Ikulu: Rais Kikwete hataidhinisha mabilioni ya kiinua mgongo kipya cha wabunge!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,034
144,388
Tuesday, February 4, 2014

jk+bunge.jpg

Dar es Salaam.
Ikulu imesema Rais Jakaya Kikwete hatakubali kuidhinisha kama akipelekewa ombi la kuongeza kiinua mgongo cha wabunge kutoka Sh43 milioni hadi Sh160 milioni.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana kuwa Rais Kikwete hajapokea maombi hayo huku akipinga maelezo kuwa Serikali ilishayakubali.

Gazeti dada la The Citizen wiki iliyopita, lilimkariri Waziri wa Fedha, Saada Mkuya akisema Serikali ilikuwa imepitisha kupandishwa kwa kiwango cha kiinua mgongo kutoka Sh43 milioni hadi Sh160 milioni baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitano.

Waziri huyo alikaririwa akisema kuwa kiwango hicho kilipitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na tayari wabunge walishaanza kuchukua fedha hiyo licha ya ukweli kuwa Bunge hili halijamaliza muda wake.

Hata hivyo, Rweyemamu alisema nao wamelisoma suala hilo kwenye magazeti na kwamba halijafika Ofisi ya Rais... "Suala hili halijafika Ofisi ya Rais hata kama litaletwa, `I really doubt if the President will endorse such matter' (Nina shaka kama Rais ataidhinisha suala hili)."

Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi tayari imekanusha vikali taarifa za kupandishwa kiwango hicho cha malipo kwa wabunge.

Kashililah akanusha

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alikanusha kuwapo kwa mapendekezo ya wabunge kulipwa kiasi hicho cha fedha.

"Malipo ya wabunge yanalipwa kwa mujibu wa sheria kwa Kiingereza inaitwa Political Service Retirement Benefits Act (Sheria ya Malipo ya Utumishi kwa Viongozi wa Kisiasa) ni sheria namba 3 ya 1999, kwa hiyo hakuna malipo yoyote yanayoweza kufanyika nje ya sheria hiyo," alisema Dk Kashililah na kuongeza:

"Sheria inaelekeza kila kitu, kwa kuzingatia uhalisi wa mishahara ya wabunge kwa sasa, malipo yao ya mwisho hayawezi kufikia kiasi cha Sh160 milioni, hata kama mishahara itaongezwa haitaweza kufikia kiwango ambacho kitamwezesha mbunge kulipwa kiasi hicho cha fedha."

Katibu huyo wa Bunge alisema malipo ya kiinua mgongo kwa wabunge yanakokotolewa kutokana na kiwango chake cha mshahara tu na siyo malipo ya posho za kuendesha shughuli za kibunge.


Licha ya Dk Kashililah kukataa kutaja kiwango cha mshahara wa mbunge kwa mwezi, gazeti hili limebaini kuwa malipo hayo kwa sasa ni Sh3.4 milioni.

Mbali ya mshahara, wabunge pia hulipwa fedha nyingine kiasi cha Sh8.2 milioni kwa ajili posho ya jimbo, gharama za ofisi, mafuta, malipo ya wasaidizi wao na dereva.

Matakwa ya sheria

Sehemu ya tano ya Sheria ya Malipo ya Utumishi kwa Viongozi wa Kisiasa katika Kifugu cha 21 inasema mbunge atalipwa kiinua mgongo ambacho ni asilimia 40 ya mshahara ya kila mwezi katika kipindi chote cha utumishi wake.

Kadhalika, Kifungu 18 (3) Mbunge atalipwa malipo ya nyongeza yanayoitwa posho ya ukomo wa Bunge (winding up allowance) ambayo ni asilimia 20 ya jumla ya mishahara yake ya miezi 24 iliyopita.

Kwa tafsiri ya sheria hiyo na kwa kigezo cha mshahara wa Sh3.4 milioni, wabunge wa sasa watalipwa kiasi cha Sh97.92 milioni watakapomaliza uongozi wao mwishoni mwa mwaka ujao.

Malipo hayo ni Sh81 milioni ambayo ni asilimia 40 ya jumla ya mishahara ya miezi 60 ya utumishi wa wabunge hao na Sh16.32 ambazo asilimia 20 ya mishahara ya miezi 24 kwa ajili ya malipo ya posho ya ukomo wa ubunge.

Malipo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia zaidi ya 100 ya kiinua mgongo cha Sh43 milioni walicholipwa wabunge waliostaafu 2010.

Kabla ya kupandishwa kwa kiwango hicho kuwa Sh43 milioni mwaka 2010, kwa miaka kadhaa kiwango cha kiinua mgongo kwa wabunge kilikuwa Sh20 milioni.


Chanzo:
Mwananchi

MY TAKE:

Sijui Jk kaangalia upepo unakwendaje au ndio ilikuwa dhamira yake,mimi sijui.

Na je wale wabunge ambao taarifa za awali zilidia kuwa wameshachukua mikopo huku wakitarajia mafao hayo kuwa ndio dhamana yao itakuwaje?

Napata mashaka na ukweli wa hii taarifa kwan mbunge atakopeshwa vipi bila dhamana yake kudhibitishwa na taasisi inayomkopesha.

Je,ina maana walipewa mikopo bila taasisi husika kupewa uthibitisho wa mafao hayo?!

Hii habari inaweza kuwa ni funika kombe mwanaharamu apite!
 
wabunge wetu ni janga la taifa. pamoja na ugumu wote huu wa maisha na hali ya uchumi kuwa mbaya lakini wao wanajiongezea posho. huu ni usaliti mkubwa sana kwa wananchi waliowachagua.
 
Ikulu imetoa taarifa kuwa haitaidhinisha ongezeko jipya la kiinua mgongo cha wabunge kutoka milioni 40 za sasa mpaka milioni 160.

CHANZO:Mwananchi.
Kama ni kweli basi Kikwete atakuwa ametumia akili saba na ujasiri mkubwa. Watu wote wanatucheka kwa kusikia wanachotaka kujilipa ambapo BBC wamesema ni ongezeko la asilimia 274.
 
Watu wepesi sana kusahau!
Hivi mnakumbuka kuhusu sakata la kuongeza mishahara na sitting allowance ya wabunge?! Ikulu ilisema yake, bunge likasema yake kutia katibu wa bunge kisha makinda nae akasema yake!

Mwisho wa siku ikaidhinishwa kimya kimya! Huku tukichekelea kama mazuzu
 
Ngoja wamkoromee kidogo uone jinsi atakavyonywea ghafla. Kwani kama hatasaini ni lazima hiyo kurugenzi yake ya habari itoe taarifa? mbona kuna mengi amesaini pasipo kutoa taarifa kwa umma ikiwemo mikataba tata aliyosaini na wachina.
 
Wabunge wenyewe wengi vichwa maji wanachofanya bungeni kupigana na kutoka bungeni hiyo hela yote wapewe ya nini waende zao wala wasituchefue kabisa kabisa.
 
Zuga tu wabunge watachukua chao kama kawa.Walalahoi tutaendelea kuminywa na makato ya kodi kuwalipa hawa wazandiki mpaka hawa jamaa waelewe kwamba sisi ni mabosi wao.
 
Watu wepesi sana kusahau!
Hivi mnakumbuka kuhusu sakata la kuongeza mishahara na sitting allowance ya wabunge?! Ikulu ilisema yake, bunge likasema yake kutia katibu wa bunge kisha makinda nae akasema yake!

Mwisho wa siku ikaidhinishwa kimya kimya! Huku tukichekelea kama mazuzu

Mkuu,hili neno!
 
Kikwete haaminiki.
Hii habari ilivyokuwa imeandikwa kwenye gazeti la the citizen na jinsi wahusika walivyo comment baada ya kuulizwa ni wazi atakuwa 'kasikilizia' na itakuwa tunajidanganya kukubali kuwa hakujua kilichokuwa kinaendelea.

 
Watu wepesi sana kusahau!
Hivi mnakumbuka kuhusu sakata la kuongeza mishahara na sitting allowance ya wabunge?! Ikulu ilisema yake, bunge likasema yake kutia katibu wa bunge kisha makinda nae akasema yake!

Mwisho wa siku ikaidhinishwa kimya kimya! Huku tukichekelea kama mazuzu

Ni aibu!
 
Back
Top Bottom