Zanzibar 2020 Je, Kuapishwa kwa Maalim Seif kunatupa somo jipya katika Siasa za Tanzania?

Tusikate tamaa tuendelee kusimamia kile tunachokiamini hata kama wengi wanaweza dhani tumechanganyikiwa.
Siasa duniani kote haitoi nafasi ya kufanya unacho amini, ila hutoa nafasi ya wewe kufanya kile kinachotakiwa kufanywa muda huo.

Kwa wenye madaraka ndio huwa wanarusha kitu gani ukifanye kwa muda huo. Na utakacho ruhusiwa kukifanya ni kile kitacho wapa faida au hakito wadhuru.
 
Siasa za njaa upatikana tz zaidi.
Siku moja, Stalin alimnyonyoa kuku manyoya yake yote akiwa hai kisha akamuacha akiwa anatoka damu mwili mzima! Alipomrushia punje za ngano, yule kuku akaanza kumfuata! Kuona vile, Stalin akawaeleza viongozi waliokuwa chini yake akisema: "Hivi ndivyo inavyokuwa rahisi kuwatawala watu wapumbavu. Wataendelea kukufuata haijalishi unawatesa na kuwanyanyasa kwa kiasi gani ili mradi unawapatia maslahi kidogo hata kama ni mara mojamoja"!

Huo ndio uliokuwa mtazamo wa Kiongozi wa zamani wa Urusi!
Mtu mwenye njaa hawezi kuwa kiongozi bora
 
Naombeni kujua.keaiyo zanzibari kuna makamu wawili wa raisi ??
Ndio. Kwa muundo wa serikali ya kitaifa inayojumuisha vyama vyote ambayo ilianza kufanya kazi 2010 kuna Makamu wa kwanza wa Rais pamoja na Makamu wa pili wa Rais.
 
Siasa za njaa upatikana tz zaidi.
Siku moja, Stalin alimnyonyoa kuku manyoya yake yote akiwa hai kisha akamuacha akiwa anatoka damu mwili mzima! Alipomrushia punje za ngano, yule kuku akaanza kumfuata! Kuona vile, Stalin akawaeleza viongozi waliokuwa chini yake akisema: "Hivi ndivyo inavyokuwa rahisi kuwatawala watu wapumbavu. Wataendelea kukufuata haijalishi unawatesa na kuwanyanyasa kwa kiasi gani ili mradi unawapatia maslahi kidogo hata kama ni mara mojamoja"!

Huo ndio uliokuwa mtazamo wa Kiongozi wa zamani wa Urusi!
Mtu mwenye njaa hawezi kuwa kiongozi bora
Hakika ndugu umenena vyema. Nafikiria kipindi kile cha wakoloni kama mababu zetu wangeweka njaa mbele tungeweza kweli kupata uhuru? Jibu ni hapana Mandela alikubali kufungwa jela miaka 27 lakini na kufungwa kwake kote aliendelea kusimamia kile anachokiamini mpka pale muda ulipofika Afrika kusuni ikapata uhuru.
 
Siasa duniani kote haitoi nafasi ya kufanya unacho amini, ila hutoa nafasi ya wewe kufanya kile kinachotakiwa kufanywa muda huo.

Kwa wenye madaraka ndio huwa wanarusha kitu gani ukifanye kwa muda huo. Na utakacho ruhusiwa kukifanya ni kile kitacho wapa faida au hakito wadhuru.
Lakini siyo kila wanachotaka wao kifanyike ni sahihi. Inabidi vyama vya upinzani viwe na misimamo mikali ya mambo yale wanayoyaamini na siyo kufwata mtakwa ya watawala.
 
Mfano mmoja halisia; Jana nilikuwa na mazungumzo kuhusu Uchaguzi na Katibu wa kanda jina ninalihifadhi. Ananiambia uchaguzi huu umeacha makovu makubwa ya kila kitu pamoja na madeni sehemu alizopita Mgombea Urais Tundu Lissu.

Viongozi wa kanda ambao kwa kawaida hulipwa na Chama makao makuu mpaka muda huu hawajalipwa, mbali ya madeni yanayo wakabili hawajalipwa na wadai wameanza kuwa wasumbufu na kuanza kudai kwa karaha madeni yao.

Hali hii ikiendelea Mh. Mbowe atatusikiliza sisi ama itabidi wakati umlazimishe akubaliane na CCM ili wampe hiyo Ruzuku 196 millioni akinusuru chama na watumishi wake au aendelee kukomaa huku waajiriwa wa chama wanaondoka.

Wakati mwingi tunawalaumu kwa maamuzi hata sisi tungekuwa tukishikilia hizo offisi tungeamua kama wao wanavyo weza kuamua leo.
 
Hakika ndugu umenena vyema. Nafikiria kipindi kile cha wakoloni kama mababu zetu wangeweka njaa mbele tungeweza kweli kupata uhuru? Jibu ni hapana Mandela alikubali kufungwa jela miaka 27 lakini na kufungwa kwake kote aliendelea kusimamia kile anachokiamini mpka pale muda ulipofika Afrika kusuni ikapata uhuru.
Mnachekesha sana wote wawili, kwa kiufupi uhuru tulimdai mtu baki, Usawa wa kisiasa tunamdai kaka yetu..

Unavyo mshugulikia mtu baki kwa kawaida huwa tofauti sana na unavyo mshugulikia kaka yako.

Na kuchelewa kujitoa muhanga wa kisasa kutimiza majambo yetu kwa kuwa madai yetu tuyaelekeza kwa kaka yetu na sio mtu baki.
 
Heri mkoloni alituhurumia kuliko huyu kaka yetu.
 
Back
Top Bottom