Je, kanisa la mhubiri Christopher Mwakasege liko wapi?

BAD NEWS:-
Mwalimu Christopher Mwakasege amefiwa na baba yake mzazi, shughuli za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Tukuyu Mbeya zinafanyika Mbezi Beach kituo cha Jogoo kwa kaka mkubwa wa Mwalimu Mwakasege kuanzia saa tatu. Muwakumbuke kwa sala wafiwa na wale wote watakaosafiri kuelekea Tukuyu Mbeya
 


Ahsante bwana Pukudu maana umesema ukweli na ukweli mtupu kumhusu huyu mtumishi wa MUNGU. Mwakasege ni moja ya wahubiri wachache ambaye akikwambia acha dhambi na ukimwangalia matendo yake(japo kwa nje maana ni mungu anayejua ya sirini) utakubali kwamba kaul zake zinaongozwa na ucha mungu. Ni tofauti sana na wahubiri wengine ambao wanavyohubiri na ukiangalia matendo yao inatia shaka wazi wazi.
 

Mtumishi C. Mwakasege amefiwa na baba yake mzazi nafikiri juzi au jana kwa hiyo nafikiri atakuwa anashughulikia maandalizi ya mazishi ya baba yake mzazi. Na siku 9 zijazo atakuwa na semina pale Dar viwanja vya Ananasif Kinondoni hivyo apeleke huyo jamaa yake pale akafanyiwe maombi.
 

You're quite right Nasolwa. Mi simfagili huyu mtumishi na nipo naye usharika mmoja wa KKKT Kijenge hapa Arusha. Niko karibu sana na watu wa naofanya ktk huduma yake pamoja na jirani yangu wa karibu ambaye anamsaidia wife wake kwa shughuli fulani fulani. Nimejaribu kuwafuatilia hawa wote kwani napenda kujua huyu mtu wa Mungu anavyokuwa akiwa nyumbani. Hawa watu wote huwa wananiambia Mwakasege is real a servant of God kwani hana double life kwa maana ya kwamba anacho hubiri ndivyo alivyo popote pale alipo . Nyumbani ana upendo na mahusiano yake na timu yake ni ya Kiroho sana kiasi kwamba ukimletea mashataka au umbeya umbeya atakwambia basi mpendwa piga magoti tumwombee huyu mtu unayemsema vibaya. Hana kashfa ya ngono ,fedha wala huwezi kusikia akisemwa kwa mambo ya ovyo ovyo au kujiingiza au kujipendekeza kwa viongozi wa kisiasa.

Sisi tunamwombea Mungu aendelee kutumika kwa ukamilifu huo
 
Huyu Mwakasege ndiye mwenye upako haswa mafundisho yake utayapenda tena ni mtu anayefahamika vizuri toka zama hizo matendo yake yanajieleza yenyewe kwa wale wanaomjua,siyo kama wale wanaotuelezea kuwa wameshawahi kuwa ma Dj au wezi haijulikani wamepataje upako au nguvu za giza
 


Nakubaliana na sifa ulizompa mtumishi huyu wa Mungu - lakini naona kama vile umesifu kama vile UNAMWONA HADI MOYONI.......
wakati anapofanya huduma yeye mwenyewe.......naamini anakaa kiti cha mbele ... au??? Hivyo kukaa kiti cha mbele wakati upo kwenye huduma ni kitu cha kawaida na UNAPOMKARIBISHA MTU AKAE KITI CHA MBELE KWENYE HUDUMA YAKO ... ni kawaida pia - so Wachungaji wana haki zote kumkaribisha wakiwa kwenye huduma zao - Pia kukaa kiti cha mbele haiongezi wala kupunguza utukufu mtu alio nao mbele za Mungu na kukaa kiti cha mbele sio kukosa unyenyekevu, au kukaa kiti cha nyuma sio unyenyekevu ... ile ni "seat" tu - mambo yote yako moyoni.

Umesema anakuwa mnyenyekevu sana kwa Wachungaji ..........sasa kwa Mtumishi (Mwalimu mkuu) kama yeye ........... what do you expect??? MIMI NADHANI SIFA AMBAYO UNGEMPA ... BILA KUMSEMEA ROHO MTAKATIFU AU MUNGU AJUAYE MIOYO YETU NI KUWA ANAFANYA KAZI YA MUNGU KWA BIDII BILA KUCHOKA ........................MENGINE NI HAPO TUTAKAPOSIMAMA MBELE ZA MUNGU AMBAYE ATAPIMA NA KUHUKUMU KILA MTU.....
Nakushauri na wewe uige na ufanye alivyo yeye ............ila YESU awe kielelezo chako zaidi.

Hayo ni mawazo yangu tu ..................ubarikiwe na Bwana Yesu
 
Christopher Mwakasege ni "MWALIMU" na huwa anapenda kujiita hivyo. Si Nabii, wala Mtume, wala Askofu Mkuu, wala Mchungaji. Na hana kanisa. Yeye ni muumini wa KKKT na anasali KKKT. Ni mtu mwenye upeo mkubwa na ni mwalimu mzuri wa dini. Uzuri wake ni kwamba hana kanisa, so wewe ukitoka kanisani kwako basi jioni unawea kwenda kumsikiliza amnapotoa mahubiri
 
Wewe unasema hivyo coz hujawahi kukutana na wachungaji/manabii wanaoua kujikweza na kujisifia mahubiri mazima na kutoa amri za kipuuzi kwa waumini. Kama Mwakasege ni mnyenyekevu lazima tuseme kwani ndivyo anavyoonekana. Kuhus roho yake hiyo ni juu yake na Mungu wake
 
Wakuu ahsdante sana. Nimefarijika sana na michango yenu kuhusu mtumishi wa Mungu mwl. Christopher Mwakasege. Mie pia ni mfuatiliaji mzuri wa vipindi vyake, na nikikosa huwa roho inaniuma sana.
Haangalii dhehebu wala dini, ndo maana hata wenzetu waislamu wanapewa ujumbe wa neno la wokovu upatikanao katika damu ya Yesu inenayo mema.

ee Mungu mwenyezi, wewe uliyetupa mtumishi wako ili kupitia yeye, neno lako liaenee nchini mwetu, mjalie na umzidishie baraka, mpe nguvu akutanapo na magumu, wewe ukamfiche na mwovu ili Bwana, hatimaye wengi wakakujue wewe kuwa ndiwe Mungu wa kweli.
Amen
 
Semina ya Mwl Christopher Mwakasege itaanza tarehe 19 February 2012 mpaka tarehe 26 February 2012 ktk viwanja vya biafra Kinondoni Dar es salaam. Karibuni tujifunze neno la uzima. Watu wa dini na makabila yote mnakaribishwa
 
Ukiona we mtumishi harafu unasifiwa na walevi, wavuta sigara, watukanaji, wazinzi na wanaofanana na hao ujue umechakachua maandiko hujahubiri kweli yote but if opposite kweli your behalf of the Jesus christ (umekemea dhambi vya kutosha)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…