Je kuna uhusiano wowote wa ac ya gari na ilaji wa mafuta?

Nimetumia hillo neno kuonyesha tofauti mfano subaru yangu nikiweka ya elfu 10 na AC mjini kukiwa na foleni ni km 25 bila folen km 32 bila AC kilometa 40, nikiweka mafuta ya laki na AC bila foleni napoteza kilometa 80, na foleni napoteza mpaka kilometa 95 kwa mafuta ya laki moja, tofauti ni kubwa sana.
Kumbe...hata mimi subaru nikiweka mafuta ya elfu 10 natembea kilometa 40 bila Ac.
 
Demu wangu akiingiaga kwenye gari yangu, cha kwanza utamsikia "washa AC".
Ananikeraga, basi tu
 
Kuna siku fulani nilikua nimetoka kituo cha mafuta gati ilikua inasumbua cylinder head kwaio ukiwasha A/C tu lazima ichemshe nimetia wese la 50,000 sababu ya jua kali nina sweat vibaya mno basi konda wa pembeni "alivyoniona akasema baba majqsho yote hayo kulikoni? Si umetoka sheli washa kiyoyozi hicho niliishia kucheka tu kilichofamnyika nilijichanga ku repair cylinder head sasa hivi ni full time a/c hata safari iwe buguruni kariakoo ni mwendo wa a/c foleni iwe ndefu kiasi gami haitembei ni full time a/c..ubahili hauna faida yoyote ile..wese la 55,000 full time a/c natumia siku 7 au 8..
Samahani ni gari Aina gani!?

NB: sijabahatika kununua gari Ila nafuatilia forum hii kwa umakini, pengine kuna siku yangu!
 
Back
Top Bottom