Je kuna haja ya kupiga kura Tanzania?


QUALITY

QUALITY

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2010
Messages
854
Likes
2
Points
0
QUALITY

QUALITY

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2010
854 2 0
Uchaguzi wa mwaka huu unatupatia mafunzo mengi sana. Matokeo ya udiwani na ubunge katika majimbo mengi yameishatangzwa. Katika majimbo mengi, hakukuwa na ulalamishi kwa sababu karatasi kutoka kwa mawakala zimetumika kujumlisha matokeo. Katika majimbo mengine kumwkuwa na fujo kwa sababu fulani akishinda, kura hazitangazwi. Mfano ni Ubungo, Kawe, Nyamahana n.k. Mpaka kura zihesabiwe mara tatu tatu. kama karatasi zilizotumika kuhesabu na kusainiwa na mawakala zipo, ya nini kuhesabu upya? Halafu kujumlisha kura ni zoezi la dakika kati ya 30 na 60, iweje itumie siku mbili au zaidi? wanatumia calculator au kuhesabu vidole?

Hapa kuna hoja kubwa ya kufanyia kazi. Kama kura za kina Mnyika zinachezewa inawezekana ni kwa sababu wakurugenzi wenyewe wanahofia kutamka kura hizo maana watapoteza kazi.

kwa jimbo la Segerea, ni tusi kwa wapiga kura kumtangaza Mahanga Makongoro. Mahanga kutangazwa mshindi ni kuwambia wapiga kura wa jimbo la segerea hawakuwa na haja ya kwenda kujipanga na kupiga kura kwa mtu wanayemtaka (Mpendazoe) na kisha wao wanamtangaza aliyeshindwa kuwa ndiye mshindi. Hapo haki iko wapi?

Halafu hapo ni katika jimbo ambalo ni dogo na ni rahisi kufuatilia kwa karatasi toka kwa mawakala. Je kwa rais ambaye karatasi hizo hatunazo? ufuatiliaji katika nafasi ya Urais unaweza kufanyikaje kwa usahihi? Je siyo nafasi ya kuwakatisha tamaa wapiga kura ili waseme "Hata nikipiga kura, zitaibiwa". Ili watawala, waendelee kutawala milele.

Mimi nadhani watanzania watapiga kura tutakapokuwa na tume huru ya Uchaguzi na tusitumie wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia uchaguzi ambao wameteuliwa na Rais!!
 
The Good

The Good

Senior Member
Joined
May 26, 2010
Messages
153
Likes
6
Points
35
The Good

The Good

Senior Member
Joined May 26, 2010
153 6 35
Bado kuna haja kupiga kura.

Kama watu wasingepiga kura hawa wabunge walioshinda (kwa vyama vyote) tungewapataje?
 
QUALITY

QUALITY

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2010
Messages
854
Likes
2
Points
0
QUALITY

QUALITY

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2010
854 2 0
You have a point, but Lakini kwanini maamuzi ya wananchi hayaheshimiwi? kweli wanaoshindwa na kuchakachua wana nia ya kuwawakilisha watanzania au wana lao jambo?
 
The Dreamer

The Dreamer

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2009
Messages
1,280
Likes
0
Points
0
The Dreamer

The Dreamer

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2009
1,280 0 0
Kuna haja ya kupiga kura lakini baada ya wizi wa kishindo sijui kama watu watajitokeza kupiga kura tena hasa kwa Tanzania bara
 
Digna37

Digna37

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2010
Messages
723
Likes
45
Points
60
Digna37

Digna37

JF-Expert Member
Joined May 17, 2010
723 45 60
Zamani nilikuwa sioni umuhimu. Lakini nakwambia kuna mapinduzi makubwa sana. Elimu tu, na matumaini mapya vitawafanya watu waone umuhimu wa kupiga kura kiasi ambacho wezi wataumbuka na kuiba watashindwa. Sivunjiki moyo tena kupiga kura maana matumaini yapo karibu sana.
 
G

Gurtu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2010
Messages
1,210
Likes
10
Points
135
G

Gurtu

JF-Expert Member
Joined May 15, 2010
1,210 10 135
Naomba nieleze habari ambayo nimeikumbuka baada ya kusikia matokeo ya Urais. Habari yenyewe iko hivi:

Wakati kampeni zimepamba moto huku maeneo ya Babati vijijini, siku moja nilikuwa na katibu wa Tawi la CCM katika sherehe. Wakati tunajadiliana juu ya ushindi ambao anaweza kuupata Dr. Slaa katika uchaguzi wa Oktoba 2010, yule katibu wa CCM alituambia jambo ambalo leo nikilikumbuka natamani nilie.

Yule katibu wa CCM alituambia kuwa Mkuu wa wilaya ya Babati aliwambia viongozi wa CCM katika tawi hilo kwenye vikao vya ndani kuwa "msihangaike na kura ya urais kwani hizo zipo tayari ila ninyi hangaikeni na kura za madiwani na mbunge kwani hao ndiyo watu wenu". Kwa matokeo haya ya sasa ambayo Jk ana kura nyingi ambazo zinamshangaza kila mmoja, nina kosa la kusema.

Hakika demokrasia imebakwa, Watanzania tumebakwa tena mchana. Kama mimi ni mwongo.....
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,218
Likes
878
Points
280
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,218 878 280
tunajua kabisa tuna akina mugabe wengine hapa tz no doubt.
 
Lucchese DeCavalcante

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Messages
5,473
Likes
68
Points
145
Lucchese DeCavalcante

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2009
5,473 68 145
tunajua kabisa tuna akina mugabe wengine hapa tz no doubt.
Hakuna marefu yasiyo kuna na ncha iko siku waTZ watasema tumechoka sasa basi
 
chobu

chobu

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Messages
308
Likes
17
Points
35
chobu

chobu

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2010
308 17 35
Haja ya kupiga kura ipo, tena ni haki ya msingi kabisa ya kila MTANZANIA kama Bunge litasimamia mabadiliko ya KATIBA iwe ya vyama vingi kuliko hii ya sasa ni chama kimoja. Bila kubadilisha katiba tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.
 
Abdulhalim

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2007
Messages
16,510
Likes
196
Points
160
Abdulhalim

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2007
16,510 196 160
Nakubaliana na maneno yako muungwana Quality.

Kuwahamasisha wananchi waache shughuli zao ili wajiandikishe, kushiriki mchakato wa kampeni na hatimaye kupiga kura BILA YA KUWA NA UTARATIBU TIMAMU KABISA WA KUJUA NANI MSHINDI, Nasema kwa kwa KINYWA KIPANA kwamba hiyo NI KAZI BURE. Sawasawa kabisa na KUTWANGA MAJI KWENE KINU. Vyama vyote vya upinzani vinavyojali mustakabali wa nchi hii viliangalie hili kwa kina katika chaguzi zijazo. Visijitumbukize kwene chaguzi kwa mihemuko na wala visiwachoshe watz kama hazina mikakati ya kuondoa udhaifu huu.
 

Forum statistics

Threads 1,235,787
Members 474,742
Posts 29,235,603