Wakuu Wakuu kwemaa?
Hivi kwa wadau tusaidieni hapa, kwa uzoefu wenu kweli kuna urafiki wa kweli kabisaaaa? Yaani bila hata chembe ya unafiki?
Maana unafiki naokuwa nakutana nao kwa baadhi ya marafiki, aiseee [emoji856] Unaona mshkaji wako kabisa, lakini ndo huyo at some point unasikia anakupiga majungu other side.
Wengi wa marafiki wanaoonekana wa kweli, wanapokuwa tested (wanapojaribiwa) na kitu fulani ambacho kwa namna moja ama nyingine ni fursa kwao ila ni maumivu kwako, hawasiti kufanya hivyo!
Hivi kuna huo urafiki wa kweli kabisa kabisaaa?
Au mtu upige tu mishe zako na familia yako, hao wengine wote uwachukulie tu kama mtu wa kuja leo na kuweza kuondoka muda wowote?
Wakuu Wakuu kwemaa ?
Hivi kwa wadau tusaidieni hapa, kwa uzoefu wenu kweli kuna urafiki wa kweli kabisaaaa? Yaani bila hata chembe ya unafiki ?
Maana unafiki naokuwa nakutana nao kwa baadhi ya marafiki, aiseee [emoji856] .. unaona mshkaji wako kabisa, lakini ndo huyo atsome point unasikia anakupiga majungu other side.
Wengi wa marafiki wanaoonekana wa kweli, wanapokuwa tested ( wanapojaribiwa ) na kitu fulani ambacho kwa namna moja ama nyingine ni fursa kwao ila ni maumivu kwako, hawasiti kufanya hivyo!!!
Hivi kuna huo urafiki wa kweli kabisa kabisaaa?
Au mtu upige tu mishe zako na familia yako, hao wengine wote uwachukulie tu kama mtu wa kuja leo na kuweza kuondoka muda wowote ??
Marafiki wa kweli wapo,ila hawatafutwi.tunachokosea waswahili tunadhani kila tuliyezoeana nae ati ni rafiki.
Rafiki wa kweli hatafutwi bali mnakuwa connected kutokana na mazingira fulani.mfano mkiwa kazini unaweza kupata rafiki huko alafu ikawa mnaendana baadhi ya tabia hapo mtakuwa marafiki.
Sasa wewe ukiona umezoweana na mtu mnapiga story za hapa na pale unadhani ndo rafiki,hapana.
Kumbuka katika maisha lazima uwe umezoeana na watu wengi alafu marafiki lazima wawe wachache.ukiona kila uliyemzowea unamfanya rafiki basi ujue unakaribisha wanafiki wengi katika maisha yako.
Kwa sababu kinyesi ndo hufuatwa na Nzi wengi na wala sio dhahabu.
Rafiki katika maisha awe mmoja tu au wamezidi wawili,rafiki ni yule ambae unamuambia jambo lako la siri kisha hulisikii kwa mwingine.
Bora umpate rafiki ana kasoro zote lakini asiwe na kasoro ya kutoa siri,kutunza siri ni neema kubwa katika maisha.
Mimi binafsi kuna watu wananipa siri zao sio ili niwape ushauri bali wanataka kutua mizigo yao tu na wana uhakika hawataziskia kwingine,sipendi majungu hata kama sio rafiki yangu haijawa tiketi ya kukuoiga majungu.
Sinaga utaratibu wa kutoa siri za mtu hata akama sio rafiki yangu.
Nina rafiki yangu hayuko tanzania na hatujawahi kuonana lakini ni marafiki sana kiasi kwamba naweza kushare nae jambo ambalo hata wife siwezi kumuambia kamwe(wanawake wivu)na tunashauriana vizuri,na hata yeye yakinikuta hunipa makubwa mpaka nashangaa kwamba kumbe hata yeye huwa yanamkuta.na life linaenda.tunawasiliana kwa mtandao tu.
Pesa tunatumiana hakuna kudhulumiana mpaka tumepanga tutembeleane.
Rafiki wa kweli ni yule ambae ukimwambia mambo yako ya siri huyasikii kwingine.mnashare mawazo na kupeana moyo hata kama mafukara.
Usitake kila anaekuzowea awe rafiki yako,kuna watu wameumbwa kuzowea zoea ovyo tu na kujipendekeza.
Rafiki hatafutwi kuna kitu kinawaunganisha tu mnajikuta marafiki as the day goes.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Sent using
Jamii Forums mobile app