Je, Kanisa Katoliki linahujumiwa na wanahabari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Kanisa Katoliki linahujumiwa na wanahabari?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kieleweke, May 3, 2011.

 1. K

  Kieleweke Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka juzi waraka wa Kanisa Katoliki ulijadiliwa kila kona. Wanahabari walijitoma huku na huko. Wengine walidiriki hata kuingia kanisani Jumapili na kuona jinsi unavyogawiwa kwa waumini.

  Leo kanisa hilo tena limetoa andiko jingine. Safari hii si waraka bali ni sala. Sala ya kuliombea Taifa katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.

  Tofauti ni kwamba kelele si nyingi kama wakati ule. Kanisa lenyewe lilisema waraka ule si lazima ufuatwe hata na wakatoliki wenyewe kwa sababu haukuwa msahafu. Lakini sala hii ni lazima. Ukitaka kuhakikisha basi Jumapili fika kwenye misa yoyote uone inavyolazimika kuisali hii sala.

  Lakini cha ajabu, vyombo vyote vilivyojitutumua kuandka waraka ule mara mia mia leo viko kimya kuhusu sala hii.

  Sijasikia mbunge akihoji sala hii waziwazi. Sijamsikia Kingunge Ngombare Mwiru wala mwanasiasa mwingine akiongelea sala hii kama walivyohoji waraka ule!

  Sala yenyewe ni hii ifuatayo:

  Ee Mungu Mwenyezi, asili ya kilicho chema,tunakushukuru kwa mema yote uliyotujalia sisi Watanzania.
  Tunapoadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya Uhuru,tunakushukuru kwa kutuwezesha kuishi maisha mema,
  Kama iwastahilivyo wana wa Mungu, Kwa kutumia busara za Waasisi wa Taifa letu,

  Umetujalia tuwe Taifa moja lililounganika katika umoja, upendo, amani na mshikamano wa kitaifa.
  Katika Kanisa kwa Baraka zako, umetujlia ufanisi mkubwa tunavyoshuhudia hivi leo.


  Kwa ajili ya kifo na mateso ya Mwanao bwana Yesu Kristo, Tunaomba msamaha kwa yote kabisa,
  ambayo kama mtu mmoja mmoja, kama jumuiya, kama Kanisa na kama Taifa tumeyfanya kinyume cha mapenzi yako


  Utuangazie sisi sote Waamini na watu wote wenye mapenzi mema, tuwe chumvi na nuru, dira na chahu bora a kukuza upendo, haki, uelewano, uvumilivu, mapatano, Amani na umoja, na hivyo uhuru wetu upate mvuto kwa ajili ya wote.

  Uwaangazie viongozi wanaotutawala kwa niaba yako, watuongoze tuweze kukaa kwa Amani na mshikamano wa Kitaifa.

  Sheria wanazotunga ziwe adilifu kadiri ya pango wako Wewe uliyetuumba kwa ajili yako.
  Bariki Taifa letu, liweze kukaa kwa mapatano na mataifa mengine.


  Tunaweka mbele yako changamoto nzito zinazolikabili Taifa hili, na mambo yote yaliyo kinyume kabisa na mpango wako wa kutaka tuishi kwa amani, zishindwe kuathri tunu bora ulizotujalia.

  Tunawaombea Waasisi wa Uhuru wan chi hii waliotutangulia. Uwapumzishe kwa Amani kwako mbinguni.
  Nasi utufadhilie kufikia ukomo uliottayarishia Wewe Mungu wa kuwa raia katika ufalme wako mbinguni milele yote.


  Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo mwanao, anayeish na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu Daima na Milele, Amina.

  Bikira Maria Malkia wa Amani, Mwombezi na Msimamizi wa Taifa letu, Utuombee.
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  kikunge huwa anatatizo la kuangalia upande mmoja tu hili ndio tatizo kwa viongozi wa kisiasa nchi hii si ccm tu hata cdm
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana na waandishi wa bongo wengi wao ni makanjanja tu, hawawezi kulifanya chochote zaidi ya kutafuta vichwa vya habari tu!
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wanahabari wengi wa Bongo, lakini sio wote, wana-suffer from parochialism and less serious brains in engaging critical thinking. Wamekaa kama parrots of some sections of the rich people or certain organizations.
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  May 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Chichiemu wamezidiwa na matatizo wangesharopoka kama ngumbalo wao kingwendu ambaye hajulikani ni mwanamke(muislamu) au mwanaume(mkiristo) utafikiri popo!
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kanisa naona kama linajipendekeza hivi!! eeeti waislam wenzangu!
   
Loading...