Nimefurahi kwanza kuona uzi huu hapa kwa mara ya kwanza mtu anayetaka kujua zaidi kuhusiana na watu ambao hawapati ukimwi.
Nikiri kwamba mimi ni mmoja wapo na niliwahi kuweka uzi hapa kuulizia kama kuna watu wa desighn yangu ili tuweze kujuana na kujaribu ku share mambo mbalu mbali.
Nisiende mbali kikawaida kuna watu wa aina tatu ambao mungu kawapendelea (naona ni neno zuri kulitumi) ambao wana uwezo mzuri wa kuvi ongoza virusi vya ukimwi niatelezea kiufupi.
1.long term non progressors.
Hawa ni wale ambao wanapata virusi lakini huwa virusi havikui kwa hali yoyote ile japo vinaendelea kubaki ndani ya damu.hutawahi kusikia akimeza dawa(ARV) au akiumwa.
2.short term non progressors.
Hawa ni wale wanapata virusi lakini mashambulizi yake yanakuwa ya taratibu mno na huwa hawaumwi mara kwa mara na pia huwa hawategemei sana dawa (ARV).
3.Innate resistance to HIV.
Hawa ndo tunasema wamepewa baraka zote (nilipima hospitali moja hapa hapa ndani ya nchi inapatikana kaskazini mwa tanzania , na ndiyo hospitali pekee wanayohusika na maswala ya genetics kwa tanzania , nikipata muda ntawek ni kitu gani kilinifanya nikafika huko).
Hawa huwa wanapata virusi ila huwa vinaondoka baada ya muda fulani kwa maana kwenye cell zao huwa hawana vipokezi( receptor proteins) hivyo kuvifanya virusi vishindwe kuingia ndani ya cell na kujigawa .hii imetokana na wao kuwa na mutation kwenye delta 3 gene kwenye miili yao .
Na huwa wamaumwa magonjwa mengine mengine ila si ukimwi au ugonjwa wa kirusi unaotegemea receptor kuingia mwilini.
Sent using
Jamii Forums mobile app