Je, kuna ubaya kwenda kumjulia hali na kumpa pole Mama Janeth Magufuli?

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
JE, KUNA UBAYA KWENDA KUMJULIA HALI NA KUMPA POLE MAMA JANETH MAGUFULI!?

Kwanza nilimuona mtoto wa Hayati Rais Magufuli akisema mama yao hajisikii vizuri tangu Mzee alipotangulia.

Baadae nikaona habari ya Baba Mdogo kupita Chato akielekea Kigoma na watoa habari walisema amekwenda kumjulia hali Mama Magufuli and it made sense, ukizingatia hotuba ya kijana wake alisema Mama hajisikii vizuri.

Sasa kama Mama Janet yuko Dar hata Baba Mkubwa juzi alienda kumuona, kwa mila zetu Watanzania ni vizuri Watanzania wakaendelea kumtembelea kumpa pole na kumfariji.

NB.
Tusisahau kwamba Mama Janeth Magufuli anaweza kutumika kama MTAJI WA KISIASA kwa mazuri aliyofanya Hayati Rais John Magufuli kwa ajili ya Uchaguzi ujao wa 2025.
 
Muacheni mama janeth apumzike. Ulishatoa ramvirambi inatosha. Msije mkajazana mkampelejea covid bure acheni apumzike anatakiwa apumue hata mwaka hivi arudi purukushani kila siku kusongesha familia hasa watoto. Kuwaomvea ombea kuwachomeka....hata ubalozi DAS na RAS.
 
Akili finyu sana kuhusisha na siasa kila kitu. Wazo la kumjulia hali sawa lkn kumtumia kisiasa ni finyu sana.
 
GIA yako ya kutafuta teuzi nimekubali mwanangu....naona umepigia Pasi ndefu Hadi Kwa mama Janet
 
Hata ukiamua kuhamia Chato ni sawa tu, kitovuni kule mambo mazuri sana....
 
Back
Top Bottom