Je kuna maprofesa na madokta (PhD) jeshini??

Kuna mmoja tena ni best ' Neurologist ' akiwa amesomea nchini Urusi na amehudumu sana hapo Lugalo Hospital anaitwa Professor Yardon Kohi amestaafu akiwa na Cheo cha Brigedia anaishi Mbezi Beach barabara ya zamani ya kwenda Goba. Tena asikudanganye Mtu huko Jeshini ndiyo kuna ' Wasomi ' waliotukuka hadi balaa.
Duh, basi wako kimya sana, hawajioneshi!
 
Habari.
Nilitaka kujua maana sijawahi waona wala kusikia hawa 'wasomi' ktk nyanja ya jeshi eidha jwtz au polisi au jeshi lolote!
Wa kutosha sana tu (hasa JWTZ). Kamishna general wa magereza mwenyewe ana PhD (Dr. Malewa). Juzi tu pale rais anatoa kamisheni Arusha umesikia zile takwimu pale kulikuwa na Masters za kutosha sana tu.
 
Wapo wakutosha Dr mkuu wa jeshi kipindi cha mgomo wa ma Dr Muhimbili alikuwa anaitwa Dr,Prof,Brigadier general? ???? Namuhifadhi kwa wasiojulikana taaluma zote zilizo uraiani pia ziko jeshini.Kudhibitisha hili wakati waongoza ndege waligoma hawa jamaa kitengo cha anga walikwenda kushika usukani.Vyeo vyao ambavo ndio maarufu vinafunika vyeo vyao vya kisomi hawa jamaa hawana majivuno.Jeshi la Marekani tafiti za mambo ya tiba na anga zinafanyikia kwao. Enzi za Nyerere marubani wa ATC japo walikuwa wanaonekana raia lakini walikuwa wanajeshi.Hivi unajua mkuu wa jeshi la magereza ni mwanamke na ana phD?
Acha uongo....magereza mwanamke?You are not serious, uhamiaji ndo ke
 
Wapo wakutosha Dr mkuu wa jeshi kipindi cha mgomo wa ma Dr Muhimbili alikuwa anaitwa Dr,Prof,Brigadier general? ???? Namuhifadhi kwa wasiojulikana taaluma zote zilizo uraiani pia ziko jeshini.Kudhibitisha hili wakati waongoza ndege waligoma hawa jamaa kitengo cha anga walikwenda kushika usukani.Vyeo vyao ambavo ndio maarufu vinafunika vyeo vyao vya kisomi hawa jamaa hawana majivuno.Jeshi la Marekani tafiti za mambo ya tiba na anga zinafanyikia kwao. Enzi za Nyerere marubani wa ATC japo walikuwa wanaonekana raia lakini walikuwa wanajeshi.Hivi unajua mkuu wa jeshi la magereza ni mwanamke na ana phD?
Mkuu yote umetiririka vyema, ila hili la mkuu wa jeshi la magereza kusema ni mwanamke ni uongo wa mchana kweupe.
Sema kama ulikuwa ukimaanisha mkuu wa jeshi la uhamiaji hapo sawa.
 
Habari.
Nilitaka kujua maana sijawahi waona wala kusikia hawa 'wasomi' ktk nyanja ya jeshi eidha jwtz au polisi au jeshi lolote!
Kuna mmoja tena ni best ' Neurologist ' akiwa amesomea nchini Urusi na amehudumu sana hapo Lugalo Hospital anaitwa Professor Yardon Kohi amestaafu akiwa na Cheo cha Brigedia anaishi Mbezi Beach barabara ya zamani ya kwenda Goba. Tena asikudanganye Mtu huko Jeshini ndiyo kuna ' Wasomi ' waliotukuka hadi balaa.

prof major general Dr yodan mtalima kohi alikaa COSTECH kama mkurungezi kwa miaka 13 ,ila Bwana mkubwa wa awamu ya nne alitengua uteuzi wake na kurudishwa Jeshini ,inasemekana utendaji mbovu wa walio chini yake na alishindwa kuiindeleza sayansi nchi kwa miaka yote hiyo aliyokuwa mtendaji mkuu wa chombo cha wanasayansi TZ ,Tetesi zingine kuwa bwana mkubwa alichukia aliposikia watendaji wa chini yake walikuwa wanatumia magari kwenye ishu za ujangili,mara jengo la serikali watumishi waliochini yake wakapaka rangi za matangazo ya kampuni fulani ya simu nk........ miaka ya mwisho ya utumishi wake alitumika vizuri kama mtabibu lugalo na kufanya vizuri sana kwenye fani yake.Pia inasemekana ni mtaalam pekee wa medical law TZ
 
Mkuu yote umetiririka vyema, ila hili la mkuu wa jeshi la magereza kusema ni mwanamke ni uongo wa mchana kweupe.
Sema kama ulikuwa ukimaanisha mkuu wa jeshi la uhamiaji hapo sawa.
Hakuna jeshi la uhamiaji, ile ni idara ya uhamiaji.

Kwanza nchi hii tuna jeshi moja tu JWTZ hivyo vingine ni vikosi tu.
 
Wapo wakutosha Dr mkuu wa jeshi kipindi cha mgomo wa ma Dr Muhimbili alikuwa anaitwa Dr,Prof,Brigadier general? ???? Namuhifadhi kwa wasiojulikana taaluma zote zilizo uraiani pia ziko jeshini.Kudhibitisha hili wakati waongoza ndege waligoma hawa jamaa kitengo cha anga walikwenda kushika usukani.Vyeo vyao ambavo ndio maarufu vinafunika vyeo vyao vya kisomi hawa jamaa hawana majivuno.Jeshi la Marekani tafiti za mambo ya tiba na anga zinafanyikia kwao. Enzi za Nyerere marubani wa ATC japo walikuwa wanaonekana raia lakini walikuwa wanajeshi.Hivi unajua mkuu wa jeshi la magereza ni mwanamke na ana phD?
Sio magereza mkuu... ni uhamiaji!!!
 
Kwa vile uprofesa hupatikana kwa kupanda cheo mtu mwenye PhD, uwezekano pekee ni mtu ambaye tayari ni profesa kutoka taasisi ya elimu ya juu kuingia jeshini akiwa tayari ni Profesa.
Si rahisi kihivyo lakini. PhD mtu akiwahi sana Itakuwa chini ya miaka 30. Kunaweza kuwa na exceptions chache. Kutoka PhD hadi Profesa kawaida ni miaka 9. Sasa mtu huyo kuingia jeshini atakuwa na miaka 40 tena yule aliwahi kabisa.
Hapo ndiyo Kuna kimbembe!
 
Yupo mmoja ni 2/c wa komandi ya Anga, jina kapuni. Mzee yule alianza kwa kuwa daktari (MD), then alivyoingia jeshi akachaguliwa akasomee uinjinia wa ndege (aeronautics engineering, ambapo ana masters kwenye upande huo!). Mpaka sasa jamaa ni brigedia jenerali (kama sijakosea).
Alafu mzee yule ukimuona wala huwezi mdhania..! Very social!
 
Back
Top Bottom