Je kuongeza kodi kwa wafanyakazi (PAYE) kutamkwamua mfanyakzi au ndiyo maumivu kwao?

satellite

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
616
164
Bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha inaonesha kuwa baada ya ya serikali kuongeza mishahara(kwa wafanyakazi wake wa serikali)imerevenge kwa kuongeza kodi ya mishahara hii inamaana kuwa mshahara uliongezwa kwa kiasi kidogo ila kodi imeongezwa kwa takribani 30% ss maana yake kuwa mshahara ulioongezwa ni kiini macho tu na kamwe haimsaidii mfanykazi,je ww mtazamo wako ukoje?

Nawakilisha!

Watanzania acheni kujadili na kulalamika kwa kwa kufuata mkumbo, ukweli kuhusu PAYE ni huu hapa:

Kwa miaka mingi sasa serikali imewafutia kodi hiyo wafanyakazi wake wa kima cha chini kwa mwaka huu unaoishia June mfanyakazi anayepata kima cha chini cha 135,000/= halipi hiyo PAYE hivyo basi kuanzia July 1 mfanyakazi atakayelipwa kuanzia 170,000/= kushuka chini naye hata lipa paye,kwa wachambuzi wa mambo hii inaashiria kwamba kuanzia July kima cha chini kitakuwa 170,000/= hii ni sawa na ongezeko la 25.9%.

Hivyo nafuu hiyo ataipata kila mfanyakazi bila kujali analipwa sh ngapi kwa mwezi, ijapokuwa mwenye mshahara mkwubwa nafuu hiyo inaonekana ni ndogo.

Mfano mtumishi anayelipwa 300,000 kwa mwezi, ataktwa kodi kama ifuatavyo:

300,000-170,000=130,000, hii 130,000 ndiyo itakayopigiwa hesabu ya kodi kwa asilimia 18.

Hii ndiyo maana yake, japo kuwa hata wabunge walishindwa kuelewa
 
hakuna kilicho ongezeka zaidi ya uchulo tu ndugu yangu,ngoja tuone msimamo wa TUKTA na CHADEMA maana walikuwa wamesema kodi ipungue hadi asilimia 9.
 
Nimesikiliza hapo ila sikuelewa km wabunge wengi. Km huu ndio ufafanuzi wake basi ni kilio kwetu wafanyakazi kweli ni kiini macho.
 
Yan hapo watanzania tume ambiwa tutajuta. Kazi kwetu sasa.
 
Nimechoka na hawa wababaishaji tujaribu chadema
Mkuu wewe mpaka sasa hivi ulikuwa hujashtuka tu?magamba yameamua kutuua wabaki wao na ma V8 yao,hakiak Chadema ni faraja yangu hata kama napigika hivi ukombozi nauona mbele!!!
 
Nimesikiliza hapo ila sikuelewa km wabunge wengi. Km huu ndio ufafanuzi wake basi ni kilio kwetu wafanyakazi kweli ni kiini macho.

pole bwana km hukuelewa habari ndo hiyo maumivu kwa kwenda mbele
 
Bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha inaonesha kuwa baada ya ya serikali kuongeza mishahara(kwa wafanyakazi wake wa serikali)imerevenge kwa kuongeza kodi ya mishahara hii inamaana kuwa mshahara uliongezwa kwa kiasi kidogo ila kodi imeongezwa kwa takribani 30% ss maana yake kuwa mshahara ulioongezwa ni kiini macho tu na kamwe haimsaidii mfanykazi,je ww mtazamo wako ukoje?
Nawakilisha!

Mkuu KODI ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote, mgogoro pekee upo kwenye jinsi gani kodi inatumiwa na taifa husika. Tatizo la TZ ni kodi kupelekwa sehemu kusiko sahihi.
 
PAYE ni exponential function hivyo haiwezi kuwa sawa kwa wote hilo lipo miaka yote wenye mishara mikubwa PAYE ni kubwa kuliko wale wa chini.
 
Mkuu KODI ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote, mgogoro pekee upo kwenye jinsi gani kodi inatumiwa na taifa husika. Tatizo la TZ ni kodi kupelekwa sehemu kusiko sahihi.

Tume ya Katiba sijakataa kulipa kodi ila wafanyakazi wanakamuliwa kweli maana ukifanya tathmini ya kawaida makato ya kodi kwa wahadhiri wa chuo kikuu kimoja unawalipa waalimu wa primary zaidi ya 20,wafanyabiashara wanaongoza kwa kukwepa kulipa kodi ila kodi kwa wafanyakazi iko juu sana na bado wameongeza hapa mfanyakazi atajikwamuaje?
 
bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha inaonesha kuwa baada ya ya serikali kuongeza mishahara(kwa wafanyakazi wake wa serikali)imerevenge kwa kuongeza kodi ya mishahara hii inamaana kuwa mshahara uliongezwa kwa kiasi kidogo ila kodi imeongezwa kwa takribani 30% ss maana yake kuwa mshahara ulioongezwa ni kiini macho tu na kamwe haimsaidii mfanykazi,je ww mtazamo wako ukoje?

Nawakilisha!

ndg kama hujaelewa ni vizuri kuuliza kuliko kuwapotosha wengine.
Amepunguza kima cha chini cha kutoza kodi kutoka 135k to 170k, hii ina maana kila mtu atapata unafuu wa kodi kwa kiasi. Kama unafahamu jinsi paye inavopigwa utakuwa umenielewa.

Acheni kupotosha watu jamani.

  1. "Adjust PAYE threshold as a result of enhancement of salary scales from Tshs 135,000 to Tshs 170,000"
 
Back
Top Bottom