Je, jamii imejaa udanganyifu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, jamii imejaa udanganyifu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MdogoWenu, Dec 22, 2010.

  1. M

    MdogoWenu Senior Member

    #1
    Dec 22, 2010
    Joined: Dec 23, 2009
    Messages: 168
    Likes Received: 23
    Trophy Points: 35
    Ukichunguza kwenye jamii yetu yaani ndugu, jamaa au marafiki utaona kuna maneno yanatumika sana mfano: "tushirikiane", "tusaidiane "tuwe na umoja", "tuchangiane", "tusiwe wachoyo", na mengine ya namna hiyo.

    Sifa moja ya maneno haya yanamfanya kila mwanajamii asiyeshawshika nayo "hana umoja", "anajiona", "anajisikia", "anajitenga na jamii", "anajifanya anazo", "mpanda ngazi hushuka" .

    Lakini sifa nyingine ya maneno yale ni kwamba yanatamkwa na watu ama wenye hali ya chini kimaisha au wababaishaji maishani ambao shughuli za kwenye jamii hazieleweki.


    Kwa nini kwenye jamii hiihii hayatumiki sana maneno sahihi kama vile "utabeba mzigo wako mwenyewe", "tuwajibike", "turidhike na tulicho nacho", "mtegemea cha ndugu hufa masikini".

    Mimi nadhani kuna jambo kwamba wale wa kwanza ama ni wavivu na wanaficha matokeo ya uvivu wao kwa kusisitiza "umoja" na lugha kama zile ili wafaidike na juhudi za wenye juhudi za kimaisha.

    Kwamba wenye juhudi tutawapata tu kwa kuvumisha maneno yale watakayoyaogopa kwani yanawafanya wajione wako nje ya jamii.

    Sijui wenzangu mnasemaje.
     
Loading...