Je kuongeza kodi kwa wafanyakazi (PAYE) kutamkwamua mfanyakzi au ndiyo maumivu kwao?

Daah sasa kihama! tujipe pole sisi walalahoi! Maana watoa kushoto waweka kulia, ombilangu kwa viongozi wetu wa chadema tuliowapa dhamana kubwa ya kututetea na kulinda maisha yetu,tunaomba mtuwakilishe kwa kutoipitisha bajeti hii! Kwani sasa wanatuwaliza kabisa, hadi itakapo fika 2015 chamoto tutakuwa tumekiona.mungu watienguvu(makamanda) wote watakao kwenda kunena juu ya sisi maskini 71% tuliopo vijini tusiejua tofauti ya jana na leo,na ukawalaani wote watakao kwenda kunena kwa unafki juu ya bajeti hii (magamba). Amiina!
 
Bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha inaonesha kuwa baada ya ya serikali kuongeza mishahara(kwa wafanyakazi wake wa serikali)imerevenge kwa kuongeza kodi ya mishahara hii inamaana kuwa mshahara uliongezwa kwa kiasi kidogo ila kodi imeongezwa kwa takribani 30% ss maana yake kuwa mshahara ulioongezwa ni kiini macho tu na kamwe haimsaidii mfanykazi,je ww mtazamo wako ukoje?



Nawakilisha!

sidhani kama umeelewa

[FONT=Bookman Old Style, serif]Adjust PAYE threshold as a result of enhancement of salary scales from Tshs 135,000 to Tshs 170,000. [/FONT]
 
WanaJF
Naipenda nchi yangu na ndio maana nachangia kodi kila kina,japokuwa wajanja wanaifuja na kuyafanya maisha yangu na waTanganyika wenzangukuwa hoi, hiyo sijali kwni naishi kwamatumaini kuwa ipo siku na hasa 2015 nitapata unafuu wakati ukombozi utakuwaumepatikana.
Kila kikija kipindi cha bajeti ya Taifa kichwa huniumain-advance kwani huwa najiuliza safari hii wapi ninareruhiwa. Kwa bahati mbayanikiwa katika miche miche za kimaisha nimechelewa kumsikiliza Mkuu Mgimwa akitemacheche zake za mwaka 2012/2013, na hivyo nimeambulia kupata yale ya mwishoni.
Nashangaa kwanini (Shinikizo la Damu = BP) halijafanyamawasiliano nami nilipoona Pay As You Earn (PAYE) imeongezwa. Sitaki kusikiamikakati ya nchi kuongeza mapato au sitaki kusikia siasa za kupunguza matumizi (kwani najua huwa hawapunguzi).

Niachooomba wanaJF waliotuliza mizuka na kuisiliza ilehotuba watuambie hapa sehemu nyingine zipi tumeumizwa?

 
Kwenye uongezaji za gharama za simu, na kodi za magari

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
hapa mnatuchanganya jamani,Tunaomba anaejua PAYE inavyopigwa atusaidie.tuelewe maana ya hilo ongezeko.
 
Nashauri wenye uchungu na wananchi waikatae bajeti ,wabakie wachumia tumbo na kauli mbiu yao ya ndiyoooooo! Lakini wajue cha moto 2015 watakiona kwani tumeshajua kuwa wabunge wote wa CCM wanaenda bungeni kutetea CCM na sio wananchi,kwa hiyo tutaona kati ya wananchi na magamba nani kawapeleka bungeni
 
PAYE ni exponential function hivyo haiwezi kuwa sawa kwa wote hilo lipo miaka yote wenye mishara mikubwa PAYE ni kubwa kuliko wale wa chini.

Whatever the case, wenye mishahara midogo ndio wanaoumia zaidi na ndio wengi. Solution MGOMO!!
 
Kama sikosei alichosema ni kuongeza msamaha wa kodi kutoka wale wanaopokea kima cha chini cha sh 130,000 mpaka wale wanaopokea sh 170,000 kwa mwezi.Yaani hawatalipa kodi kabisa.
 
PAYE haijaongeza, iko vilevile wamepandisha tu kile kiwango anbacho hakikatwi kutoka 135,000 hadi 170,000 sasa naona inawachanganya watu wanadhani ni PAYE inaongezeka, kimsingi kama income yako ni fixed basi kodi itapungua lakini kidogo sanaaaa kwa sababu taxable amount itapungua kwa sh 35,000
 
ndg kama hujaelewa ni vizuri kuuliza kuliko kuwapotosha wengine.
Amepunguza kima cha chini cha kutoza kodi kutoka 135k to 170k, hii ina maana kila mtu atapata unafuu wa kodi kwa kiasi. Kama unafahamu jinsi paye inavopigwa utakuwa umenielewa.

Acheni kupotosha watu jamani.


  1. "Adjust PAYE threshold as a result of enhancement of salary scales from Tshs 135,000 to Tshs 170,000"

MJI MPYA wale wanaopata mshahara chini ya laki 3 ndo wananufaika na hiyo kitu but PAYE (PAY AS YOU EARN)Kadri kwa wenye mshahara zaidi ya laki 3 sahau hiyo kitu kadri mshahara unavyopanda ndiyo makato yanaongezeka,hiyo 135k na 170k ndugu yangu ni matokeo ya jumla,makato ya kodi kwa ss hivi ni 20% ss kuanzia julai kama alivyosema itakua inakaribia 30% ss ukifanya calculation hapo sijui kama hiyo uliyosema hapo juu inaingia akirini
 
sidhani kama umeelewa

Adjust PAYE threshold as a result of enhancement of salary scales from Tshs 135,000 to Tshs 170,000.

Hebu funguka zaidi hapo hueleweki,wenye 135,000 mshahara navyojua hawakwati kodi hadi zaidi ya laki 3 ndo unakatwa kodi ss ww hiyo hesabu yako umeitoa wapi ya laki na 35?
 
ndg kama hujaelewa ni vizuri kuuliza kuliko kuwapotosha wengine.
Amepunguza kima cha chini cha kutoza kodi kutoka 135k to 170k, hii ina maana kila mtu atapata unafuu wa kodi kwa kiasi. Kama unafahamu jinsi paye inavopigwa utakuwa umenielewa.

Acheni kupotosha watu jamani.


  1. "Adjust PAYE threshold as a result of enhancement of salary scales from Tshs 135,000 to Tshs 170,000"


Hili ni tatizo la watu wengi hasa ambao hawajui. Kama kiwango kimepanda kutoka 135,000.00 - 170,000.00 tax free ni neema kwa mfanyakazi kuwa kodi imepungua kidogo.
 
Hakuna eneo kwenye budget inayoonyesha nafuu kwa mlala hoiM kilichofanyika ni kama maelezo ya mganga wa chienyeji bAada ya kupiga ramli yaani futi kafutifuti tu.
 
Kwenye uongezaji za gharama za simu, na kodi za magari

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Kodi za magari hazijaongezwa, nilivyosikia mimi ni kuwa miaka ya magari chakavu imepunguzwa kutoka 10 hadi minane, maana yake ni kuwa kama kwa sasa tunalipia kodi ya uchakavu 20% kwa magari ya kuanzia miaka 10 na kuendelea, kwa sasa ni miaka 8 na kuendelea. Nadhani hii ni nzuri sana, mwakani wafanye 5 tu.

Na kingine ni baadhi misamaha ya kodi kwa magari imeondolewa. Nadhani hapa watakuwa wameumia madaktari, waalim na Watanzania wanaorudi baada ya kuishi nje, bunge linavyoendelea tutaelewa zaidi.
 
Serikali ya ccm imekuwa binafsi sana kuwatumia wasomi wasiokuwa ccm wakidhani wanawakomoa kumbe wanajikomoa wenyewe pale wanaposhindwa kufanya maamuzi yasiyoumiza upande mmoja ie wafanyakazi huku wafanya biashara wakipeta!
 
sidhani kama umeelewa

Adjust PAYE threshold as a result of enhancement of salary scales from Tshs 135,000 to Tshs 170,000.

Hebu funguka zaidi hapo hueleweki,wenye 135,000 mshahara navyojua hawakwati kodi hadi zaidi ya laki 3 ndo unakatwa kodi ss ww hiyo hesabu yako umeitoa wapi ya laki na 35?

kwamba zamani ilikua kama mshahara wako ni 1 hadi 135,000 haulipi kodi, ikizidi 135,000 unalipa kodi kwa kile kinachozidi, sasa wameongeza hiki kiasi ambacho hatutakilipia kodi, kiwango kimeongezeka kutoka 135,000 hadi 170,000

 
Back
Top Bottom