Je, kuna sehemu Mwl Nyerere alikosea katika ahadi hizi?

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Toka Mwl Nyerere alipozitoa kwa umma Ahadi hizi kumi za MwanaTANU zikafundishwa toka kizazi hadi kizazi mashuleni huwa naangalia ni wapi alipokosea au tulipokosea mpaka Leo bado nchi haijasimama ktk msingi yake nashindwa kupata jibu.

Watanzania wapi tulikosea ktk ahadi hizi 10 za MwanaTANU.

1.Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

2.Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.

3.Nitajitolea nafasi yangu kuondoka UJINGA,UMASKINI,MARADHI na DHULUMA.

4.Rushwa ni adui wa haki "Sitapokea wala kutoa Rushwa"

5.Cheo ni dhamana "Sitatumia cheo changu au cha mtu mwingine kwa manufaa yangu"

6.Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7.Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yangu.

8.Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko.

9.Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.

10.Nitakuwa mtii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Hata yeye aliwahihisi kama alikosea, ila kila alipokuwa anarudia kuzisoma hakuwahi gundua kosa lake. Labda kama wewe umeligundua kosa utuambie.
 
Hata yeye aliwahihisi kama alikosea, ila kila alipokuwa anarudia kuzisoma hakuwahi gundua kosa lake. Labda kama wewe umeligundua kosa utuambie.
Nikizisoma sana hizi Ahadi naona tu watanzania tulifanya UASI wa hizi AHDI ktk kusimamia utekelezaji wake.
 
Back
Top Bottom