Je, inawezekana kushitaki kampuni za simu kwa kuuza till zetu za uwakala wa huduma za kifedha kwa watu wengine?

MmatengoOG

Member
Sep 1, 2020
28
26
Watu wengi sana wamewahi peleka documents zao ili wapate uwakala wa MPESA, TIGO PESA NK. Lakini TILL zao zilipotoka waliuziwa watu wengine. Maana now unachukua documents zile zile unaambiwa Till yako ilishatoka na hawatoi mara mbili kwa documents zile zile.

Kwa nini tusiungane na kuzishtaki haya makamuni yakatufidia?
 
Kwa nini kuungana ikiwa mimi sina tatzo?

Twende kwenye solutions.

Kama document zako zilitumika kutoa TILL kwa mtu mwingine ambae sio wewe, ni rahisi kumpata!

Kila laini ya simu za uwakala ujue zinapigiwa na kupokea simu. Hivyo ni kama laini za kawaida isipokua zimeongozewa uwezo wa kufanya biashara ya money transfer.

Uwaambie wakuoneshe hizo namba za hao watu wenye TILL ZAKO. Kama ikiwa ngumu POLISI hadi mahakamani utapata msaada vizuuuriiii!

Za mwizi 40
 
.....

Mzee wenye hili tatizo wanaweza kuwa wengi
Sema ndo vile kila mtu unaangalia namna ya kusolve balaa linalokukuta mwenyewe bila kuangalia umma unasemaje
 
Huo mchezo wanao wahudumu mimi till nimeaaply nikapewa baada ya miez 6 nikaweka kwenye smartphone nilikuta imefanya miamala zaidi ya miez mitatu.
Ila hakuna namna kufa kufaana
 
Watu wengi sana wamewahi peleka documents zao ili wapate uwakala wa MPESA, TIGO PESA NK. Lakini TILL zao zilipotoka waliuziwa watu wengine. Maana now unachukua documents zile zile unaambiwa Till yako ilishatoka na hawatoi mara mbili kwa documents zile zile.

Kwa nini tusiungane na kuzishtaki haya makamuni yakatufidia?
Kama wametumia documents zako kusajili till, maana yake hiyo till ni mali yako, na kwa utaratibu ninao ujua itakua una line ya till ambao ulipewa siku ya kwanza ulipoenda kuomba till...na documents zako zimefanana na majina yaliyopo kwenye iyo till.
So fanya uombe kama kuna till ingine kwa documents zako ifungwe au u swap uwe nayo wewe.
 
Back
Top Bottom