Je kuna cheo cha katibu wa kitongoji kisheria?

Mosahe

Member
Feb 22, 2017
67
33
Mwenyekiti wa Kitongoji ana Katibu wake?
Kama anakuwa naye nipeni muongozo huo maana kuna shida imetokea kwenye kijiji kimoja eti kuna mtu anaitwa katibu wa kitongoji sasa anahudhuria vikao vya H/kijiji kwa cheo hicho baada ya mwenyekiti wa kitongoji kufariki.
 
kila kitongoji kina katibu, ni sahihi lakini km mwenyekiti kafariki fanyeni utaratibu wa kujulisha uongozi wa juu ili uchaguzi wa mwenyekiti huyo ufanyike
 
kila kitongoji kina katibu, ni sahihi lakini km mwenyekiti kafariki fanyeni utaratibu wa kujulisha uongozi wa juu ili uchaguzi wa mwenyekiti huyo ufanyike
umesema kuwa na katibu ni sahihi, je ni sahihi kisheria au kutabia/mazoea
 
Hapana si kisheria bali ni mazoea. soma GN no. 320 ya 2014 ya Sheria ya serikali za mitaa SURA, 287. nikanunu za uchaguzi ambao unataja Mwenyekiti tu si Katibu. Isipokuwa imekuwa ni mazoea vitangoji kuunda kamati ya kitongoji ambayo inakuwa mtendaji wa kitongoji kile
 
Kitongoji ni nini? Tuchanganye na kithungu ili twende sawa.Nijuavyo ngazi ya kwanza ya serikali ni kijiji au mtaa.Maeneo haya ndipo kuna watendaji/makatibu
 
Back
Top Bottom