Mkandara,
Are you a betting man? It doesn't have to be money, we can bet reputations. Turudie hii thread baada ya uchaguzi.Mimi nasema Kikwete anashinda, no brainer, wewe unaweza kusema hivyo kwa Slaa?
Mkuu wangu naweza kusema kulingana na nafasi ya Dr. Slaa kabla na hadi kufikia leo hii - huko mbeleni sijui, Na sielewi Chadema wana mipango gani kuendeleza umaarufu alokuwa nao Dr.Slaa uzidi kupanda, sielewi Chadema wameweka mikakati gani ya kampeni dhidi ya ile ya CCM lakini hadi leo hii zikipigwa kura Dr.Slaa atamfunika JK kama nilivyofikiria siku za awali kwa kutazama uwezekano..Nashukuru Mungu, Chadema na Dr. Slaa waliweza kunisikia kwa hiyo..
Swala kubwa ulouliza kuhusiana na Chadema wamefanya nini au Dr.Slaa amefanya nini kustahili ushindi? Hakika unashindwa kuelewa kwamba kazi kubwa ya Upinzani popote pale duniani ni kutofanya kitu zaidi ya kuonyesha udhaifu wa uongozi, sera na ilani za chama ambazo zimeshindwa kuwaletea maendeleo.
Obama na Domocratic hawakufanya kitu chochote wakati Bush yupo madarakani isipokuwa waliweza kuonyesha mapungufu yake na wakaonyesha sababu ya uchumi wao kudondoka, Haki ktk Social issues, kuiweka Marekani ktk hatari zaidi (Usalama wa Taifa) pamoja na Mazingira.Na muhimu zaidi wao watafanya nini tofauti! - Huwezi kunambia ati Democratic walifanya nini kustahili ushindi au huyo Obama alifanya kipi kustahili kumshinda McCain - Hakuna.
Ndivyo ilivyo sehemu zote duniani, siku zote upinzani hawana sababu ya kununua madaraka kama hao kina Lowassa, Chenge na kina Mramba kutumia fedha zao za mfukoni kujiwekea nafasi ya ushindi hali Ubunge hautakiwi kuwa hivyo. Na maadamkweli sisi ni maskini watu kama Lowassa wamekuwa wakisifiwa zaidi pasipo kufahamu kwamba hwa viongozi wanauza Uhuru wetu, ardhi yetu na uzalendo wao kwa wawekezaji haramu ili mradi wapate fedha za ziada kununua wadhifa.
Loosers ni wananchi ambao taratibu wana loose ardhi, mashamba na nyumba zao na kadhalika kwa kufikiria wamejengewa barabara, hospital na Zahanati. Wabunge au viongozi kama hawa hawana tofauti na Barricks waliyoyafanya Bulyanhulu, Tarime na Kahama. Migodi yao (yetu) worth billions (maliasili) imechukuliwa bure kwa kuvutiwa maji toka Ziwa Nyanza na kujengewa barabara, shule na hospital wakati Barricks wakivuta mabillioni ya fedha. Tunauziwa vitu ambavyo vimeweza kuletwa na hata NGos za kidini (World vision) bure tumeuziwa na Barricks vitu hivyo hivyo kwa gharama kubwa ya Uhuru wetu. Na kwa ujinga huu wa kupenda vya bure CEO wa Barricks anaweza kugombea urais nchini akapewa vilevile.. ndio akili ya Mdanganyika.
Chadema hawana sababu, nia wala uwezo wa kuwachuuza wananchi kwasiasa kama hizi. Uzalendo wao (Patroitism) ndio utawaweka meza kubwa.