Je kuongeza kodi kwa wafanyakazi (PAYE) kutamkwamua mfanyakzi au ndiyo maumivu kwao?

kwa hiyo mgomo wa madaktari umepewa tiketi rasmi
 
kwa hiyo mgomo wa madaktari umepewa tiketi rasmi

Mgomo wa madaktari hauhusiani na kodi za magari. Badala ya kodi watapatiwa kila mmoja VX 8 walipe shillingi 10,000/= kila mwezi. Wakifa kabla ya deni kwisha wanasamehewa.
 
Serikali inayo tegemea kukusanya kodi kutoka kwa wanywaji ni mfilisi kabisa wakisusa kunywa serikali itashindwa kujihudumia yenyewe bure kabisa.
 
kila kilichotangazwa ktk bajeti ni maumivu. Unapotenga 30% ya bajeti kwenda kwenye
uzalishaji na hakuna viwanda ila huduma tu. Ngoma ipo kwa wasomi wetu. watakwenda wapi
wanasayansi wetu. Ambao siku hizi wanapewa mitihani rahisi ili wafaulu vizuri zaidi ya 'arts'?

Kilimo chetu hakijapewa kipaumbele cha umwagiliaji kama alivyokuwa akipiga kampeni rais wetu.
Kodi nyingi zimeongezwa lakini si uzalishwaji uliotazamwa. Watoto wetu watafanya nini? Mikoa
kibao. Matumizi juu sana, uzalishaji kidogo.Bajeti tunashauri iwe ya mikoa kushindana na kupewa tuzo pia.
 
Hivi kuna watu bado wanapata mshahara wa 170000/=? unatosha nini sasa .....Mtu yeyote anayepata mshahara wa zaidi ya 1m anakatwa PAYE sawa sawa na miezi 3.4 kwa mwaka mzima,wakati wengine wote kutoa kima cha chini wanaifanyia serikali kwa muda wa miezi 2. Hivyo hiyo nafuu haijasaidia kitu chochote
 
PAYE ni exponential function hivyo haiwezi kuwa sawa kwa wote hilo lipo miaka yote wenye mishara mikubwa PAYE ni kubwa kuliko wale wa chini.

kumbuka haya makato yanakatwa kwa asilimia hivyo maumivu ni yale yale hata wenye mishahara mikubwa ni maumivu matupu hasa kwa sekta binafsi tunaumia sana
 
Sasa ikiongezwa asilimia 30% inakuwaje? kwa sasa hivi nalipa PAYE 26% ina maana kodi yangu itakuwa more than 40%, weka VAT, kila kitu ninachonunua kina VAT, ina maana nitalipa serikalini kodi almost 60%, hapo sijakatwa 10% ya NSSF. Nabakiwa na nini?? Wafanyakazi lets fight for our rights. This is too much. Yale matrilioni yanayosamehewa wameongeleaje?
 

Hata mimi sijwamwelewa huyu mleta mada. Nimeisoma bajeti yote ambayo iko hapa jamvini sijaona mahali waziri wa fedha ametangaza kuongeza PAYE kwa wafanyakazi. May be nimeruka kama anacho kipengele hicho atuwekee hapa vinginevyo mods waondoe huu uzi maana unapotosha watu.
 
Hivi wabunge na Rais wanalipa kodi?? inawezekana hapana, Watakuwa na ubavu wakutetea wafanyakazi? Its high time hili liingie kwenye katiba. Kwa nini watu wengine wasilipe kodi-PAYE. Kwani hawatumii services za nchi hii? Kwa nini wafanyiwe na wengine???
 

hata mimi namshangaa sijui kaitoa wapi. mathalani mwenye kima cha chini cha Tsh 170,000 PAYE yake ni Tsh 0 sasa hiyo 30% inatoka wapi?
 
pia mimi nimeelewa kuwa kiwango kati ya 135000-170000 haitakatwa kodi. kwangu naona kama ni mchezo wa kuigiza kwa sababu serikalini anaepata kiwango hicho ni yule asie kuwa na ujuzi na kazi anayoifanya kwani kuanzia certificate mshara ni zaidi ya kiwango hicho.
 

wewe ndio unataka kupotosha watu.

Hiyo statement imewekwa kuficha hali halisi. Kama unataka ukweli subiri muswada uone moto wake.

Hiyo sentensi haina tofauti na ile inayosema mfanyakazi analipa kodi 15% wakati ki-ukweli kuna wanaolipa 30% ya mshahara.

Kwa hiyo yale madai ya kupunguza kodi toka 15% hadi 9% haimaanishi kwamba wafanyakazi wote wanalipa kodi ya 15% kwa sasa ingawa hakuna anayetaka kusema hilo kwamba kuna wafanyakazi wanalipa 30% ya mapato yao ya mwezi
 
mjimpya yuko sawa. Mleta uzi hakujua anachoongelea zaidi ya kupotosha watu humu. Kama hukuelewa ungeuliza badala ya kupotosha wewe mleta mada.
 
Hata mimi sijwamwelewa huyu mleta mada. Nimeisoma bajeti yote ambayo iko hapa jamvini sijaona ............mods waondoe huu uzi maana unapotosha watu.
Kama wewe ni mfanyakazi subiria mshahara wa mwezi wa 7 ndio utamwelewa huyo mleta mada.
 
Huu ni wizi wa mchana kweupe.Haingii akilini mwangu kwamba wachangiaji wakubwa wa kodi Tanzania wawe wafanyakazi,wakati tuna makampuni makubwa ya uchimbaji wa madini,viwanda,makampuni ya simu nk.This is typical of freemason governments.Kutoa dimbwini kupeleka baharini. kupeleka
 
Mkuu KODI ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote, mgogoro pekee upo kwenye jinsi gani kodi inatumiwa na taifa husika. Tatizo la TZ ni kodi kupelekwa sehemu kusiko sahihi.

kodi ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa lakini logic hapa ni unapandisha mshara kisha unapandisha na kodi, kwa asiejua hesabu atafurahi mshahara kuongezeka lakini mwisho wa siku kama net pay ilikuwa ni laki tatu itabaki laki tatu ileile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…