Je, kuna kasoro katika kutamka kiswahili

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
13,997
15,111
Lugha hii mara nyingi hutamka neno mara mbilimbili KM:-
Pilipili
pikipiki
Tikitiki
tete
lialia
chuchu
kuku
koko

............. endeleza tuona wapi..!!!!
 
Hakuna kasoro na hali ya maneno hayo kujirudia ilitokea pale ambapo lugha ilipohitaji maneno mengi zaidi .Mf. wa maneno mengine ni kama :
sawasawa.
 
Hakuna kasoro na hali ya maneno hayo kujirudia ilitokea pale ambapo lugha ilipohitaji maneno mengi zaidi .Mf. wa maneno mengine ni kama :
sawasawa.
Mie naona kama washiriki na watunzi wa lugha walikuwa hawajiamini..!!!!
 
Zamiluni Zamiluni

Labda nianze kwa kusema Lugha yoyote huunda maneno ili kuongeza msamiati, kukuza lugha na pia kukidhi haja ya mawasiliano.

Kuna namna 10 za uundaji wa maneno katika lugha, sitazitaja zote najikita kwenye hii uliyo ionyesha inatwa "KUDURUFISHA" yaani kurudia neno moja mara mbili.

Mfn: neno "SAWA" ni kivumishi chenye hali ya usahihi lakini ukidurufisha neno hilo na kuwa "SAWASAWA" linakuwa kielezi cha mlinganganyo.

Hivyo ndio maneno huundwa. Nikupe kidokezo kidogo kuna maneno huundwa kwa kuzingatia matumizi Mfn: Fagio lilitokana na tendo fagia
Ufungua - tendo Fungua nk.

Soma mada ya UUNDAJI WA MANENO
 
ndio hizo nyenzake na "barabara" "katakata" ni katika kutengeneza misamiati ili lugha iwe inajitosheleza.
Shukrani "kemkem" tuta endeleza endeleza mlolongo wa kuukuza kupitia matawi na mifereji yote nahau yenye ufasaha.....
chomachoma/ vujavuja/ lialia/ lala/ konokono/ zeruzeru/ taputapu/ tonetone/ nk nk
 
Lugha hii mara nyingi hutamka neno mara mbilimbili KM:-
Pilipili
pikipiki
Tikitiki
tete
lialia
chuchu
kuku
koko

............. endeleza tuona wapi..!!!!
Baba
Bibi
Bubu
Cheche
Chacha
Chuchu
Dada
Dodo
Dudu
Fofofo
Gogo
Jiji
Kaka
Kiki
Koko
Kuku
Lala
Lulu
Mama
Mimi
Nini
Papa
Pipi
Popo
Barubaru
Sasa
Sisi
Sawasawa
Takataka
Wewe
Zuzu
 
Mie naona kama washiriki na watunzi wa lugha walikuwa hawajiamini..!!!!
Hapana sidhani kama ni kutokujiamini.Kama ilivyo unominishaji hata urudufishaji pia una dhima(kazi/umuhimu) zake kwa mfano neno vunja linapokuwa vunjavunja inaweza kuwa na maana zaidi (kuvunja bila mpangilio(hovyo) hivyo hivyo hata katika maneno pigapiga,chezacheza n.k
 
Back
Top Bottom