Je, inawezekana huu ndio mwisho wa utumbuaji wa papara na kukurupuka?! Mkuu kutumbuliwa soon!

Wanabodi,

Tangu kuanza kwa zoezi la tumbua tumbua kunakofanywa na uongozi wa awamu ya tano, kuna baadhi yetu, mimi nikiwemo, tunaounga mkono nia njema na ya dhati, ya rais wetu katika tumbua tumbua hizi, kwa kusema "He is doing the right thing, at the right time, but in a wrong way!", tukisisitiza, mtindo anatumia kutangaza kutumbuliwa huku, sometimes ni wrong way.

Pamoja na kuwa kiongozi wetu ni binadamu na sio malaika, hivyo anaweza kufanya makosa, ila kwa vile macho na masikio yote ya Watanzania yako kwake, he has an obligation ya perfectionism, to be perfect!, "He got to do the right thing, at the right time, and do it right!".Watanzania

Sasa leo katika pita pita yangu, viwanja fulani, nikakutana na very encouraging news ya mkuu fulani wa taasisi fulani ya umma ilikuwa atumbuliwe, ila utumbuaji huo umeahirishwa na muda na kusongezwa mbele!. Hizi ni habari za kutia moyo sana kwa sababu sasa inaonyesha kuna kila dalili ya kupungua kwa papara na utumbuaji wa 'fuahisha genge', na badala yake, kuongezeka kwa umakini, kuwepo kwa subra na matumizi ya busara badala ya mihemuko kwenye zoezi la tumbua tumbua!.

Kama kawaida yetu sisi wana JF, unapokutana na habari yoyote kubwa from a trusted source, na wewe unawapakulia wana JF wenzako, ili kuwafanya wana jf kuendelea kuipata ile jf advantage ya "Be the first to know!", kuwa kuna kiongozi mwingine mkuu wa taasisi ya umma, atatumbuliwa next week!.

Kiongozi huyo wa taasisi ya umma (jina kwenye mabano) iliyo chini ya wizara fulani (kwenye mabano), ilikuwa atumbuliwe wiki hii, lakini utumbuaji huo, umeahirishwa kidogo kwa sababu fulani maalum na muhimu, hivyo atatumbuliwa rasmi anytime next week, or probably kuanzia weekend ya wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo inayoanzia Julai 11!.

Nawaombeni msiniulize source, kwa sababu nafuata misingi ya kitu kinachoitwa "the confidentiality of the source" wala msiniulize ni mkuu wa taasisi gani, iko chini ya wizara gani, na kwa nini anatumbuliwa!.

Tangu tumbua tumbua ianze, tumeshuhudia watu wakitumbuliwa papo kwa papo wengine kwenye kadamnasi ya watu kwa mtindo ambao hufanywa na ma populist leaders wa tawala zote za kiimla kote ulimwenguni!, wengine wetu mimi nikiwepo, tukalipigia sana kelele hili la tumbua tumbua za papara na kukurupuka!, sasa nafarijika kuwa kilio chetu hatimaye kimesikika, mtumbuaji amekuwa msikivu, zile kelele zetu na kiritiki kwa zoezi la utumbuaji wa kutafuta sifa na kutaka tuu kushangiliwa na umati wa watu,zimesikika, sasa utumbuaji sio tuu unafanyika kwa makini zaidi, bali pia unafanyika kwa kistaarabu kidogo,ikiwemo subra na kutumika kwa busara zaidi ya hisia!, tena na sio ghafla na kushtukiza kama tumbuaji za nyuma!.

Nasifu na kuunga mkono kwa asilimia 100% utumbuaji wa majipu unaofanyika kutumbua majipu ya ukweli kwa kistaarabu kwasabu jipu lilioiva halina dawa nyingine yoyote zaidi ya kutumbuliwa, ila sio utumbuaji wa kukomoana, au kuonyeshana, au utumbuaji wa vijibu uchungu ambavyo havihitaji hata kutumbuliwa, bali kunahitajikakuwekwa kwa mfumo ambao kukijitokeza tuu kijipu, kinajitumbua chenyewe bila kuonekana maigizo ya oneman show kutumbua kijipu kimoja, viwili kwa mbwembwe na kushangiliwa na umati wa watu, huku kuihalisia ni mfumo mzima ndio umeoza!.

Utumbuaji wa kiongozi huyu ninayemzungumzia kwenye uzi huu, ilikuwa atumbuliwe papo kwa papo this week lakini kuna majitu very bold nchi hii, yakamkabili mzee mtumbuajia majipu, yaka inject some senses za busara into his head, na kweli juhudi hizo zikazaa matunda!, zoezi la utumbuaji likasitishwa kwa muda, na sio kufanyika kwa ghafla na kwa pupa kama walivyotumbuliwa wengine!, swali kuu la kujiuliza sio mkuu huyo anayetumbuliwa ni nani, bali kuna sababu gani, iliyopelekea mtumbuliwa huyu ambaye alikuwa atumbuliwe wiki hii, lakini utumbuaji huo ukasitishwa, kwa nini utumbuaji usitishwe na ni mtu gani huyo bold enough aliyemkabili mtumbuaji, kuzuia utumbuaji huu?!.

Haya ni maswali wanaojiuliza watu wenye uwezo wa kufanya kitu kinachoitwa "critical thinking" hawa hutafuta "the motive behind", "the causative factors or agents" na "the underlying facts" yaani visababishi, sababu sio zilizosababisha atumbuliwe, bali zilizopelekea utumbuaji uhairishwe na kusongezwa mbele kidogo!.

Majibu ya maswali yote hayo ninayo, ila naomba niyahifadhi kwanza, kuusubiria huo utumbuaji wenye kwanza kama utafanyika, au taahirishwa jumla!, ukiishafanyika, ndipo nitarejea kuwajulisha wanabodi humu, hilo jitu very bold lililomkabili mtumbua majipu, na kitu kilichopelekea kucheleweshwa kutangazwa kwa utumbuaji huo!.

Tip kama hizi sometimes zinasaidia, kwa sababu siku zote utumbuaji hufanywa siri, na hufanyika kwa ghafla, sasa inapotokea taarifa za siri za utumbuaji, zime leak hadi zimetufikia watu kama akina sisi wa media, ili na sisi tukazilikishe kwenye media kama hapa jeiefu, kunaweza kupelekea mtumbuaji akaahirisha jumla utumbuaji huu alioupanga, hivyo tip hii ndio ikawa manusura ya mtumbuliwaji huyu!, na hili likitokea, them mimi nitakuwa sina pa kutokea zaidi ya kuonekana ni muongo na mzushi, kuwa kulikuwa hakuna utumbuaji wowote uliopangwa na ndio maana hakuna yoyote aliyeyumbuliwa kufuatia bandiko hili!.

Nitayakubali matokeo!.

Nawatakia Jumatatu Njema.

Pasco

Rejea.
Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete .
Hii Tumbua Tumbua ya Rais MAGUFULI, Hivi KIKWETE Anajisikiaje ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ..
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais

Kwahiyo unasema Mkuu anaendeshwa na mihemko??..???
 
Sio ngumu kumbaini huyo mtumbuliwa Pasco, atakuwa ni yule aliyepingana na maamuzi ya kukurupuka ya mkulu hivi karibuni. Amini nakwambia, akiondoka huyu Mpogolo ambaye ameonyesha assertiveness ya hali ya juu halafu akawekwa huyo bosi mpya wa aina ile ya 'NDIYO MZEE' basi tujiandae kwa majanga zaidi ya kiuchumi ktk nchi hii hasa endapo bosi huyo mpya atakuwa kama yule wa TRA hapo hesabu tumeumia.
o_O:confused:
 
Nashangaa mnapohangaika kumshauri Magufuli na kumuacha mfalme Mbowe akitumia mabilioni ya fedha kufanya maandamano nchi nzima , lkn akiulizwa lini atajenga ofisi ya chadema anasema hana hela !!!!


Ufipa boys amukeni kutoka usingizini chadema inaliwa na mafisadi
Yaani wewe mtu uvyama unauweka mbele kuliko utaifa dah
 
Unajua wao walichokuwa wanaangalia ni rangi ya mwamvuli siyo mwenye kuubeba na kuingia nao kwenye mvua kujikonga. Hata hivyo madhara yakaanza kuonekana ni makubwa kuliko angekuja yule mjombake Richard. Ila ninaamini mkwe alichanganyikiwa baada ya little brother kuonekana wateja hawamkubali kwahiyo mambo yakawa mambo
 
Back
Top Bottom