Je kuna uhusiano wowote kati ya Mungu na Pesa? Je pesa ni mpango wa Mungu?

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
59,999
104,320
Wanabodi,
Nimekuwa nikijiuliza sana sisi tunaomwabudu Mungu wa dini mbalumbali na madhehebu mbalimbali, utakuta tunapingana kwa mengi mpaka tunatowana macho lakini likifika swala pesa hizi dini na madhehebu yote hayapingani kwenye swala la mshiko dini zote zinahamasisha kutowa sadaka na fungu la kumi tena mpaka pesa za watu maskini kabisa wanazitaka kwa maneno ya kuwafariji maskini kwamba sadaka yao ni kubwa kuliko ya tajili, tena kuna madhehebu ukihudhuria ibada zao 99% ya mahubiri yao ni kuhusu kujitowa fedha, najiuliza why money?

Sasa mimi nauliza je pesa iliumbwa na Mungu au iliumbwa na binadamu? Na ni kwa nini Mungu tumtolee sadaka ya pesa? Je Mungu anahitaji pesa? Na kama Mungu anahusika na pesa si angetujaria binadamu wote kama zilivyo nywele kila mtu na zake?

Karibuni tufunguwane akili.
 
Bro umegusa penyewe. Niwe mkweli MI ni mkristo Nashangaa makanisani tunahubiriwa sadaka Sana. Maendeleo ya Kanisani

NA mimi swali nalojiuliza ni kwanini kama sadaka ni suala Zuri LA kumtolea MUNGU kwanini wanasisitiza Sana kwanini tusiachiwe sisi Waumini tuguswe ndio tutoe.. Lakini UKIJA Kwa upande swinging ukifikiria unaona MICHANGO Ile ina faida Kwa sababu hizi( dini) TAASISI zimejitahidi kufanya makubwa na lazima hela imetumika. MFANO madhehebu yana mashule. Na yanajitoa kwenye huduma za kijamii. Pale pesa inazunguka. Ila binafsi Nashangaa kwenye mahubiri habari ni za sadaka tu. Baraka za sadaka. Yale mafunzo ya kiroho hayapewi msisitizo. Ndio maana tukubaliane MUNGU mmoja na sio lazima uwe wa dini fulani ndio uende Mbinguni. Amini hivo MUNGU tuko naye rohoni sio misikitini wala makanisani
 
Wanasema kwamba kila kilichopo na kinacho tokea dunia ni mipango yake Mungu..

So hata hizo pesa nimipango yake mungu

Uwepo ISIS.nimipango mungu

Watu kuuwana na kubakana ,watoto wadogo kuteswa na.kuuwawa yote ni mipango yake mungu

Uwepo wawa kina.kaoge na james delicious ni mipango yake mungu

Maana Mungu ni mkubwa ana nguvu na anajua ya ljana,ya leo na hata ya kesho...


Hakika imani kitu kibaya maana Mungu ni.gaid,mbinafsi,mfitinishi zaid ya binadamu

Namsubili.kwa kwa.hamu kama kweli yupo
 
Umegusa penyewe

Mngu hajawahi kua na shida na hela,,mungu anashida na hali zetu kwake. Anataka tumwabudu tu BA's,sadaka sio kipaumbele kwa mungu bali kwa binadamu, kutoa fungu LA kumi yaaan faida yako moja ya kumi au mshahara wko moja ya kumi yake unapeleka kusidia masikini. Ni afadhali usaidie mayatima ma wajane na wazee na wagonjwa a watto wa mazingira mag;umu kuliko kutoa hela yajengo kila wiki pale kanisan,tens wengine wana minada kabsa kanisan,mboga mboga unauziwa mpka 20000 fungu tatu za sukuma wiki daaaah hatari sana.

Kiukwel tumegeuza dini biznes,michango weeeeeee mpka unasema kwel mungu ndio anachotaka? Kuna mafungu ya watu wanahitaj msaada kiukwel kbsa lakin sio makanisa hata shue zenyewe ukichelewesha ada wana mrudisha mtoto nyumban sasa unajiuiza msaada wao ni UPI? Hata Ndoa ukifunga hela unachangia sasa nn maana ya kanisa... Ila nmewakwepa siku hiz baada ya kugundua mengi...
 
Dini zooote ni miradi ya watu. Imani zoote juu ya Mungu ni mali yake Muumba.
 
Kiukweli siku hizi imekuwa too much tofauti na miaka ya zamani maana siku hizi asilimia kubwa ya mahubiri ni kuhusu kutoa dhaka na sadaka kwa wakiristo kuliko kueneza injili na neno la mungu ambalo ndo lengo mama la hizo dini kuanzishwa.
 
fe865e4045561c58720630ab0c4cbb3f.jpg

Kwa sasa amna kondoo na mazao ya kutosha kwaajili ya sadaka,
PESA ni alternative
 
Fedha na dhahabu ni Mali yake.kama wewe pia ni wake unahaki kutumia lakini vipi unatumia ni shauri yako. Na anataka umpende kwa nguvu zote,moyo wote na kila ulichonacho. Hatakuangusha.
 
Kimsingi kwa namna nijuavyo mimi ni kwamba,ni makosa kumhusisha Mungu na makosa ya wale wanaodai kuwa wanamfuata kwasababu kama yeye anaagiza mambo ambayo wao hawayafuati ni wazi kwamba hao siyo wafuasi wa wanayejinadi kuwa wanamfuata....

Nadhani namna njema ya kujadili ni kujadili vitabu husika vya imani na siyo waumini maana waumini wanaweza kuwa wanakwenda kinyume na maagizo ya kwenye vitabu vyao na kama ni hivyo basi wanaopaswa kuhukumiwa ni wanadini na siyo dini na Mungu.....

Suala lako la viongozi wa dini kuwa na mtindo wa kuhubiri sana kuhusu kutoa na wasiwasi wako wa watu hao kudai hata pesa ya masikini naweza kusema kwa namna mbili...

1;Kama wanahubiri hivyo kinyume na maagizo ya kwenye maandiko ni makosa na inaonekana wanakosea kwa mujibu wa maelezo yako kwasababu umesema "asilimia kubwa ya mahubiri yao ni kutoa tu",kwasababu hii nasema ni kosa kwasababu malengo makuu ya Mungu ni kuokoa roho za mwanadamu na siyo hayo mengine,kama wanafanya kama usemavyo wanakosea....

2;Kuhusu kutoa na kuhimiza hata masikini kutoa hili nitalisema kwa mtazamo wa Kikristo ambao ni kwa mujibu wa nijuavyo mimi...

Hili ni kwamba siyo kwamba Mungu anaposema tutoe inakuwa inamaana kwamba Mungu anahitaji pesa,hapana.Ni hapana kwasababu kwanza Mungu hana uhitaji wowote ule kwasababu ni Mungu na akishaanza kuwa na uhitaji anapoteza sifa yake ya kuwa Mungu hivyo siyo kweli kuwa Mungu anahitaji sadaka au fedha....

Kabla sijasema kwamba sadaka ina uhalali au hapana labda niseme kwanza sadaka ni nini hasa.Nyakati za kale,japokuwa kulikuwa kuna fedha Mungu alikuwa akiwaagiza watu watoe sadaka lakini haikuwa fedha japokuwa pia inaweza kuhusishwa.Mara nyingi sana alikuwa akihitaji mavuno ya mazao yao kama sadaka na wanyama,hii ilikuwa kabla ya ujio wa maokozi wa ulimwengu na walikuwa wakihitajika kutoa sadaka kwasababu mbali mbali...

Je sadaka ni halali na ni kwaajili ya nini/nani?

kikristo,sadaka yoyote huwa ni kwa faida ya mtoaji.Unapotoa sadaka unakuwa unatoa kwaajili ya mambo mbali mbali na hili ni somo refu sana lakini kimsingi sadaka ina faida kwa mtoaji na ndiyo maana Mungu amesisitiza tutowe sadaka...

Je ni faida gani?

Nikichukulia mfano zaka,zaka ni sadaka lakini ipo katika fungu la kumi la mapato yako.Zamani walikuwa wakitoa mazao kama nilivyosema hapo juu kwasababu za kimazingira lakini leo wanatoa fedha kwasababu za kimazingira pia.Unapotoa zaka hii inamaana nyingi sana lakini maana rahisi kabisa ni kurejesha shukrani kwa Mungu kwa kukupatia mapato hayo,iwe ni mazao au fedha.Unaposhukuru unakuwa unajichotea baraka tele na uhalali wa kupata mafanikio kama hayo wakati mwingine na pengine mafanikio zaidi ya hayo....

Kushukuru ni hitaji la kiroho hivyo ni muhimu sana kulitumia kwaajili ya faida.Unaposhukuru kwa kutoa zaka hii ina maana kwamba unajichotea baraka na uhalali wa kupata tena na tena na siyo kinyume chake,unapoacha kutoa unapoteza uhalali wa kudai mafanikio mengine.Zaka inamaana zaidi ya hiyo lakini kwa faida tu ya wasomaji maelezo hayo ya kawaida yanaweza kuwafungua macho....

Sadaka kama sadaka kama nilivyoeleza hapo juu zinatofautiana,kuna sadaka ya shukrani,sadaka kwaajili ya maombi,sadaka ya shukrani n.k...

Sadaka ya shukrani kwa mfano,hii ni sadaka ambayo unaweza kuitoa kwa kumshukuru Mungu kwa kukupatia kazi kwa mfano,unaposmshukukuru Mungu unafanya wewe upate baraka kazini na pia uhalali wa kuendelea kudai ulinzi kazini kwa Mungu na mengine mengi hivyo unaweza kuona namna ambayo sadaka hii ina faida.....

Je,sadaka hizi nani anapaswa kupewa?

Hili ndilo swali ambalo wengi wanajiuliza.Kimsingi hizi sadaka maalum ikiwemo zaka ni aina ya sadaka ambazo wewe mhusika unaguswa wa kumpa.Unaweza kuguswa kutoa kwa wasiojiweza,unaweza kuguswa ukampe mtumishi fulani wa Mungu,unaweza ukaguswa ukamlipie mgonjwa matibabu hospital n.k,angalia kile ambacho wewe unaambiwa ndani yako na ukifanye na siyo kulazimishwa na mtu pa kupeleka sadaka hii.Hata kale Mungu alikuwa akielekezeza mahali au namna ya kuifanya sadaka husika hivyo usilazimishwe na mtu mahali pa kuipeleka sadaka yako....

Vipi kuhusu sadaka za kila siku ya ibada?

Hizi sadaka kimsingi ni tofauti na zile sadaka maalum nilizozisema hapo juu,sadaka hizi hutolewa kwaajili ya kugharamia maisha ya watumishi wa Mungu na pia kujenga majengo ya ibada na gharama zingine za kila siku za watumishi na mahitaji ya shughuli nzima ya kueneza neno la Mungu.Sadaka hizi nazo zina faida kubwa sana maana kitenmdo cha wewe kuwezesha watumishi kwenda kutangaza neno la Mungu na watu kusikia habari za Kristo na hatimaye maisha yao kuokolewa ni jambo la baraka sana.Unapotoa sadaka hizi unajichotea baraka nyingi sana pia na utaona baraka kila siku katika maisha yako,hivyo ni muhimu pia....

Kubwa katika yote ni kwamba,kinachofanya yote hayo niliyosema ni ile imani yako iliyoko ndani yako wakati unatoa sadaka yoyote miongoni mwa hizo hapo.Usitoe sadaka ili uonekane nawe unatoa,usitowe sadaka kwa kujionesha,usitowe sadaka huku unanung'unika kama ukifanya moja au zaidi ya hayo yanayofanana na hayo utakuwa unajisumbua tu....

Kama umeguswa sadaka yako ya shukrani ukampe mtoto wa jirani yako ada ya shule,nenda kampe na hakuna haja ya uliyempe au mtu mwingine kujua sababu ya wewe kufanya hivyo,sababu ya wewe kufanya hivyo iwe ni siri yako wewe na Mungu tu.Usimsimange kwa chochote kwasababu umempa fedha utasababisha lengo lako lisitimie kabisa,toa sadaka yako endelea na maisha yako na sahau kabisa jambo hilo.....

Kwa uchache sana ni hivyo.....

Barikiwa sana.....
 
Kaka Matola , Kanisa lina sehemu mbili, kuna sehemu ya Kimwili na Kiroho, nazungumzia Makanisa makongwe tukiacha haya ya Kisasa, Mwili ndio unaobeba roho (spirit), lakini mahitaji ya kimwili yapo tofauti na ya kiroho, Japo kuna wakati mahitaji ya Kimwili na Kiroho yanaingiliana.

Lakini pia ukisoma maandiko utaona hata wakati wa Yesu watu walikuwa wakitoa Sadaka za pesa, unakumbuka habari za mama mjane na Dinari yake moja na Yesu akasema huyo ndio aliyetoa zaidi ya wote? Unakumbuka pia Yuda ambaye alikuwa ni mtume wa Yesu ndio alikuwa mshika Pesa wao? Pesa za Nini? Unakuta walikuwa wanahitaji mahitaji ya Kula, Kuvaa, Kusafiri nk,
 
Fedha lazima zitolewe tu lakini udhibiti wa matumizi lazima uwepo.
Gharama za kimwili kuendesha Nyumba za ibada ni kubwa na zinaongezeka.

Unahitaji Waendesha ibada wapate fedha kwa ajili ya kuendeshea maisha yao (kula, kuvaa, kunywa, mawasiliano, kodi
ya pango, umeme, maji, usafiri nk) kwa sababu anatumia muda mwingi kuhudumia Waumini)

Ukiacha hilo nyumba ya ibada ina gharama za umeme, usafi, ukarabati nk. Kuna Waumini huwa wanachagua mpaka
Kanisa au Msikiti fulani kwa ajili ya ibada mbali na alipo, inawezekana ni kwa sababu ya mpangilio wa mahubiri lakini
wapo wanaenda kwa sababu kuna parking kwa usalama wa gari yake, usafi wa nyumba ya ibada pamoja na maliwato nk.
Hayo yote huwezi kuyapata kama hakuna fedha inayotolewa na Waumini kwa sababu makanisa/Misikiti mingi
haina vitega uchumi.

Nakubali kuwa wapo Viongozi wa nyumba za ibada wasio waaminifu lakini haiondoi umuhimu wa kutoa fedha (zamani walitoa kondoo, dhahabu nk)
 
Dini ni Taasisi... Taasisi haiwezi kujiendesha kwa maneno matupu pesa lazima itumike...
 
Kwa uelewa wangu,nadhani sadaka ni mshahara wa awa jamaa wakuitwa wahubiri,ila ni swali gumu.Ngoja siku Mungu akija atawaumbua kama izo sadaka walikua wanampa kweli au waliweka matumboni mwao.
 
fe865e4045561c58720630ab0c4cbb3f.jpg

Kwa sasa amna kondoo na mazao ya kutosha kwaajili ya sadaka,
PESA ni alternative
Kondoo wako wengi tu! Au hujasikia watu wanaitwa Kondoo wa Bwana?
Zamani watu walikua wanatafuta kondoo wa sadaka . Lakini sasa watu ndio wamekua kondoo wanatafuta pesa ya Sadaka
 
Wanasema kwamba kila kilichopo na kinacho tokea dunia ni mipango yake Mungu..

So hata hizo pesa nimipango yake mungu

Uwepo ISIS.nimipango mungu

Watu kuuwana na kubakana ,watoto wadogo kuteswa na.kuuwawa yote ni mipango yake mungu

Uwepo wawa kina.kaoge na james delicious ni mipango yake mungu

Maana Mungu ni mkubwa ana nguvu na anajua ya ljana,ya leo na hata ya kesho...


Hakika imani kitu kibaya maana Mungu ni.gaid,mbinafsi,mfitinishi zaid ya binadamu

Namsubili.kwa kwa.hamu kama kweli yupo
shetani pia ni mpango wa mungu.
 
Back
Top Bottom