QUALITY
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 853
- 115
Uchaguzi wa mwaka huu unatupatia mafunzo mengi sana. Matokeo ya udiwani na ubunge katika majimbo mengi yameishatangzwa. Katika majimbo mengi, hakukuwa na ulalamishi kwa sababu karatasi kutoka kwa mawakala zimetumika kujumlisha matokeo. Katika majimbo mengine kumwkuwa na fujo kwa sababu fulani akishinda, kura hazitangazwi. Mfano ni Ubungo, Kawe, Nyamahana n.k. Mpaka kura zihesabiwe mara tatu tatu. kama karatasi zilizotumika kuhesabu na kusainiwa na mawakala zipo, ya nini kuhesabu upya? Halafu kujumlisha kura ni zoezi la dakika kati ya 30 na 60, iweje itumie siku mbili au zaidi? wanatumia calculator au kuhesabu vidole?
Hapa kuna hoja kubwa ya kufanyia kazi. Kama kura za kina Mnyika zinachezewa inawezekana ni kwa sababu wakurugenzi wenyewe wanahofia kutamka kura hizo maana watapoteza kazi.
kwa jimbo la Segerea, ni tusi kwa wapiga kura kumtangaza Mahanga Makongoro. Mahanga kutangazwa mshindi ni kuwambia wapiga kura wa jimbo la segerea hawakuwa na haja ya kwenda kujipanga na kupiga kura kwa mtu wanayemtaka (Mpendazoe) na kisha wao wanamtangaza aliyeshindwa kuwa ndiye mshindi. Hapo haki iko wapi?
Halafu hapo ni katika jimbo ambalo ni dogo na ni rahisi kufuatilia kwa karatasi toka kwa mawakala. Je kwa rais ambaye karatasi hizo hatunazo? ufuatiliaji katika nafasi ya Urais unaweza kufanyikaje kwa usahihi? Je siyo nafasi ya kuwakatisha tamaa wapiga kura ili waseme "Hata nikipiga kura, zitaibiwa". Ili watawala, waendelee kutawala milele.
Mimi nadhani watanzania watapiga kura tutakapokuwa na tume huru ya Uchaguzi na tusitumie wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia uchaguzi ambao wameteuliwa na Rais!!