Elections 2010 Je Kikwete atakubali matokeo au atakuwa kama Mugabe

Mkuu kwa Tanzania hata sasa bado mambo ni easy tu. Simu moja inaweza kubadilisha matokeo na wananchi wakakaa kimya, bado wengi wetu tumelala. Mfano mzuri ni EPA, wezi wapo wanajulikana lakini mpaka leo wanapeta tena hao hao tumewachagua kwenye kura za maoni kuwa wagombea ubunge kwa chama chetu. It is so easy kuwadanganya watanzania waliowengi kwa kuwa wengi bado hawana uelewa wa nini kinachoendelea. This time CUF walikuwa wamefikia braking point, wanajua kuwa wakiibiwa mara ya tatu ni lazima pachimbike, ndio maana wameogopa kuiba kura.

Huku bara it happens every now and then, and it will keep on happning until wote tukiwa kama watu wa tarime au Zanzibar.

Inawezekana ni easy kuwa fool general population ambao hata hawapati habari, lakini wewe mwenyewe unavyosema "This time CUF wamefikia breaking point..." unaonyesha ugumu wa kuiba kura unapoanzia, you can only steal votes and rig elections so many times in a row.

Sasa mbinu za wizi zinazotumika Zenji si hizo hizo zinatumika bara? Kwa nini CCM wajishtukie Zenji na wasiweze kuwa contained bara? Vyama si vile vile ?

Inabidi wapinzani waweke mkakati ulio well coordinated kuhakikisha hawaibiwi kura. Vyama twawala vinashirikiana hivyo. Mugabe aliomba majeshi kuenda kumfundisha wizi wa kura kutoka Tanzania kina Kingunge wakaenda huko (some say hata January naye alikuwapo katika mchongo huo). Kwa hiyo kama hawa magwiji wanashirikiana katika hili kwa nini wapinzani nao wasiweke mkakati imara ?

Ikumbukwe majuto mjukuu hivyo.
 
You lack HOPE, Dear Kiranga.

Hope without the support of facts is delusion, a poisoning addictive drug with a deadly anticlimax

Kama kila mtu akikata tamaa hivyo itakuwaje?

Mimi sijakata tamaa, ndiyo maana nasema vote Slaa, lakini najua Slaa hawezi kushinda. Slaa akipata 25% sitakuwa disappointed. I am a realist who is not afraid to face the cold and ugly facts. If you are sick with a certain disease hoping may give you a placbo effect, but if you are really sick no hope can cure a disease, only hard work towards eradicating that disease, seeking medical help, applying the right medicine at the right dosage and things of that nature will help you. Right now we are really sick, and not much has been done, how can you have hope? Ingekuwa hope ndiyo solution watu tusingefanya kazi, tungehope kupata mahitaji yote na tungepata. Hope si solution, hope ni part ya tatizo, badala ya watu kuihold serikali reponsible, watu wana hope serikali itakuwa responsible yenyewe.Badala ya watu kufanya kampeni (upinzani) wana hope wananchi watawaelewa etc. Migodi inaangusha madongo na kuzika watu hai, badala ya watu kusisitiza quality control na responsibility, watu wanahope haitatokea tena, ris anasema ni kazi ya mungu, in other words ana hope mungu hatatupa maafa kama haya tena.

No sir, hope is not the solution.Hope is our problem.

You argue that he won by a huge margin last time and therefore he will win agin. Non sequitur. I does not follow. Hakuna wabunge walioshinda kwa asilimia kubwa hapo nyuma na sasa hawapiti hata kwenye primaries?

Kulinganisha chaguzi za wabunge na uchaguzi wa rais baada ya mambo yote niliyoyasema kuhusu "strongman" culture yetu ndiyo kitu ninachokiona kuwa "Non sequitur" hapa. Kama unafuatilia trends za uchaguzi wa rais kutoka Mkapa kwenda Kikwete asilimia ya kura zimeongezeka. The other point kwamba machoni pa Watanzania wengi Kikwete hajafanya kitu chochote gravely outrageous kama kum shoot mtu mchana kweupe kitakacho warrant a 30% tumble is not addressed. Hizi scandals zote na mabaya yote ya Kikwete less than 5% of the population know, of which half are Kikwete client's, the other 2.5% probably half of them won't even vote, they are out of the country or wont see the point. That is the unscientific guesstimation, a rather generous one if I might add. Wengine hao largely ni mali ya CCM, ukiacha wale wachache wtakaofanya "ana ana ana doo" na kuangukia upinzani by chance.I would be surprised kama upinzani ukipata 35% jumla. And I am being overly generous here too. Time will tell, let us revisit this thread after the election.

Kuhusu wizi wa kura, nikukumbushe kesi dhidi ya ushindi wa Ubunge wa Slaa. Unaikumbuka? Ulitolewa ushahidi mahakamani kwamba viongozi wa CCM walipita wakibadilisha matokeo ya kura zilizohesabiwa. Yaani idadi kama ya kura 170 kwenye kituo inabadilshwa kuwa 1700. Ndio maana kwenye vituo vingine idadi ya kura za CCM huzidi hata idadi ya waliojiandikisha.

Sijakataa wizi wa kura umetokea, hili nimeweka wazi tu hapo juu. Nilichosema ni kwamba, if the opposition people are sane at all, wizi wa kura uchaguzi huu utakuwa mgumu zaidi kwa sababu ya a simple issue of entopy, CCM wanavyozidi kuiba ndivyo wapinzani wanavyozidi kutakiwa kujua mbinu zao na kuzi block. Of course there is always the chance kwamba upinzani uko too slow na utaendelea kuruhusu CCM kuendelea kuiba kura, hapo wataweza kuni prove wrong. Na kwa kiasi kikubwa wizi wa kura ni crucial kwenye ubunge. Kama alivyosema Mwanafalsafa hapo juu, kuiba kura mpaka mtu ufikishe 80% kutoka under 50% is a bit of a stretch. Kuiba kura wakati kinachohitajika ni simple majority hakuleti mantiki, labda uwe na zealous partisans wanaoutaka ushindi wa "tsunami" tu, ambapo hapo issue inabadilika kutoka kuiba kura ili kubadili matokeo au sommersaults za kuremba ushindi zaidi (nevertheless nakemea wizi wa aina yoyote).

CCM haikuiba kura Zanzibar?
Nimesema hili hapo juu, sasa sijui hili ni rhetoric question?
Inafanya hivyo karibu chaguzi zote.

Right, lakini hapa tuna focus uchaguzi wa rais, like the last won Kikwete won by 80%, unataka kutuambia kaiba 30% ?
Uliza mitaani, utaambiwa watu walivyoona wenyewe masanduku yakitoroshwa na kujazwa kura za mgombea.

Mimi siulizi mitaani habari kama hizi, nikikaa na wakurugenzi wa usalama wa taifa wenyewe wanasema. Kwa hiyo this is not news to me, however, the discussion was about Kikwete na uchaguzi wa rais. Ambao najua hata kama kuna wizi huo wa kutaka kuremba ushindi, hauwezi kufikia 30%
 
Mkuu nakubaliana na wewe lakini maelezo yako haipaint the whole picture bali ina isolate eneno moaj. Kwanza kwenye hayo majimbo mkuu hizo ni chaguzi za ubunge wakati tunaongelea uraisi but I will give it the benefit of the doubt. Mkuu ukisema jimbo fulani mmegain hauelezei majimbo mliyo pungua. Kwa haraka haraka naweza nika taja majiimbo ambayo yalikua ya Chadema na yaka rudi CCM mfano jimbo lililo kuwa la Marehemu Chacha Wangwe (R.I.P.). So ukigain sehemu moja uka poteza nyingine hapo chama kina baki stationary.

Pia mkuu kuhusu msisimko uliopo sasa naomba Chadema muwe very careful kwa sababu perception can be very deceiving. Kwanza lazima uangalie hao wenye msisimko ni wakina nani? Na je ni asilimia ngapi ya wapiga kura? Maana hauwezi ukaona watu wa mijini au wasomi au wana JF wana msisimko ukaichukulia kama trend ya wapiga kura wote. That's why kwenye threa moja nime suggest vyama vya upinzani viwe vina fanya poll kuangalia ni wapi wana simama.

Kwa hiyo mkuu kwa sababu tunaangalia uachguzi wa uraisi lazima tuangalie nchi nzima na si majimbo mawili tu. Sawa Busanda na Biharamulo Chadema ili panda na kufikia asilimia 42 but hauja onyesha proof kwamba hii ni trend nchi zima bali ni sawa na kuassume kwa sababu ume faulu mtihani wa biologia basi na geographia nayo lazima utafaulu kutokana na matokeo ya biologia.

MwanaFalsafa1

Hata wanaofanya tafiti huwa wanachukua sample ya population hawaendi kila sehemu, Mag3 amekupa mifano ya Busanda na Biharamulo ambapo uchagu zi wa 2005 Chadema walipata 4% lakini baada ya miaka minne 2009 wakapata 48% kwanini isiwezekane kwenye maeneo mengine.

Halafu unavyosema wenye msisimuko ni wa mijini na JF tu kwani wewe unauhakika gani na unachosema. Hivi huko mikoani wanaomdhamini Slaa wote ni wamijini au ni wanaJF, je kuna wana JF wangapi wanafuatana na Slaa kwenye kampeni yake. Je na wale wanaotoka CCM na kujiunga Chadema nao ni wa mijini au JF.
 
Ccm haiondoki madarakani mpaka siku majina ya vyama pinzani na wagonbea wake watakapokuwa household brands.....

Jiulize wewe unaywzungumIa chadema hapa unazungumzia hizi siasa na mkwe wako wa kike? Mke wako?

Zanzibar wameshafika huko na ndo maana ccm Ina wakati mgumu na kulazimika kubadili matokeo......

Ccm bado Ina miaka angalau mitano mengine kabla ya kutikiswa kwenye nafasi ya uraisi
 
Mkuu unajuwa kuwa hamasa na msisiko wa kisiasa hapa JF kwa kiwango fulani ni mkubwa, lakini je vipi wale wengi ambao wanaishi vijijini kusiko na mitandao au websites je wanafikiwa na hizi hamasa!?
Hivi nyie mbona mnajidanganya hamasa ya JF ni tofauti na hamasa ya watu wa vijijini, JF tunachambua yanayotamkwa na viongozi watu wa vijijini wanasikiliza yanayosemwa, si lazima watu wote wawe na komputa ndipo wawe na hamasa. Nauliza tena hivi wanaohudhuria mikutano ya Slaa wote ni wana JF wenye komputa?
 
Wengi tunajua historia ya Zimbabwe kwa takriban chaguzi mbili hivi Mugabe anashindwa na mpinzani wake wa karibu Tsvangirai. Kwenye uchaguzi uliopita pamoja na chama cha MDC kuwa na wabunge wengi lakini Mugabe kwa ubabe wake bado anang'ang'ania ikulu.

Tunamuomba Kikwete asiige wala asithubutu kufanya hivyo maana ataliangamiza taifa na kuandika historia mpya. Hatutaki yatokee ya Zimbabwe na Kenya, kama alivyoingia salama ndivyo hivyo atakavyotoka salama na heshima yake italindwa, ni angalizo tu.

Naamin hakuna wa kumshinda Kikwete kabisa ila kutakuwepo na tofauti kubwa ya ushindi ikilinganishwa na mwaka 2005. Nasema hivyo kwa sababu Dr. atampunguzia wingi wa kura. Mkitaka kuitoa CCM madarakani ni kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 na siyo wakati huu. Nyota ya Kikwete inang'ara kuliko ya Slaa.
 
Siri kubwa ni aina ya watu. Ni kweli Slaa ni mgombea mwenye nguvu binafsi na slaa anaweza kuibeba CHADEMA kwenye uchaguzi. Lakini mimi nimekuwa convinced na hoja za Kiranga. Test nyepesi ni aina ya Wagombea Ubunge Chadema itasimamisha katika Majimbo ya uchaguzi. Swali la kwanza itasimamisha wagombea katika majimbo yote? Kwa nini isiwe majimbo yote? Je itasimamisha wagombea wa aina ile tuliyoiona Busanda na Tarime kwenye Chaguzi ndogo?

Time of truth ni huu wakati wanapoteuliwa watu kugombea Ubunge. Tumeona jinsi CCM Primaries zilivyokuwa hotly contested. Kwa upande wa Chadema je hali iko hivyo? Aina ya wagombea Ubunge watakaopatikana ndo watakuwa back-up za Mgombea Urais katika majimbo husika. Ikiwa kuna majimbo Chadema haitasimamisha mgombea au katika majimbo Mengi Chadema itasimamisha Bora wagombea, ujue hii inampunguza na kum-dilute mgombea wa urais (ni push and pull effect). Slaa atavutia watu, lakini wagombea Ubunge dhaifu watawafukuza wapiga kura wengi vile vile. Ukweli ni ukweli hata kama si mzuri sana maskioni, Kikwete hatahitaji kuiba kura wala kucheza faulo. Najua sitampigia kura, ila hiyo hainipi matumaini ya uongo kuwa nitakayempigia kura atashinda. Pengine kusema wazi wazi hapa ndo watu wasichopenda!

Ukiangalia Primaries za CCM zilivyoendelea unazidi kujua jinsi nchi hii tulivyo ingia kwenye hatari kubwa kabisa, yaani kama mgonjwa ni yule wa ICU tena ya Muhimbili (ambako ni kama 30% tu hutoka wazima). CCM hawawezi kujizuia tena kucheza rafu na 99% ya wagombea wa CCM (hiyo asilimia moja ni wale waliopita bila kupingwa) wanaamini kuwa ushindi bila kucheza rafu haiwezekani. Hata wanachama wa chama chenyewe wanaoshiriki chaguzi wanajua kuwa rushwa ni lazima ili kupiga kura. Kila mgombea aliyepoteza ana horror stories za rushwa zinazokinaisha. Kwa mtazamo huo, ni kweli kabisa bado watu wataona ni lazima washiriki jadi yao ya kuiba kura hata pale isipolazimika. Lakini hata hiyo haitoshi kuelezea kushindwa kwa wagombea wa upinzani.

Slaa akipata asilimia hata 25% na Chadema ika-double idadi ya Wabunge bado mi nitaona kama mafanikio positive kabisa. Katika jimbo langu, kura zangu tatu zitaenda Chadema, kwa sababu wagombea wote watatu wanachagulika. Ila nikiangaza kurunzi katika majimbo mengine naweza kuona kabisa zaidi ya asilimia 50% ya wagombea wa Ubunge na Udiwani wa Chadema wakiwa si watu wanaochagulika. Ni kuwa mkweli katika nafsi yangu tu!
 
Kikwete hana confidence baada ya Dr. Slaa kujitosa kama mgombea urais. Hata hivyo, kama alivyoandika Mzee Mbwambo katika gazeti la Raia Mwema kwenye article yake yenye kichwa cha habari "Ya Jenerali Guel, Dk. Slaa na chaguzi zetu!" Mzee Mbwambo amehadithia kwa kina na kwa mifano jinsi ambavyo viongozi wengi wa Afrika huwa hawakubali matokeo kiasi cha kuamua kuyapindisha kwa sababu moja kubwa - kutokuwepo kwa TUME HURU YA UCHAGUZI. Ametoa mifano ya jinsi ambavyo Jenerali Robert Guel wa Ivory Coast, baada ya kuona ameshindwa uchaguzi akakataa matokeo yasitangazwe na kusema kwamba "Hayana manufaa" (not useful). Mzee Mbwambo akabainisha kwamba katika siasa za Afrika za viongozi kupenda madaraka kupindukia, kwenye chaguzi za kutafuta rais wa nchi unaweza kushinda kwa kura lakini usishinde urais. Kwa kuthibitisha kwamba hayo si maneno matupu akatoa mifano:
Mwaka 1995 katika uchaguzi mkuu, CUF ilishinda. Seif Shariff Hamad alimbwaga Dk. Salmin Amour (Komandoo) wa CCM, lakini kabla hayajatangazwa rasmi Komandoo Salmini aliona "hayana manufaa (not useful)" CCM ikaelekeza yacheleweshwe kidogo kutangazwa ili itafutwe mbinu kukokotoa/kupika tarakimu itakayoonyesha kwamba Dk. Salmini ndiye mshindi. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar wakati huo Bwana Zuberi Juma Mzee ikabidi atangaze kwamba aliyeshinda ni Komandoo na si Seif Shariff. Mzee Mbwambo akaeleza kwamba hiyo ndiyo maana ya yeye kusema kwamba "unaweza kushinda kura lakini usishinde urais!"

Akaendelea kutoa mfano wa majirani zetu Kenya mwaka 2008 ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya alipompelekea Rais Kibaki matokeo kwamba ameshindwa na Odinga, akamkuta Kibaki ameishaita Jaji Mkuu kwa madhumuni ya kumwapisha kuwa Rais huku akijua kwamba ameshindwa uchaguzi! Kibaki aliyaona matokeo ya uchaguzi "not useful" akaamua kumdhulumu Odinga!

Mfano mwingine ni wa Rais Mugabe wa Zimbabwe ambaye naye alijikuta ameshindwa na kiongozi wa upinzani Morgan Tshangarai. Naye hivyo hivyo akayaona matokeo yale sio "useful." Tshangarai akawa amenyimwa haki yake ya kuwa kiongozi wa Zimbabwe.

Nampenda Mzee Mbwambo, anaendelea kutuambia kwamba kosa ambalo vyama vya upinzani hapa nyumbani vimefanya ni kutoshinikiza Serikali ibadilishe katiba ili iwepo TUME HURU YA UCHAGUZI ili kuzuia vitendo vya aina hiyo vya marais walio madarakani kubadilisha matokeo ya kura pale wanapogundua kwamba wameshindwa.

Kwa wale ambao tunapenda kudokoa baadhi ya maneno wanayosema wanasiasa majukwaani na kuyawekea tafsiri zetu, ni kwamba wakati JK anarudisha ama kuchukua fomu alieleza jinsi ambavyo CCM ina mtandao mpana hadi kwenye nyumba kumi kwa hiyo ina uhakika wa kushinda. Ikanikumbusha jinsi ambavyo mjumbe wetu wa nyumba kumi alikuwa akilazimisha kutaka kujua iwapo tumekwenda kujiandikisha kupiga kura. Ni jambo jema kuhimiza wananchi kujiandikisha kupiga kura. Lakini, kwa CCM tunayoijua inayonuka uvundo wa rushwa kwenye chaguzi na hujuma kwenye matokeo ya kura, haitashangaza hata kidogo kwamba tayari CCM kuanzia ngazi ya shina tayari wameishasukwa na kupewa maelekezo ya nini cha kufanya kwa kutumia mizengwe na hadaa ili CCM ishinde. Wapo wananchi waliokata tamaa ambao wala hawakutaka kwenda kujiandikisha, huenda majina yao yameshachukuliwa ili yatumike kuipa CCM ushindi wa bandia endapo kura za JK hazitatosha!

Naamini kabisa maji yakiwafika shingoni CCM watayaona matokeo "not useful" na watarudia kufanya ujangili wa kuyabadilisha!
 
Hivi nyie mbona mnajidanganya hamasa ya JF ni tofauti na hamasa ya watu wa vijijini, JF tunachambua yanayotamkwa na viongozi watu wa vijijini wanasikiliza yanayosemwa, si lazima watu wote wawe na komputa ndipo wawe na hamasa. Nauliza tena hivi wanaohudhuria mikutano ya Slaa wote ni wana JF wenye komputa?
Duh! Pole mkuu sina uhakika kama umenielewa...!
 
Kamwe hawezi kukubali matokeo na mfano mdogo tu ni pale tuhuma za ufisadi zilipoibuliwa na Dr. SILAHA walisema kwa jicho kavu kuwa ni uzushi na uongo sembuse matokeo!! na ndola wanashikilia wao.
 
Kwamba JK atakubali kushindwa au la ni swala la kusadikika,the man will WIN,tu discuss percentage.

Mugabe na Zimbabwe ni suala tofauti kabisa na Tz
 
Kwamba JK atakubali kushindwa au la ni swala la kusadikika,the man will WIN,tu discuss percentage.

Mugabe na Zimbabwe ni suala tofauti kabisa na Tz
 
Wanabodi,
wakuu zangu kwanza namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia kuyaona mambo mengi ambayo watu wengine huyapuuza au kuyafanyia mzaha. Niliwahi kusema wazi kwamba coalition baina ya CCM na CUF hakika loosers will be CUF. Na hata baada ya kura za maoni na kuwaona Wazanzibar wengi (pro CUF) wakishangilia USHINDI, lakini wameshindwa kuelewa kwamba it's CCM who walks away as a winner..

Nasema hivi kwa sababu mwaka huu CCM wasingeshinda kabisa uchaguzi na hakika ingebidi wizi utokee tena mkubwa hivyo kungekuwa na hali mbaya zaidi kwa CCM na utawala wake. Lakini kwa kutumia mbinu huku wakijua fika kwamba hawawezi kushinda uchaguzi huu wamekubali muafaka wa ku share uongozi hata kabla ya uchaguzi. Na CCM watashika usukani wao regardless ya matokeo - washinde washindwe.

Sasa kama CUF ndiye angekuwa mshindi iweje leo CUF wafikirie kwamba serikali ya mseto ni ushindi kwao na sii kwamba wamemeza a bitter pill..na kibaya zaidi ni kwamba maumivu yatabakia palepale. Hii ndio CCM wakuu zangu, ina kila mbinu za kuwazuga watu wasiweza kuona mbali.

Na hii habari ya kusema Dr.Slaa hawezi kushinda mtakuja shika tama siku ya siku kwani hisia zangu ni kali sana ktk utetezi wa DR.Slaa. Chadema kama Chama mwaka huu wataonyesha maajabu sana na hakika hata kama DR.Slaa hatashinda lakini matokeo mtayaona kwenye Madiwani na Wabunge kama Chadema wataweza kuhakikisha uhesabuji wa kura unakuwa wazi na hakuna maswala ya kulaza siku kuhesabu kura au rabsha ktk usafikirishaji wa masanduku ya kura.

Sina hakika kabisa kwamba JK atashinda uchaguzi huu, na nasema wazi kwamba hata wao CCM wameweka nguvu yao kubwa ktk kuchukua Bunge (mtandao) kwa maandalizi ya mwaka 2015. Na siku zote nimekuwa nikisema na kusisitiza kwamba Adui yetu sii Kikwete na wala hamtaweza kujua hadi siku ya siku isipokuwa jueni moja - Nawahakikishieni kwamba JK anapigwa vita nje na ndani ya chama chake mwenyewe na Dr.Slaa anaweza kabisa kupenya ktk penyo waliyoiacha.

Utabiri wangu umekamilika!
 
Kwanza Kiranga ajue kuwa na "hope" haimaanishi kutegemea mambo yajifanye yenyewe. Ni kutokata tamaa. Yeye Kiranga kakata tamaa kwamba CCM inaweza kushindwa. That is regardless of the analysis done. Watu walidhani hivyo hivyo kwamba KANU na UNIP hazishindiki, lakini zimeshindika.

Kusema Slaa hawezi kushinda ni kukata tamaa. To not have hope is to give up. It does not mean all those et ceteras that you have attributed to it. Na ni vibaya kukata tamaa. Kuna waliokuwa wamekata tamaa kwamba Wamarekani Weusi wangeweza kuwa Rais mapema hivi. Na walikuwa na vijianalysis vyao kama hivi vya Kiranga. They were wrong.

Hata Kiwete anadhani kwamba Slaa anaweza kushinda. That is why he has panicked sufficiently to increase salaries at this time. Only a desperate leader would hike salaries at a time when almost all the money had already been siphoned off for election bribery.

Hayawi, hayawei, yatakuwa. Kiranga, una lengo la kutukatisha tamaa?
 
Kwanza Kiranga ajue kuwa na "hope" haimaanishi kutegemea mambo yajifanye yenyewe. Ni kutokata tamaa. Yeye Kiranga kakata tamaa kwamba CCM inaweza kushindwa. That is regardless of the analysis done. Watu walidhani hivyo hivyo kwamba KANU na UNIP hazishindiki, lakini zimeshindika.

Kusema Slaa hawezi kushinda ni kukata tamaa. To not have hope is to give up. It does not mean all those et ceteras that you have attributed to it. Na ni vibaya kukata tamaa. Kuna waliokuwa wamekata tamaa kwamba Wamarekani Weusi wangeweza kuwa Rais mapema hivi. Na walikuwa na vijianalysis vyao kama hivi vya Kiranga. They were wrong.

Hata Kiwete anadhani kwamba Slaa anaweza kushinda. That is why he has panicked sufficiently to increase salaries at this time. Only a desperate leader would hike salaries at a time when almost all the money had already been siphoned off for election bribery.

Hayawi, hayawei, yatakuwa. Kiranga, una lengo la kutukatisha tamaa?

Mwalimu,

Kitu gani kinakupa matumaini hivi? Mimi sikatai matumaini, ila kwe na balance basi baina ya kuwa overly optimistic na kuwa overly nihilistic, hapo ndipo unapata realist.

Hivi upinzani umefanya nini cha ajabu ku close hiyo gap ya 30% ? Kitu gani hasa walichokifanya wapinzani kiwasababishie ushindi? Na Kikwete anaendeleza showmanship yake ya "Ndugu wananchi blah blah blah" anapandikiza data za uongo na kweli, anakupa figures za shule za makuti alizojenga, anakufunga kamba za ajenda yake kwa miaka mitano iliyobaki etc na vile watanzania wasivyouliza anapeta.

Upinzani umefanya nini cha ajabu ku close the gap? Unajionyeshaje kwa wananchi kwamba unaweza?

Kuna mkuu katoa point muhimu ana kuhusu wagombea ubunge, watanzania wengi (sio wote) ukianza kuwawekea economic data utawa bore tu, wao wataangalia mtu wanayemjua, mtu mwenye haiba ya uongozi hata kama ni kiongozi mbovu. CHADEMA so far choices zao za wagombea ubunge, ukiacha watu wachache, si attractive hivyo, na watu wengi wataona hiyo kama sababu ya kumpigia Kikwete pia. Vote for the guy with the team, not with the dream, watasema.

Mimi ni mmoja wa watu ambaye ningependa kuona mabadiliko Tanzania lakini CHADEMA bado hamna team, hamna candidates, na mnahitaji miaka kadhaa ya maandalizi.

If you were a betting man I would say put your money where your mouth is, but I suspect you are piously not so since you have been ignoring my betting advances since yesterday.Mara nyingine kuargue sana kabla ya uchaguzi inakuwa blah blah, you just put your money where your mouth is and wait for the election.

Oh, I almost forgot, even if Kikwete wins by a landslide the opposition will cry he won by foul.Of course he will win by foul stupid, he has the entire machinery against your one gun army. no llevel playing field.

Which will mean he does not have to steal votes.
 
Wanabodi,
wakuu zangu kwanza namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia kuyaona mambo mengi ambayo watu wengine huyapuuza au kuyafanyia mzaha. Niliwahi kusema wazi kwamba coalition baina ya CCM na CUF hakika loosers will be CUF. Na hata baada ya kura za maoni na kuwaona Wazanzibar wengi (pro CUF) wakishangilia USHINDI, lakini wameshindwa kuelewa kwamba it's CCM who walks away as a winner..

Nasema hivi kwa sababu mwaka huu CCM wasingeshinda kabisa uchaguzi na hakika ingebidi wizi utokee tena mkubwa hivyo kungekuwa na hali mbaya zaidi kwa CCM na utawala wake. Lakini kwa kutumia mbinu huku wakijua fika kwamba hawawezi kushinda uchaguzi huu wamekubali muafaka wa ku share uongozi hata kabla ya uchaguzi. Na CCM watashika usukani wao regardless ya matokeo - washinde washindwe.

Sasa kama CUF ndiye angekuwa mshindi iweje leo CUF wafikirie kwamba serikali ya mseto ni ushindi kwao na sii kwamba wamemeza a bitter pill..na kibaya zaidi ni kwamba maumivu yatabakia palepale. Hii ndio CCM wakuu zangu, ina kila mbinu za kuwazuga watu wasiweza kuona mbali.

Na hii habari ya kusema Dr.Slaa hawezi kushinda mtakuja shika tama siku ya siku kwani hisia zangu ni kali sana ktk utetezi wa DR.Slaa. Chadema kama Chama mwaka huu wataonyesha maajabu sana na hakika hata kama DR.Slaa hatashinda lakini matokeo mtayaona kwenye Madiwani na Wabunge kama Chadema wataweza kuhakikisha uhesabuji wa kura unakuwa wazi na hakuna maswala ya kulaza siku kuhesabu kura au rabsha ktk usafikirishaji wa masanduku ya kura.

Sina hakika kabisa kwamba JK atashinda uchaguzi huu, na nasema wazi kwamba hata wao CCM wameweka nguvu yao kubwa ktk kuchukua Bunge (mtandao) kwa maandalizi ya mwaka 2015. Na siku zote nimekuwa nikisema na kusisitiza kwamba Adui yetu sii Kikwete na wala hamtaweza kujua hadi siku ya siku isipokuwa jueni moja - Nawahakikishieni kwamba JK anapigwa vita nje na ndani ya chama chake mwenyewe na Dr.Slaa anaweza kabisa kupenya ktk penyo waliyoiacha.

Utabiri wangu umekamilika!

Mkandara,

Are you a betting man? It doesn't have to be money, we can bet reputations. Turudie hii thread baada ya uchaguzi.Mimi nasema Kikwete anashinda, no brainer, wewe unaweza kusema hivyo kwa Slaa?
 
Kichuguu you nailed it.Watu wanafikiri kuiba mmatokeo ni rahisi tu.

Wewe unafikiri kwa nini CCM wamekubali muafaka Zanzibar, CCM na uchu wao wote wa kuhodhi madaraka na uhasama wote uliokuwa Zanzibar.

Wameona kila siku zinavyozidi, kila wanavyoiba, ndiyo mbinu zao zinavyojulikana. Wakaona sasa hapa siku CUF watashinda, tutashindwa kuiba, tutakuwa nje ya serikali kabisa. Bora tuingie muafaka ni insurance policy, wakishinda CUF at least tutakuwamo katika serikali ya mseto.

Kuiba kura si rahisi hivyo.

na wakishakuwa kwenye hiyo serikali wataangalia upepo baada ya miaka mitano kama upepo ni mzuri wanaifuta hiyo serikali kaazi kweli kweli huu mseto hata mimi niliouna hivyohivyo ugumu wa kuiba kura
 
Back
Top Bottom