Je, kati ya Nuhu wa safina na Genghis Khan nani apewe heshima ya kuwa baba wa vizazi ulimwenguni?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,689
106,812
Salute Intellectuals..
Wakuu naomba kuuliza kati ya Genghis Khan na Nuhu wa safina nani baba wa vizazi ulimwenguni?
Biblia inasema..
1 Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.
Mwanzo 10 :1


2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
Mwanzo 10 :2


3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
Mwanzo 10 :3


4 Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
Mwanzo 10 :4


5 Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
Mwanzo 10 :5


6 Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
Mwanzo 10 :6


7 Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
Mwanzo 10 :7


8 Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
Mwanzo 10 :8


9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
Mwanzo 10 :9


10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
Mwanzo 10 :10


11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
Mwanzo 10 :11


12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.
Mwanzo 10 :12


13 Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
Mwanzo 10 :13


14 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.
Mwanzo 10 :14


15 Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
Mwanzo 10 :15


16 na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,
Mwanzo 10 :16


17 na Mhivi, na Mwarki, na Msini,
Mwanzo 10 :17


18 na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.
Mwanzo 10 :18


19 Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
Mwanzo 10 :19


20 Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
Mwanzo 10 :20


21 Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana.
Mwanzo 10 :21


22 Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu.
Mwanzo 10 :22


23 Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
Mwanzo 10 :23


24 Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi.
Mwanzo 10 :24


25 Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani.
Mwanzo 10 :25


26 Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera,
Mwanzo 10 :26


27 na Hadoramu, na Uzali, na Dikla,
Mwanzo 10 :27


28 na Obali, na Abimaeli, na Seba,
Mwanzo 10 :28


29 na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
Mwanzo 10 :29


30 Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki.
Mwanzo 10 :30


31 Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
Mwanzo 10 :31


32 Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.
Mwanzo 10 :32


Genghis Khan ni nani..?
Genghis Khan or Chinggis Khaan[note 3](born Temüjin,[note 4] c. 1162 – August 18, 1227), was the founder and firstGreat Khan of the Mongol Empire, which became the largest contiguous empirein history after his death. He came to power by uniting many of the nomadic tribes ofNortheast Asia. After founding the Empire and being proclaimed "Genghis Khan", he launched theMongol invasions thatconquered most of Eurasia. Campaigns initiated in his lifetime include those against the Qara Khitai, Caucasus, andKhwarazmian,Western Xia and Jindynasties. These campaigns were often accompanied by large-scale massacres of the civilian populations – especially in the Khwarazmian and Western Xia controlled lands. By the end of his life, the Mongol Empire occupied a substantial portion of Central Asia andChina.

Sasa ipo hivi..
Historia iliyopo duniani tunaambiwa Nuhu ndio baba wa mataifa yotee baada ya Gharika kuu Lakini
Huyu Genghis Khan alizaa na watu wengi wengi sana kutokana na vamizi zake za kujipanulia utawala, kila alipopita aliacha lundo la watoto Hivyo basi Tafiti za kisayansi (DNA) zinasema Ukichukua watu kumi ukapima DNA yao basi watuNane Dna yao ita link na Dna za Genghis Khan. Hivyo Bloodlines yake imesambaa dunia nzima!


Sasa naomba kujua tu bandugu nani apewe heshima ya baba wa mataifa?
Cc.
wick zitto junior rajabkisauti
 
Huyu Genghis Khan anatakiwa apewe heshima yake sababu ndio mtu aliyeleta ustaarabu mzuri sana duniani lakini sijajua kwanini Baada ya kufa majenerali wake aliamua wamfiche alipozikwa (hajulikani alipozikwa na waliomzika au kushuhudia msafara waliuawa kuficha siri).
Kwangu mimi ingawa hawa wote ni stori za kufikirika lakini ya Genghis Khan ina ushahidi ukifatilia unaambiwa huyu jamaa vizazi vyake vimeenea hadi Mongolia, India, China, Russia, Asia na huko Middle East. Basi nitampa kura yangu yeye, Nuhu atabaki kuwa biblical figure lakini sioni impact yake kwenye jamii!..
 
A bit off the topic, but just to be curious; Hao walioua wenzao ili kuficha siri za mahali alipozikwa Khan ni akina nani nao waaminike kuwa wasingeweza kutoa siri mahali alipozikwa?
 
Huyo Genghis Khan wakati wa gharika alijificha wapi asiangamizwe?

Maana hakuna kiumbe ambacho kilikuwa nje ya safina kilichopona ndio maana Nuhu ndio anatajwa kuwa mwanzo wa vizazi baada ya gharika
Hakuna kiumbe kilichpona??
samaki pia waliinguzwa kwnye safina??!!
 
Hakuna kiumbe kilichpona??
samaki pia waliinguzwa kwnye safina??!!
MWA. :7:21
Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;

MWA. :7:22
kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.

MWA. :7:23
Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina.

Hakuna chochote kilichokuwa nje ya safina kilichopona kwa hiyo waliingia pia samaki
 
I assume unaamini katika Biblia pamoja na historia yake and this is why umeleta ushahidi wa maandiko ya Biblia kama reference; again unaamini katika sayansi na ndio maana umeleta mambo ya DNA kama reference as well; well, mimi ndio nasoma leo habari za huyo mhindi mwenye vizazi vingi namna hiyo, before nilikua sijui so thumb to you kwakua nimeongeza knowledge; back to the topic; Kwenye hayo maandiko ya Biblia, kabla ya hapo dunia ilikua na watu waliokua sehemu tofauti tofauti though I think mostly if not all walikua maeneo ya mashariki ya kati na hasa nchi ya Iraq (other Bible scholars wanaweza kuongeza) so Nuhu/Noah aliishi maeneo hayo (hi ni kutokana na mito na milima inayo tajwa hapo kama mto Frati na mlima Hararati, vinapatikana Iraq or mashariki ya kati) kwenye hilo gharika la Nuhu tunaambiwa watu wote walio kua duniani wakati huo walikufa maji except Nuhu na mkewe pamoja na wanae hao 3 wakiwa na wake zao so waliopona ni watu 8 tu dunia nzima ya wakati huo, then baada ya gharika Nuhu hakuzaa tena (I assume kwasababu ya umri) but watoto wake hao 3 walizaa watoto ambao kupitia wao ndio dunia ya leo, Swali, huyo Mhindi aliishi miaka ipi!?
 
MWA. :7:21
Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;

MWA. :7:22
kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.

MWA. :7:23
Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina.

Hakuna chochote kilichokuwa nje ya safina kilichopona kwa hiyo waliingia pia samaki
Samaki hawajatajwa hapo!
Ikiilezwa juu ya nchi ina maana bahari haipo sababu bahari sio juu ya nchi!u got my point
 
Back
Top Bottom