Je, kanisa la TAG nalo limeunga juhudi?

Je, kanisa la TAG nalo limeunga juhudi?

Makanisa ni ROMAN CATHOLIC na LUTHERAN wengine ni njaaa kwenda mbele, Mimi nilikuwa Msabato nikaamua kuacha mara baada ya kuona wanaunga juhudi
Leo Mh Rais amepewa tuzo na kanisa ambalo enzi za Lina Lazaro na Mzee Klora lilikuwa ni kanisa ambalo lilitela matumaini.

Sipingi kumpa tuzo lakini naangalia hotuba ya Askofu mkuu Bwana Mtokambali kwa kuamua kuwa sehemu ya praise timu bila kuangazia mambo ambayo katika jamii yamezorota kuliko vipindi vyote vya urais wa nchi hii.

1. Watu kupigwa risasi
2. Watu kupotea
3. Kutekwa na kuteswa
4. Kuokotwa mitaani na kwenye fukwe za baharini

Mambo hayo ndiyo kanisa lilitakiwa kuwa jicho. Hakuna nabii kwenye Biblia aliye heka na mfalme mwovu.

Tanzania Assemblies of God, mmepotoka!

View attachment 1536928
 
Ukisoma unabii hasa kitabu cha ufunuo hao unaowasema wanaitwa manabii wa uongo. Yaani ktk zile roho tatu za mfano wa vyura hao hao ndugu zetu wanasimama kwa yule nabii wa uongo. Hawana lolote hao wasanii tu hao.
 
Hao ni vijana wa Ufipa wajinga. Wanafikiri waliwazalo wao ndio sahihi kuliko wengine. Wanatukana kila mtu mwenye mawazo tofauti halafu wanajiita akili kubwa. Dawa yao inachemka. Watainywa Oktoba 28!

TUKUTANE OKTOBA 28!
Mnatumia makanisa kupitisha mambo ya KISHETANI?
 
Kijana mdogo akiwa na roho ya chuki akizeeka lazima awe mchawi. Rais Magufuli yupo hadi 2025 na mkileta za kuleta tunamuongezea muda. Nyie jifanyeni mnajua, mtaona!
Kuna tofauti yoyote ya kimkakati kati ya ccm na shetani?
 
Uongozi wowote duniani unatoka kwa Mungu. Uongozi wa Rais Magufuli unatoka kwa Mungu. Kama wewe unafikiri uongozi unatoka Ubeleji, subiri uone.

TUKUTANE OKTOBA 28!
Nikisoma Biblia kwa habari za wana wa Israel, walipotenda dhambi na kukataa kutubu, Mungu aliachia Shetani kuweka mfalme wa giza (maana Mungu ni Nuru) ambaye atawatesa watu mpaka watakapopata akili na kumrudia Mungu. Mungu siku zote yeye ni mwema na anapoondoa mkono wake Ibilisi anatawala. Kwa wafalme waovu ninaowafahamu, tunaweza kumsema sana Rais wetu lakni tukimlinganisha na wengine, kwa macho ya kibinadamu bado raisi wetu ni mcha Mungu. Tunapoongelea wafalme waovu ni kama Hitler, Idi Amin na wengine wengi waliowahi kutokea.
 
Wajasilia dini katika ubora wao , yaani bora usalie nyumbani , Mungu atakusikia kuliko kwenda kanisani kusalishwa na wanafiki kama hawa.
 
Na uende, safari njema. BWANA atajitwalie kondoo wengine. Hata mawe atayainua
Maneno yenu ya ki Mungu mnayo yataja mnapokua kwenye mic hovyo tusha yazoea hivyo hamtusumbui Mungu mnae midomoni ila ktk imani na matendo yenu holaaa
 
Kwani niliposema "Uongozi unatoka Mungu" kuna mahali nimeandika "Uongozi wa Urais"? Au ni matatizo ya kuchelewa kuelewa na kuwahi kujibu?

..samahani kama nimekukwaza.

..nilikuwa najaribu ku-address imani tunayolazimishwa kwamba ni Raisi wa Jamhuri peke yake ndiyo ametokana na Mungu.

..ukweli ni kwamba viongozi wote wanatokana na Mungu.
 
Back
Top Bottom