Wazo: Serikali ishushe PAYE kufikia single digit, kisha Serikali ifanye biashara ya kutoa mikopo kwa wafanyakazi kupitia BoT kufidia kodi itakayopotea

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,983
Mikopo ya wafanyakazi, ni biashara nzuri sana kwa taasisi za fedha hasa mabenki na biashara hii inachangia sana katika faida za mabenki ya kibiashara.

Hivyo, badala ya BOT kuendelea kukopesha mabenki ya kibiashara na kisha mabenki haya ndio yatoe mikopo kwa wafanyakazi, nashauri BOT waanze kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wafanyakazi na Serikali nayo ishushe PAYE, kodi ambayo inawezeza kufidiwa na biashara hii watayofanya BOT kwa riba ndogo.

Ukishusha PAYE, kunakuwa na faida mbili ambazo ni kuongeza take home ya mfanyakazi, na faida ya pili ni kumuongezea uwezo wa kukopa huyo mtumishi. Hivyo, BOT inaweza kufanya biashara na watumishi wengi zaidi kuliko ilivyo kwa mabenki hivi sasa.

BOT kama Benki kuu, naamini wana data zote kuhusu hii biashara, data wanazowe kuzitumia kufanya tathimini kuona kama wazo hili kitaalamu linawezekana na pia kama faida itayopatikana itaweza fidia kodi itayopotea kwa kushusha PAYE.

Najua kuna watu wanaweza kusema kuwa biashara hii itahatarisha mabenki binafsi, lakini mimi naamini italeta ushindanii na hivyo kusaidia kushusha riba ya mikopo na pia itafanya mabenk yafikirie kutafuta vyanzo vingine vya fedha na sio kutegemea kukopa fedha BOT ndio waje wazitumie kukopesha wafanyakazi.

Riba zikishuka, wafanyakazi watakopa zaidi na kwa maana hiyo, biashara hii itaongezeka na serikali itakusanya kodi zaidi (kama ilivyo kwa mabenki, BOT nao watalipa kodi TRA kwa kufanya hii biashara).

Wataalamu na watunga sera mtazame jambo hili au linalofanana na hili lengo likiwa ni kushua PAYE pasipo kuathiri mapato ya serikali.

Wafanyakazi nchi hii wanalipa kodi kubwa mno kupitia PAYE na bado wanalipa kodi nyingine ambazo ni indirect bila kusahau tozo zinazoletwa na serikali kila kukicha.

Mtu kodi kwa mwezi unakatwa 200,000, wengine 185,000, wengine 170,000 na wengine 300,000, n.k . Hizi kodi ni kubwa mno jamani kwa wafanyakazi huku mishahara ikiwa hailingani na gharama halisi za maisha.

Walifuta kodi ya kichwa, ila kwa kujua au kutokujua, kodi hii sasa anabebeshwa mfanyakazi wa nchi hii kupitia PAYE.
 
Iundwe taasisi nyingine isimamiwe na BOT,hiyo taasisi itoe mikopo kwa watumishi tu kwa kuzingatia Riba ya 3.5..mambo safi
 
Serikali haifanyi biashara inatoa huduma tu..

But wazo ni nzuri sana..
Ni kawaida kusikia watu wanasema serikali haifanyi biashara, ila ukweli ni kwamba serikali inafanya biashara kupitia baadhi ya taasisi zake zinazokusanya mapato kwa huduma wanazotoa kwa umma na hizo taasisi ndio hutoa gawio kwa serikali. Hii ni biashara tu kama biashara zingine ila badala ya kulipa kodi serikalini, wao wanalipa kinachoitwa gawio kwa serikali.
 
Mkuu umeongea points. Ila hiyo itakuwa mauaji ya kimbari kwa hawa wafuatao
CRDB
NMB
TPB
NBC
'IKWITI BENKI'

Na wemgine wengi
Mnapoona haya mabenki kila mwaka yanatangaza kupata faida za mabilioni, mjue wananchi tunachangia sehemu ya faida wanazopata kwa kukamuliwa kupitia riba za mikopo,bank charges, n.k.

Wakipata ushindani, watapunguza riba na hivyo wananchi nao watafaidika na mikopo na hapo hapo itasaidia kuleta maendeleo ya watu na si tu kukua na kuneemeka kwa haya mabenki na wafanyakazi wao wanaokopeshwa mikopo ya riba nafuu(riba za upendeleo)
 
Mikopo ya wafanyakazi, ni biashara nzuri sana kwa taasisi za fedha hasa mabenki na biashara hii inachangia sana katika faida za mabenki ya kibiashara.

Hivyo, badala ya BOT kuendelea kukopesha mabenki ya kibiashara na kisha mabenki haya ndio yatoe mikopo kwa wafanyakazi, nashauri BOT waanze kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wafanyakazi na serikali nayo ishushe PAYE, kodi ambayo inawezeza kufidiwa na biashara hii watayofanya BOT kwa riba ndogo.

Ukishusha PAYE, kunakuwa na faida mbili ambazo ni kuongeza take home ya mfanyakazi, na faida ya pili ni kumuongezea uwezo wa kukopa huyo mtumishi. Hivyo, BOT inaweza kufanya biashara na watumishi wengi zaidi kuliko ilivyo kwa mabenki hivi sasa.

BOT kama Benki kuu, naamini wana data zote kuhusu hii biashara, data wanazowe kuzitumia kufanya tathimini kuona kama wazo hili kitaalamu linawezekana na pia kama faida itayopatikana itaweza fidia kodi itayopotea kwa kushusha PAYE.

Najua kuna watu wanaweza kusema kuwa biashara hii itahatarisha mabenki binafsi, lakini mimi naamini italeta ushindanii na hivyo kusaidia kushusha riba ya mikopo na pia itafanya mabenk yafikirie kutafuta vyanzo vingine vya fedha na sio kutegemea kukopa fedha BOT ndio waje wazitumie kukopesha wafanyakazi.

Riba zikishuka, wafanyakazi watakopa zaidi na kwa maana hiyo, biashara hii itaongezeka na serikali itakusanya kodi zaidi (kama ilivyo kwa mabenki, BOT nao watalipa kodi TRA kwa kufanya hii biashara).

Wataalamu na watunga sera mtazame jambo hili au linalofanana na hili lengo likiwa ni kushua PAYE pasipo kuathiri mapato ya serikali.

Wafanyakazi nchi hii wanalipa kodi kubwa mno kupitia PAYE na bado wanalipa kodi nyingine ambazo ni indirect bila kusahau tozo zinazoletwa na serikali kila kukicha.

Mtu kodi kwa mwezi unakatwa 200,000, wengine 185,000, wengine 170,000 na wengine 300,000, n.k . Hizi kodi ni kubwa mno jamani kwa wafanyakazi huku mishahara ikiwa hailingani na gharama halisi za maisha.

Walifuta kodi ya kichwa, ila kwa kujua au kutokujua, kodi hii sasa anabebeshwa mfanyakazi wa nchi hii kupitia PAYE.
Ndo maana JF itaendelea kuwa jarida la watu wenye akili uzi mzuri sana huu hope utafanyiwa kazi
 
BOT watakuwa na uwezo wa kununua hiyo mikopo kwasababu wao watakauwa wanatoa mikopo kwa riba nafuu.

Serikalu haiwezi kushusha paye kwa sababu paye au kodi inatumika kulipia madeni ya mikopo wanayochukuwa, kwanza wataongeza makato!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom