Zanzibar 2020 Je, Kuapishwa kwa Maalim Seif kunatupa somo jipya katika Siasa za Tanzania?

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
263
250
Sasa ni rasmi Zanzibar imepata Makamu wa kwanza wa Rais. Hii imetokea siku ya leo tarehe 7/12/2020 baada ya Maalim Seif wa chama cha ACT Wazalendo kula kiapo.

Hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kushika nyadhifa hiyo kwani mwaka 2010-2015 akiwa mwanachama wa CUF pia alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais.

Wanzanzibar wenyewe walichagua Serikali ya Muundo wa kitaifa na ilipita kwa kishindo kwenye kura za maoni ambapo zaidi ya asilimia 60 waliunga mkono.

Dhima ya Serikali ya muundo wa kitaifa ni kuwaleta wanzibar pamoja na mfumo huu ulianza kutumika toka mwaka 2010.

Lengo la muundo huu wa kiserikali ni jema lakini kwa Katiba ya sasa CCM inapata faida zaidi na vyama vya upinzani vikiambulia patupu.

Tusisahau kwamba CCM ina idadi kubwa ya wajumbe wa Baraza la Uwakilishi huku mkono wa kushoto ukishika Mahaka na wakulia ukiwa na Dola.

CCM kamwe hawataweza kukubali kupatikana kwa sheria za uchaguzi zenye kuleta uhuru na haki nyakati za uchaguzi hilo tuliweke akili kwani kukubali kwao ndiyo kifo chao chama hicho cha kisiasa. Jambo hili ACT Wazalendo wanalijua kwani lipo wazi kwa wote.

Maalim Seif na wenzake wameona isiwe tabu, wamekataa kufa njaa, wamekubali kula, kunywa pamoja na kucheka na watesi wao.

Binafsi jambo hili hajinistua kabisa moyo wangu. Siku ya leo Maalim Seif akiwa anaapishwa alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.

“Moja ya yaliyofanya kukubali maridhiano ni imani yetu kwako Rais Mwinyi, vitendo na ishara zako ambazo zimetushawishi kuwa una nia njema na dhamira safi ya kututoa tulipokwama na kuibadilisha Zanzibar yetu katika nyanja zote”.

Najua wananchi wengi wa kawaida ambao walikuwa bado hawajaelewa michezo ya kisiasa inavyoenenda katika nchi hii hawakutemegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye kinywa cha Maalim Seif huku hata siku 50 hazijapita baada ya uchaguzi mkuuu kufanyika.

Lakini ndugu katika ulimwengu wa siasa mambo ndivyo yanavyoenda. Wazungu wana msemo wao unaosema kwamba “If you can’t defeat them, join them” ukimaanisha ukishidwa kuwashinda ungana nao.

Hilo ndilo jambo wanasiasa wanalifanya baada ya kukosa kile wanachokitaka wanabadilika kama upepo. Naamini kila Mtanzania mwenye akili timamu anapenda taifa lenye umoja lakini kwangu mimi umoja ni vitendo na siyo maneno ambayo wanasiasa wanayahubiri majukwaani wakituona sisi kama mazuzu tuyioelewa mambo.

Hawa wanasiasa wa upinzani wakiwa majukwaani katika harakati zao za kutafuta Madaraka wanatuonyesha mambo mauvo ambayo serikali inayafanya lakini pale wakiwekwa kwenye kumi na nane huisifia serikali na kugeuza nyeusi kuwa nyeupe.

Hilo ni somo ambayo nimejifunza katika siasa za Tanzania hasa kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani
Maswali mengi magumu bado yapo moyoni hasa nikiwaangalia wahanga wa uchaguzi ambao wengi ni wananchi wa kawaida wenye kipato duni.

Wapo wananchi ambao wamepoteza maisha na wengine wakipata vilema vya maisha kutokana na hamasa waliyoipata kwa kina Maalim Seif na kujitoa kwa moyo wote kuunga mkono harakati za chama cha ACT Wazalendo.

Binafsi najiuliza, kama jambo hili lilikuwa linawezekana kuzungumnzika mezani kwanini hawa kina Maalim Seif waliwatumia wananchi kama kete ya kupata kile wanacho kihitaji?

Tukumbuke kwamba hii ni mara ya pili kwa Zanzibar kuwa na Serikali ya umoja wa kitaifa. Swali jingine jepesi lenye majibu magumu ni Je, hawa ACT Wazalendo wanauhakika gani kwamba kushirikiana na CCM kutaleta mabadiliko katika chaguzi zijazo?

Ndugu zangu Watanzania itoshe kusema kwamba Wanasiasa wa vyama vyote wanauchu wa madaraka. Uchu wao wa madaraka hupelekea kututoa kafara sisi wananchi wa hali ya chini hasa wenye elimu duni.

Tuweni makini sana na hawa wanasiasa uchwara. Nashauri tuu tuache kuwa washabikia wa hawa wachumia tumbo. Tuungane kwa pamoja na tupiganie kupata Katiba ambayo itatenganisha majukumu ya Serikali, Bunge pamoja na Mahakama hapo ndipo tunaweza kupata mabadiliko ya kweli katika nchi yetu katika nyanja zote.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,894
2,000
Somo kubwa amelipata Amsterdam nadhani hatarudia tena kuwa kihere here na siasa za TZ
Watu wapigwe waumizwe wengine wachomewe nyumba zao halafu useme somo kalipata Amsterdam, hizi akili zenu za ajabu zitaendelea kuliangamiza taifa mkishirikiana na wapinzani uchwara kama hao ACT, na hao wafuasi wa ACT wakipenda waendelee kutumiwa tu.
 
ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,711
2,000
Sikuona haja ya TAL kukimbia nchi, aliahidiwa kazi na Rais.

Kweli mabeberu wamevishika vichwa vya baadhi ya watu.hapakuwa na ishara yoyote ile ya kufanyiwa hujuma wala nini.
Au atarudi akisikia DPP amemfutia kesi zake zoote?

Nikiwa kama mtanzania sijaona sababu ya yeye kukimbia nchi.sisi tunajivunia kushiriki kuijenga nchi yetu. aje tu teuzi zipo nyingi Sana cha msingi tu aridhike na atakachopata.

Mbona Maalim kakubali kufanya kazi.badala ya kuendelea kuchochea mbovu. T.A.L njoo bana utafanya kazi hata private sector kwenye mazingira mazuri.
 
ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,711
2,000
Sikuona haja ya TAL kukimbia nchi.aliahidiwa kazi na Rais.

Kweli mabeberu wamevishika vichwa vya baadhi ya watu.hapakuwa na ishara yoyote ile ya kufanyiwa hujuma wala nini.
Au atarudi akisikia DPP amemfutia kesi zake zoote ?

Nikiwa kama mtanzania sijaona sababu ya yeye kukimbia nchi.sisi tunajivunia kushiriki kuijenga nchi yetu. aje tu teuzi zipo nyingi Sana cha msingi tu aridhike na atakachopata.

Mbona Maalim kakubali kufanya kazi.badala ya kuendelea kuchochea mbovu.
T.A.L njoo bana utafanya kazi hata private sector kwenye mazingira mazuri.
 
LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
8,176
2,000
Haahaa SoMo ni kwamba mbwa anajifukuzia mwenyewe.Wapemba wamekula kila aina ya mateso mwisho wa siku seif Kaula na wake zake. Wapemba mkiambiwa habari za maandamano mjiongeze
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,276
2,000
1456109.jpg
457901234.jpg
 
LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
8,176
2,000
Sikuona haja ya TAL kukimbia nchi.aliahidiwa kazi na Rais.
Kweli mabeberu wamevishika vichwa vya baadhi ya watu.hapakuwa na ishara yoyote ile ya kufanyiwa hujuma wala nini.
Au atarudi akisikia DPP amemfutia kesi zake zoote ?
Nikiwa kama mtanzania sijaona sababu ya yeye kukimbia nchi.sisi tunajivunia kushiriki kuijenga nchi yetu. aje tu teuzi zipo nyingi Sana cha msingi tu aridhike na atakachopata.
Mbona Maalim kakubali kufanya kazi.badala ya kuendelea kuchochea mbovu.
T.A.L njoo bana utafanya kazi hata private sector kwenye mazingira mazuri.
Haahaa mkuu umewahi tandikwa hata risasi moja?
 
Mr_X

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
1,105
2,000
Watu wapigwe waumizwe wengine wachomewe nyumba zao halafu useme somo kalipata Amsterdam, hizi akili zenu za ajabu zitaendelea kuliangamiza taifa mkishirikiana na wapinzani uchwara kama hao ACT, na hao wafuasi wa ACT wakipenda waendelee kutumiwa tu.
Miezi miwili iliyopita mlikuwa mnawasifia ACT, tena hadi ikafikia hatua mgombea wenu wa uRais Zanzibar kwa chama chenu mkamtema ili kuwaunga mkono ACT, how leo wamekuwa wapinzani uchwara
 
Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,267
2,000
Kweli kabsa,cku ukichomwa mshale hutoongea hayo mashudu
Sikuona haja ya TAL kukimbia nchi.aliahidiwa kazi na Rais.
Kweli mabeberu wamevishika vichwa vya baadhi ya watu.hapakuwa na ishara yoyote ile ya kufanyiwa hujuma wala nini.
Au atarudi akisikia DPP amemfutia kesi zake zoote ?
Nikiwa kama mtanzania sijaona sababu ya yeye kukimbia nchi.sisi tunajivunia kushiriki kuijenga nchi yetu. aje tu teuzi zipo nyingi Sana cha msingi tu aridhike na atakachopata.
Mbona Maalim kakubali kufanya kazi.badala ya kuendelea kuchochea mbovu.
T.A.L njoo bana utafanya kazi hata private sector kwenye mazingira mazuri.
 
Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
263
250
Sidhani, Amsterm anajuwa kuliko unavyofikiria siasa zetu za kiafrika.
Nadhani huyo Amsterm anakazi yake maalumu na ikishapata anachokita atanyamaza kimya.
Jambo la Msingi ni kwamba matatizo yetu yata tatuliwa na sisi wenyewe lakini hawa Mabeberu wanatumia mwanya wa matatizo yetu kupata kile wanachokihitaji.
 
Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
263
250
Sikuona haja ya TAL kukimbia nchi.aliahidiwa kazi na Rais.

Kweli mabeberu wamevishika vichwa vya baadhi ya watu.hapakuwa na ishara yoyote ile ya kufanyiwa hujuma wala nini.
Au atarudi akisikia DPP amemfutia kesi zake zoote ?

Nikiwa kama mtanzania sijaona sababu ya yeye kukimbia nchi.sisi tunajivunia kushiriki kuijenga nchi yetu. aje tu teuzi zipo nyingi Sana cha msingi tu aridhike na atakachopata.

Mbona Maalim kakubali kufanya kazi.badala ya kuendelea kuchochea mbovu.
T.A.L njoo bana utafanya kazi hata private sector kwenye mazingira mazuri.
Tatizo ni kuacha kusimamia kile unachokiamini na kuamua kula peke yako na kuwasahau wananchi waliosimama nawe kipindi chote cha kampeni.
 
Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
263
250
Seif anatumia kila aina ya maneno kuhalalisha ugali wake, Mara ooh maridhiano ya kitaifa, Mara ooh umoja wa kitaifa.Aseme umoja wa viongozi kula marupurupu kule zanzibar na ving'ora.Nimemwelewa polepole sasa
Kweli watasema mengi lakini ukweli ni kwamba wamewasalimiti wanachama wao wa kawaida na sasa wap wanakula mema ya Nchi na CCM
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom