Chilogole
JF-Expert Member
- Jun 18, 2019
- 291
- 273
We jamaa unauwezo Wa kuchambua mambo sanaLakini pia watu hawataki kuamini kuwa hata rafiki anachunguzwa.
Hakuna nabii ambae hakuwa na rafiki ambae alisuhubiana nae katika mambo yake.urafiki ni kitu kikubwa.
Angalia huyo unayetaka kumfanya rafiki je akiwa na wewe hawasemi vibaya watu wengine mbelr yako ?
Kama anawasema basi jiulize " je akiwa na wengine hatanisema mimi vibaya ?"
Akiwa hawasemi vibaya wengine akiwa na wewe basi ana sifa miongoni mwa sifa za kuwa rafiki.
Kwa sababu sio urafiki ule ambao wakikaa huwasema wengine na kuwabeza,bali urafiki ni kukaa wawili mkawa mnajadili mambo yenu wenyewe na kutafuta ufumbuzi.
Kwa sababu kwenye maisha kuna malengo na changamoto.
Kama hamjadili namna ya kutatua changamoto basi mtajadili namna ya kuyafikia malengo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app