Je, Jeshi la Polisi linaweza kukataa amri haramu ya wakuu wake?

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Juzi niliona video footage moja kwenye mtandao wa voice of America mkuu wa jeshi la polisi nchini Simon Sirroanalalamika kwamba jeshi la polisi linaingiliwa na watu mpaka wanalielekeza namna ya kufanya kazi na akaongeza akasema wasilazimishe kujenga uadui na majeshi yetu. akatoa rai kwamba wajitahidi sana kushirikiana na majeshi yao wasilazimishe kujenga uadui. Aliponiacha na nikajua anongea kitu kisicho cha kweli ni kwamba yeye hafanyi kazi ya siasa ila anafuata maadili ya kazi.

Kwa nilivyomwangalia kwenye hiyo crip ni kweli anaumia moyoni mwake kwamba jeshi limeanza kudharaulika na kutoaminiwa. Ndipo nikaanza kufikiri kwamba kwa mfumo tulionao jeshi hili litaendelea kudharaulika kwa kuwa limeanza kufanya kazi ya siasa kwa kutumiwa na wanasiasa. Kwa mfano kwenye hizi chaguzi ndogo wakuu wa mikoa wanawapeleka polisi kutisha wananchi wasiende kupiga kura na idadi inayopelekwa ni nyingi kuliko hata idadi ya wapiga kura katika jimbo husika, mfano mmojawapo ni jimbo la Siha na Monduli, akina Mrisho Gambo walipeleka askari wengi kupita maelezo wakipita mtaani wakitisha watu. Makonda alionekana akishangilia ushindi na jeshi la polisi, yule kamanda wa Mwanza ameonekana kwenye video footage akijifungamanisha na ccm hadharani bila kificho na hajakemewa, Sasa huyu mkuu anapotwambia kwamba hafanyi kazi ya siasa anamaanisha nini?

Cha pili kwa kuwa polisi wanapewa amri na wanasiasa na kwa kuwa hawaruhusiwi kuuliza amri waliyopewa matokeo yake wanafanyishwa kazi kama misukule tu, ina maana wanaweza wakaamriwa kusindikiza hata madawa ya kulevya, kusindikiza masanduku yaliyo na kura haramu, wanaweza pia kusindikiza mali za wizi za wanasiasa kwa kuwa hawana haki ya kuhoji wakubwa wao, wanaweza pia kutekeleza amri ya kuua wafuasi wa vyama vingine maana watakuwa wanatekeleza amri ya wakubwa wao ambao mostly ni wakuu wa wilaya na mikoa ambao ni makada kindakindaki wa chama tawala. Ndo nauliza je polisi ana haki ya kukataa kutekeleza amri haramu?
 
Kuna mhenga mmoja alisema ukishakiwa polisi Ubongo wako unashuka mpaka 0% kufanya kazi na kufikiri. Sababu kutoka hapo unachotakiwa kusema ni NDIO MKUU/AFANDE huruhusiwi kufikiri nje ya hapo
 
Kuna mhenga mmoja alisema ukishakiwa polisi Ubongo wako unashuka mpaka 0% kufanya kazi na kufikiri. Sababu kutoka hapo unachotakiwa kusema ni NDIO MKUU/AFANDE huruhusiwi kufikiri nje ya hapo
Hii ni hatari kwa usalama wa raia, kwa sasa hivi ambapo Magu amesema hakuna ushindi kwa vyama pinzani hata kama wameshinda raia wataamua kuchukua sheria mikononi
 
Wanasema Kule Ni Amri Kwenda Mbele

Ni kweli amri lakini iwe legitimate, kwa nchi ambazo zinaendeshwa kitaasisi mambo kama haya hayafanyiki. Ili tumfanye mkuu wa polisi nchini asipokee amri za kishenzi kutoka kwa watawala cheo cha IGP akishateuliwa isiwe rahisi kumfukuza kazi mpaka bunge lilidhie, hii itampa nafasi IGP kufanya kazi kwa weledi na kutotekeleza amri za kishenzi kama za kichaa wangu Magu.
 
Sheria ya ndio mzee ifutwe vyombo vyetu vya ulinzi kupitia hii sheria vinakua kama misukule wawe nao wana hoji kwa nini
 
ila kuwa polisi/mwanajeshi raha sana, ukiwa na boss unakuwa mpole kama fundi saa ila ukifika mtaani kila mtu ni mkeo yani full respect.
 
Back
Top Bottom