Je, Kuna watu wana experience haya mambo? Cognitive dreams

Hiyo hali ikikutokea...na maanisha kuota au kuwaza, roho kukuuma au moyo kwenda mbio then kitu kibaya kinatokea.
Cha kufanya hapo ni kupiga maombi ya kuzuia hicho kitu kibaya kisikuguse, au kukutokea.
Binafsi huwa inanitokea, nikipotezea inakula kwangu, nikiomba inapotea juu kwa juu au inaenda kwingine...sometimes huwa nawaambia wadau kwamba leo Kuna jambo litatokea....hapo nishipiga maombi.
Mungu bado anatupenda ingawa tuna mambo mengi.
 
Mimi ni mtu ambae niko positive sana mkuu, sijawahi kuwa na stress zozote juu ya maisha yangu and sijawahi kuogopa kitu kinachoitwa kifo.

Kitu unachotakiwa ujue hizo hisia huwa zinapita huwa zinanipitia hata nikiwa na watu tunapiga story, nakupa mfano mmoja, mwaka fulani wa nyuma kidogo nilikua ushagoo na tulikua watatu, Mimi, dada yangu na shangazi yangu.

Tulitoka home tukawa tunaenda kukata ndizi, dada yangu alishika panga la kwenda kufanyia hiyo kazi na tukawa tunatembea huku tunapiga story za hapa na pale na vicheko tele.

Sasa ghafla kuna picha fulani ilinijia hisiani kwamba dada yangu atatangulia mbele na atakua anayumbusha yumbisha panga then litamponyoka na kuishia kwenye sehemu fulani ya mguu wangu na litanichana sana na watanipatia huduma fulani ya kwanza(zingatia hapo, hisia zinasema mguuni na exactly area ya hapo mguuni nakua naiona).

Tulikua kwenye line moja wakati napata hizo hisia ila tukaenda kwa muda kidogo ile line ikawa iko blocked na kweli dada yangu akatangulia mbele, hazikupita dakika kuna namna akalichezesha lile panga likatua sehemu ile ile ambayo nilihisi lakini baada ya hapo wakanipa aina ile ile ya huduma ya kwanza.

Na kuhusu meditation hiyo ndio ibada yangu mkuu, nimeanza meditation tangu nipo advance na ndio njia ambayo nilikua naitumia kwenye kusoma.
 
Nifundishe namna ya kufanya hayo maombi mkuu😊😊
 
Mimi huwa ni negative tuu na jinsi ya kuzuia najua.
Nikipuuzia nadhurika.
Hiyo ya kuanguka nilikua Moshi vijijini asubuhi najiandaa kuamka...nikawaza nikifika sehemu fulani kuchukua maji nitajikwaa na kuanguka.
Nikakemea hiyo hali lakini sio kwa umakini sana...basi nilivyofika pale nilijikwaa nikayumba ila sikuanguka...
Nikamu hadithia shangazi yangu pale akashangaa tuu basi.
 
Kwa Imani yangu nilivofundishwa, chochote ninachokiota ambacho naona hakiko sawa lazima niombe ili kipishe mbali na Huwa inafanya kazi.

Chochote ninachoota ambacho Kiko sawa, lazima nikiombee ili kifanyike kwa utimilifunwaje na kwa uzuri.
 
Nifundishe namna ya kufanya hayo maombi mkuu😊😊
Una jitakasa kwa damu ya Yesu, tubu dhambi zako, una takasa watu wako wa karibu kwa kuwataja majina halafu una weza omba kwa kukataa taarifa mbaya zozote, kama unahisi ajali basi unazuia ajali au kitu chochote.
Maana muda mwingine roho inaweza kukuuma tuu bila sababu.
Nilivyokua kinder kuna kipindi roho iliniuma siku nzima kama mara Tatu hivi nyakati tofauti.
Mara zote hizo walifariki watu wangu wa muhimu, nikishapata tuu taarifa roho inatulia....so ningekuwa na maarifa haya ningefanya maombi labda kuzuia au lolote.
 
Ooh😅😅
 
Hiyo ya roho kuuma huwa ni dalili yangu moja wapo ya kupokea taarifa mbaya lakini pia hiyo siku nitashinda napiga sana miayo basi hali hiyo ikinipata najua muda wowote kuna taarifa mbaya naipokea😅😅😅.

Na kuhusu hapo kwenye kutubu dhambi, Mimi sina dhambi mkuu😂😂😂
 
Kama hauna dhambi Sawa, unaweza kuwatakasa wanao kuzunguka.
 
NB,USITOE TENA MIFANO HII NA IWE MWISHO KUSIMULIA TENA HAYA MAMBO.UTAHATARISHA NAFSI YAKO.
 
Ndoto ni lugha au taarifa ambayo ulimwengu unakupa ili uifanyie kazi au kuchukua hatua. Wengi wanapuuzia kwa kutokujua.

Uwe naandika na kurekodi ndoto zako itakusaidia na kuwasaidia wengine pia.
 
Ndoto ni lugha au taarifa ambayo ulimwengu unakupa ili uifanyie kazi au kuchukua hatua. Wengi wanapuuzia kwa kutokujua.

Uwe naandika na kurekodi ndoto zako itakusaidia na kuwasaidia wengine pia.
Nadhani huu ni ushauri mzuri saana.

Shukrani mkuu.
 
Jamaa ni kama Mimi. Tupo wengi hii ni kweli mkuu Mimi Kuna siku nipo dodoma nimekata tikti ya kwenda manyara gari ya saa 12 asbh basi nikiwa nimelala nikaota Ile gari imepata ajari na watu2 wamekufa na wamenifukwa na kanga...
Yaani niliota tupo kwenye gari hiyo namimi nikiwemo mle ndani lkn ajabu ni kwamba nikiwa kwenye hiyo ajari ghafla tu nikajikuta nashuka kutoka kwenye gari nyingine na kuanza kutazama wale majeruhi.

Nilishituka sikulala Tena! Muda ukafika wa kwenda kupanda Ile gari sikwenda ukumbuke hata nauli nilikuwa nimelipiwa na kubakiwa kama 15k ya matumizi na kuambiwa nikifika skonga atatuma ya matumizi.


Niliondoka hapo Kwa kuchelewa nikafika gari Ile imeondoka nikamwambia aliyenipa Ile nauli gari imeniacha Wakati kwenye ticket wameandika inaondoka saa12:30.


Akalalamika then akanitumia nauli nyingine...tumeenda nadhani ilikuwa kondoa pale tukakuta Ile gari imepata ajari na watu2 wamekufa kweli!!


Nikamwambia Sasa aliyenilipia Ile nauli ukweli wote na makusudi niliyofanya ya kutokwenda Kwa Wakati ule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…