Mfano No. 1
Tufanye mimi ni Mfanyakazi kwenye kampuni fulani, nikaoa m/mke. Tukaanza maisha pamoja.
Mke ni mama wa Nyumbani. Mungu akajalia tukajenga Nyumba na gari tukanunua. Sasa baada ya mwaka
tukawa na migogoro ndani ya ndoa mwishowe tukaachana.
Mke akaenda mahakamani tugawane kila kitu pasu kwa pasu. Ikawa hivyo...
Mfano No. 2: Endelezo
Nikiwa bado mfanyakazi na mke akiwa mama wa nyumbani kama ilivyokuwa mfano No. 1
tukajenga na gari tunayo. Kwa ufupi maisha mashaalah.
Ikatokea ofisini upotevu wa mali, nikahusishwa na kesi hiyo. Na kauli ni HAKI SAWA!
Je, kwa nini nishitakiwe mimi peke yangu ihali mali zile tuliwekeza wote na wife
Kwa nini tusishitakiwe wote wawili kama vile tutakavyogawana mali tukiachana? Maana tulichuma wote ati!!
Mfano No. 3
Kwa kuwa HAKI SAWA kwa wote, na tunajua mfumo wa elimu yetu bongo ulivyo;
Kwa nini Wanawake wawe na daraja la upendeleo kielimu huku likiacha watoto wa
kiume wawe vibaka na majambazi? Kwa nini Wasichana wapendelewe, wavulana waachwe
ikiwa point za ufaulu ni sawa kwa mitihani ileile
Na.....