Je kuna uhusiano kati ya pombe na usingizi?

J33

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
1,552
1,512
Salam wana jamvi!
Mimi ni mmoja wa watumiaji wa kati wa pombe hasa weekend na nikiwa likizo. Nimetumia pombe kuanzia tarehe tano had tare 26 December bila kupumzika. Mara nyingi natumia Castle lite na mara chache Value au nazichanganya. Siku ya tarehe 26 kitu cha ajabu kilinitokea ambapo nilikuwa nakunywa pombe zote hizo ila bila kulewa kabisa. Nilitafakar nikaamua kupumzika pombe kwa muda nikihisi kuwa labda kunywa bila kupumzika pombe inaanza kuzizoea. Tatizo lililonileta hapa ni kuwa kuanzia usiku wa tarehe 27 na ishirini na nane had ninavyoandika uzi huu sipat usingizi kabisa yan hata wa dakika 5. Nauliza wataalamu kama kuna uhusiano kati ya kupumzika pombe na kutopata usingiz. Natanguliza shukrani.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom