Je, kufanya mazoezi gym ukiwa na umri mdogo kuna madhara?

Binman

Member
Jul 17, 2016
68
30
Halow,

Mimi ni kijana wa miaka 21. Nataka nianze kupiga gym but kuna tetesi nazipata kuwa kupiga gym katika umri mdogo kuna madhara.

Naombeni ushauri but napenda sana kupiga gym.
 
Mmh upo ktk mawazo yangu Leo kwa mala ya kwanza nusu tu niende gym kamvua kakaanza ko nikaailisha afu naona hii thread kua kuna madhara tena du ngoja wataalam waje tujue
 
Hivi 21 ni umri mdogo?
Inategemeana,,, but kuna tetesi niliipata kuwa kupiga gym at least uwe umefikisha 23,,, eti hapo ndo mifupa yako na misuli inakuwa imekomaa but sijapata proove... Ndo mana nimeuliza
 
piga tizi wewe acha uvivu gmy umri wowote unaenda ila zingatia aina ya mazoezi tuu
 
Ukiwa na umri wa miaka 18 au zaidi unaweza kwenda gym bila uangalizi wa mzazi. Wengine wanaweza kwenda wakiwa na umri wa miaka 16.

Jambo la muhimu siyo kuwa mazoezi yatakuadhiri kwa sababu ya umri wako mdogo bali uelewa wako wa kutumia mashine mbalimbali kwenye gym bila kujidhurika.

Siyo, unaenda pale unamwona jamaa anapiga squat ya kilo 100 na wewe unataka kubeba hizo kilo. Anza taratibu. Don't feel shy and you will get there. Nakumbuka nilianza na ule mchuma bila weight zozote.

Inashashauriwa unapoenda gym kwa mara ya kwanza bila kujali umri wako ni muhimu kuelekezwa jinsi ya kutumia mashine hizo.

So far sijawahi kusikia madhara ya yanayowapata teenagers kwa kwenda gym. Tena kwa umri wako ndo mzuri wa kupiga gym.

Tafuta threads za Castr ni "super perfect" hapa JF kwenye masuala ya mazoezi.
 
Thanks much..... Nimekupata kiongozi ila,,, ntakucheki pm
 
Kuna possibility ya kupata maradhi ya moyo ukiwa chini ya miaka 13..
 
Back
Top Bottom