Je, inawezekana kiinua Mgongo Kufika Mill 100 kwa wastaafu?

IZENGOB

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
242
250
Naomba ufafanuzi kwa anayejua masuala haya,jana kulitokea msuguano kati yangu na WIFE ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi na mimi ni mfanya biashara,anadai kuwa mpaka kustaafu kwake atalipwa milioni 100 kama kiinua mgongo,kwa sasa anapokea Basic salary ni 419,000/= na take home 350,000/= ana miaka 5 kazini na kabakiza miaka 33 kazini je ni kweli anaweza kupata milioni mia?Ninaomba anayejua kuhusu masuala haya atutatulie suala hilo.

Wakiwa ofsini wanaambizana ndoto za kumiliki m100 hukuwa kitumia Reference ya walimu wastaafu wanaodai wamepewa kiasi hicho cha pesa.
 

Msungu inv

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
260
250
Kama atajiendeleza kielimu na kufikia shahada ya awali atazidi hicho kiwango. Ila kama atabakia na astashahada kwa sasa ni around mil 75 baada ya kutoa kodi
 

trigeminal

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
1,700
2,000
Achana na pensheni kama ana cheti halali ajitahidi ajiendeleze diploma mpaka degree sababu yumo kwenye system tayari
 

IZENGOB

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
242
250
mzee wangu alistaafu kama afisa elimu wilaya......... mafao yake alilipwa milion 105 total.. mwaka jana.. alikaa serikalini for 40 years

hizi ajira hizi hazilipi sana kiivyo... tusiziendekeze sana...
Duuu
 

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,698
2,000
mzee wangu alistaafu kama afisa elimu wilaya......... mafao yake alilipwa milion 105 total.. mwaka jana.. alikaa serikalini for 40 years

hizi ajira hizi hazilipi sana kiivyo... tusiziendekeze sana...
Wazee wa zamani walianza na mishahara mdogo sana, wengi wamestaafu na hela kama hiyo na kama elimu yake pia ilikuwa ndogo. Kuna jirani yangu ni teacher wa Sec alistaafu 2015 yeye ni degree zile za zamani, alianza kazi na degree alipata 158 million. Mwenyewe anasema mwaka alograduate university of daresaalam walikuwa wahitimu walimu 18 tu, chuo kizima...kabla ya utitiri wa wanavyuo kama Siku hizi.
 

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,523
2,000
Hizo mbwembwe za mkeo zisikustue sana. Ni mambo ya kibiashara tu hayo ndiyo maana wamemwambia mkeo anachotaka kusikia na roho imemruka.

Hata kwenye kutunga sheria za kodi duniani walitumia mbinu kama hizo (Robin Hood idea) sababu maskini walitaka kuona matajiri wanalipa zaidi.

Na wewe kama uko kwenye biashara tumia Algamish theory utakuwa na zaidi ya hizo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom