Labda tupate viongozi ambao wamewahi kuishi, sio kusoma tu, mbele. Nchi za mbele watu wanapanga ratiba za kazi na biashara zao mwaka mzima in advance. Rais hawezi kulishtukiza Taifa eti "kesho sikukuu."
Mtu ana appointment ya mkutano Jumatatu, ana bajeti, tiketi na reservation ya hoteli kuondoka Jumanne, wewe unatangaza ghafla "kesho sikukuu." Afanyeje? Mtu ana appointment ya kuchukua conteiner bandarini Ijumaa wewe unatangaza Ijumaa sikukuu mpaka Jumanne, nani analipa gharama za ghafla za extra storage? Vipi kama ni bidhaa zinazoharibika zisipopokelewa na kutuzwa ipasavyo siku ile ile, hujazorotesha uchumi hapo?
Tunashindwa mambo mengi sana kwa sababu tunaendesha nchi yetu kiswahili swahili kama makuzi yetu yalivyo, hatuna ratiba.