Je kuongeza kodi kwa wafanyakazi (PAYE) kutamkwamua mfanyakzi au ndiyo maumivu kwao?

ndg kama hujaelewa ni vizuri kuuliza kuliko kuwapotosha wengine.
Amepunguza kima cha chini cha kutoza kodi kutoka 135k to 170k, hii ina maana kila mtu atapata unafuu wa kodi kwa kiasi. Kama unafahamu jinsi paye inavopigwa utakuwa umenielewa.

Acheni kupotosha watu jamani.


  1. "Adjust PAYE threshold as a result of enhancement of salary scales from Tshs 135,000 to Tshs 170,000"
Mbona haya maneno na kauli zinaonekana kama za mwenyewe ma padlock kilevi?
 
kwamba zamani ilikua kama mshahara wako ni 1 hadi 135,000 haulipi kodi, ikizidi 135,000 unalipa kodi kwa kile kinachozidi, sasa wameongeza hiki kiasi ambacho hatutakilipia kodi, kiwango kimeongezeka kutoka 135,000 hadi 170,000


Mkuu uswe, heshima mbele.

Je kima cha chini (KCC) cha mshahara itakuwa ni sh ngapi kwa sasa???
Kwa maana kama kima cha chini kitakuwa 170,000 basi hakuna releaf yeyote maana tokea miaka yote kcc haikatwi kodi. Hivo ni maigizo tu bora asingetamka.
 
Jamani tunachambua budget tunayoijua au tunabuni au kulalama tu? nilichoelewa mimi hakuna kodi kodi iliyoongezwa ili kilichobadilika ni kuwa mshahara utakaokatwa kodi p.a.ye ni ule unaoanzia 170,000/- awali mishahara iliyokuwa inakatwa kodi p.a.ye ni ile iliyokuwa inaanzia 135,000/- hii ni ahueni kidogo kwa wenye mishahara ya chini!!
 
Msamaha upo kwa wale wa kuanzia 170 kwenda 1. Wengine hunufaika kama percentage imeshuka. Kwa kuwa haijashuka, basi hali yetu ni twte sana.
 
Bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha inaonesha kuwa baada ya ya serikali kuongeza mishahara(kwa wafanyakazi wake wa serikali)imerevenge kwa kuongeza kodi ya mishahara hii inamaana kuwa mshahara uliongezwa kwa kiasi kidogo ila kodi imeongezwa kwa takribani 30% ss maana yake kuwa mshahara ulioongezwa ni kiini macho tu na kamwe haimsaidii mfanykazi,je ww mtazamo wako ukoje?



Nawakilisha!

Kodi ipi iliyoongezwa kwa mfanya kazi? mimi nilisikia kuwa kima cha chini cha kukatwa kodi kimeongezwa kutoka 135,000 mpaka 170,000. Jee, kuna unalolijuwa kwa siri?
 
Bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha inaonesha kuwa baada ya ya serikali kuongeza mishahara(kwa wafanyakazi wake wa serikali)imerevenge kwa kuongeza kodi ya mishahara hii inamaana kuwa mshahara uliongezwa kwa kiasi kidogo ila kodi imeongezwa kwa takribani 30% ss maana yake kuwa mshahara ulioongezwa ni kiini macho tu na kamwe haimsaidii mfanykazi,je ww mtazamo wako ukoje?



Nawakilisha!
Mawazo wanayotuwazia CCM si mawazo ya amani na upendo, vita ya kiaina
 
Kama kima cha chini kimepanda kutoka 135,000 mpaka 170,000 maana yake mtu anayelipwa mshahara kuanzia shs 1 mpaka 170,000 hatakatwa kodi.
Na kwa mtu kwa mfano analipwa 1,000,000 pesa atakayotakiwa kuilipia kodi ni 830,000. Kwa maana ya unachukua (1,000,000 - 170,000) yaani lazima utoe kile kima cha chini kisicholipiwa kodi ndio upige hiyo % ya PAYE.
 
Kama kima cha chini kimepanda kutoka 135,000 mpaka 170,000 maana yake mtu anayelipwa mshahara kuanzia shs 1 mpaka 170,000 hatakatwa kodi.
Na kwa mtu kwa mfano analipwa 1,000,000 pesa atakayotakiwa kuilipia kodi ni 830,000. Kwa maana ya unachukua (1,000,000 - 170,000) yaani lazima utoe kile kima cha chini kisicholipiwa kodi ndio upige hiyo % ya PAYE.

Hapo tunaenda sawa then hiyo % unaweza kuitolea maelezo ngapi hadi ngapi ni asilimia kadhaaa mkuu
 
ishiiii!!! Sa mwenye uelewa kidogo atueleweshe maana nimesoma page mbili za thread hii naona ni blah! Blah! Tu mnabishana mnachobishania hakieleweki ni hivi JE KIMA CHA CHINI KIMEPANDA? NA JE ONGEZEKO LA MSHAHARA KA LIPO NI LA ASILIMIA NGAPI? Na JE P.A.Y.E IMEPUNGUZWA AU IMEONGEZWA? Hayo nahisi ndio wengi tunataka kujua mengine ni mbwembwe
 
Kikwete alisema hataki kura za wafanyakazi sasa nawauliza mlimpa za nini ?

Ukisikia kujipendekeze ndio huko, kwakweli wafanyakazi mlio mpigia kura mlijipendekeza tu wakati yeye hataki urafiki na nyinyi sasa anawaonyeshea laivu kuwa siwataki mnanitakia nini.
 
Nijuacho,
zamani ilikuwa hadi 135,000 tax free ambayo sasa ndo imeongezwa hadi 170,000.
Kuanzia 500,000 kodi ilikuwa ni 120,000. Ile ziada ya laki tano, ndo unailipia kodi ya 30%
mfano mwenye mshara wa laki 6 kodi yake inakuwa ni
120,000 kwa ile laki tano plus 30% ya laki moja ya ziada.
 
Sasa kwa mpango huo hivi huwa mnarudi na kiasi gani cha pesa kwa wake zenu? Dah! Serikalini kuzuri ila wenyewe mnasema!
 
Tume ya Katiba sijakataa kulipa kodi ila wafanyakazi wanakamuliwa kweli maana ukifanya tathmini ya kawaida makato ya kodi kwa wahadhiri wa chuo kikuu kimoja unawalipa waalimu wa primary zaidi ya 20,wafanyabiashara wanaongoza kwa kukwepa kulipa kodi ila kodi kwa wafanyakazi iko juu sana na bado wameongeza hapa mfanyakazi atajikwamuaje?

Mkuu mfanyakazi akijikwamua sana kwa kuwa na mshahara mkubwa atakuwa na jeuri. Nadhani hii ni falsafa ya watawala wetu. Wanafikiri wakikubana upate tu hela ya kula utakuwa submisive. Anyway muda utafika wafanyakazi watajua kuwa hawana cha kupoteza. Kuwa mfanyakazi Tz ni utumwa uliokithiri. Unakamuliwa kodi hata salary slip unaogopa kuiangalia
 
Nijuacho,
zamani ilikuwa hadi 135,000 tax free ambayo sasa ndo imeongezwa hadi 170,000.
Kuanzia 500,000 kodi ilikuwa ni 120,000. Ile ziada ya laki tano, ndo unailipia kodi ya 30%
mfano mwenye mshara wa laki 6 kodi yake inakuwa ni
120,000 kwa ile laki tano plus 30% ya laki moja ya ziada.

Tukiamua kuwa wakweli huu tutauita UNYANG'ANYI. Ni muhimu kulipa kodi ila sio kubwsa kiasi hiki. What is laki sita hadi ukate 30%.
 
Wafanyakazi, juwapeni kura zetu Chadema ili watupiganie, hatuna lolote kwa CCM hapa. Fikisha ujumbe huu kwa mfanyakazi mwenzio. Tulitegemea wangepunguza mdudu huyu wa Pay as yu earn na hamna lolote lililofanywa.
 
Naomba kusaidia kidogo hili maana naona upotoshaji umekuwa mkubwa.

Kima cha chini kukatwa kodi ni 170,000 kutoka 135,000 ya zamani.wakaofaidika ni wale wa kima cha chini kabisa (chini ya 170,000) na chini ya 360,000. nimeweka chini jedwali la namna ya kukokotoa ili ambae hesabu inapanda kidogo utaona namna kodi mpya itavyokuwa (hili ndio jedwali litalotumika hadi mwezi huu hivyo hapo penye 135,000 weka 170,000)
VIWANGO VYA KODI KWA WATU BINAFSI WAKAZI KUANZIA TAREHE 1/7/2010 Na.MAPATO YA KUTOZWA KODI
KWA MWEZI KIWANGO CHA KODI

1.Mapato yasiyozidi sh. 135,000/= (sasa 170,000)Hakuna Kodi

2.Mapato yanayozidi sh. 135,000/=(sasa 170,000)

lakini hayazidi sh. 360,000/=14% ya kiasi kinachozidi sh. 135,000/=

3. Mapato yanayozidi sh. 360,000/= lakini hayazidi sh.
540,000/=Sh. 31,500/= ongeza 20% ya kiasi kinachozidi sh. 360,000/=

4 .Mapato yanayozidi sh. 540,000/= lakini hayazidi

sh. 720,000/=Sh. 67,500/= ongeza 25% ya kiasi kinachozidi sh. 540,000/=

5. Mapato yanayozidi sh. 720,000/= Sh.

112,500/= ongeza 30% ya kiasi kinachozidi sh. 720 ,000/=
 
Back
Top Bottom