici
 
Back
Top Bottom