Je, kuna ukweli kuwa vocha zinasababisha kansa?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Naomba nipate majibu ya kitaalamu kama ni kweli vocha za simu (kwa ajili ya muda wa maongezi) zinapokwanguliwa ule unga unga wake ikitokea ukaingia mwilini unasababisha madhara makubwa ikiwepo kansa.

Kumekuwa na kasumba ya kutumia sarafu kama kikwangulio. Je ni nani aliyetuaminisha kuwa kutumia sarafu ni salama? Vipi kuhusiana na mabaki ya unga unga unaobakia kwenye sarafu hizo wenyewe tunaudhibiti vipi usisababishe madhara kwa wengine? Na je ni wangapi ufuata hatua hizo za kujikinga kwa usahihi ikiwemo kunawa mikono baada ya tendo hilo la kukwangua vocha?

Ikiwa ni kweli jambo hili upelekea ugonjwa hatari wa kansa ambao hauna tiba, je serikali na wadau wa afya wanachukua hatua ipi kuwanusuru wananchi wake?

Ikiwa katika sigara imewekwa tahadhari ya kiafya kwa watumiaji wake baada ya kuthibitika kuwa ina madhara. Kwanini kitu kama hicho hicho kisifanyike katika vocha ambazo utumiwa na mamilioni ya watanzania kila siku?
 
Back
Top Bottom