je kulikua na sababu za msingi kwa mgomo wa madaktari kushughulikiwa na bunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je kulikua na sababu za msingi kwa mgomo wa madaktari kushughulikiwa na bunge?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by meningitis, Feb 6, 2012.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  wakuu,tukifuatilia sakata la mgomo wa madaktari tutaona kuna kusuasua katika kushughulikia jambo hili.inakaribia mwezi mzima sasa bila kuona kikomo cha mgomo huu wa kihistoria.kinachoendelea ni ubabe na kutunishiana misuli kati ya serikali na madaktari,hakuna suluhisho na maisha ya watu yanaendelea kuteketea.kinachoendelea ni vita ya propaganda huku serikali ikisubiri madaktari wakate tamaa.ni jambo moja la muhimu katika kutafuta suluhu ya mgogoro huu ambalo halijafanyika nalo ni kukutana kati ya serikali na madaktari,ninaposema serikali ni lazima tuwaweke pembeni wizara ya afya ambao ni watuhumiwa namba moja katika kuanzisha mgomo unaoendelea.
  Baada ya serikali kupitia pinda kuamini kwamba vitisho mikwara na dharau ni suluhisho la mgomo tumeona danadana nyingine zikitokea bungeni,eti suala hili waachiwe kamati ya huduma za jamii na wamalize kazi yao haraka iwezekanavyo(haina muda maalum)
  sawa sasa tukubali hiyo kamati itafanya kazi yake haraka je mapendekezo ya kamati yatachukuliwa kwa uharaka upi kama serikali hiyohiyo imeshindwa kutatua mgogoro huu kabla ya kufikishwa bungeni?kamati italeta kipi ambacho serikali haikijui?hizi ni hadaa za kipuuzi huku ndugu zetu wakiendelea kufa.sioni nafasi ya kamati hii ya bunge kuwarudisha madaktari kazini.kilichopo ni waziri mwenye dhamana na walio chini yake kuwajibika halafu kamati au tume ifuatilie nini chanzo cha tatizo na njia bora za kutatua matatizo ya madaktari.kamati hii itawahoji kina nani iwapo madaktari wamekatazwa kukaa kwenye vikao?sidhani kama kulikuwa na umuhimu wa kamati kupewa jukumu hili.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  atakaye amua mwisho wa mgomo ni serikali na sio bunge,bunge litapendekeza tu.
   
Loading...