Je imeshawahi kukutokea?

Je imeshawahi kukutokea?

TANMO

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
12,211
Reaction score
13,052
Umekwenda Ofisini kwa watu kuwarekebishia Sinki lao ambalo wanalalamika kuwa limeziba. Basi ile unaingia kwa Ofisi unakuta Sekretari ni Mchuda mmoja msupuu kinoma, basi unajiapiza ni lazima utupe ndoano zako kwake na utahakikisha Mchuda hachomoi. Basi Mchuda anakupa ushirikiano kweli kweli na mnapiga mastori kinoma na matabasamu kibao. Unaamua kuomba namba na Mchuda bila kinyongo anakupatia namba zake zote za Voda, Tigo hadi Titisii elo. Ile umemaliza kazi unaaga kwa ahadi kuwa siku moja utampigia mpate kujuana vyema.

Siku unampigia simu anakuambia alipo na wewe kwa mbwembwe zote unaamua kabisa kuazima gari ya Sela ili ukampagawishe Mchuda, unampitia haoo mnaenda kuweka pozi mahali ili mle Bata. Ile mnafika viwanja Mchuda anaagiza Fanta Pasheni na wewe kwa mbwembwe zote unamwambia aagize kitu nyingine kama anatumia, Mchuda anakupa info kuwa hanywi Pombe unamwambia powa, basi unaagiza kitu yako halafu mnaendelea na Mastori.

Sasa katika ile kuchombeza chombeza Mchuda anaanza kukuhoji kama wewe ni fulani, Maza yako alikuwa anapika vitumbua vitamu kweli na Dingi ni Mshona viatu Maarufu Kitaa enzi hizo, kimsingi anagusa mule mule.. una mdogo wako anaitwa fulani ambaye ulimuacha Darasa la tatu halafu anaanza kukueleza kuwa yeye alisoma na huyo Dogolasi wako na walikuwa Mabesti. Ile unavuta kumbukumbu basi inakukaa akilini na unakumbuka kuwa ulishawahi hata kuwapiga Twisheni enzi hizo. Ukikumbuka enzi hizo uko Praimari ulikuwa mfano wa kuigwa kwa Tabia nzuri mpaka ukawa Kiranja Mkuu na madogo walikuwa wanakuheshimu kinoma. Mpaka ulikuwa idol wao kitabia, kimwili, kiakili mpaka kiroho.

Ingelikuwa ni wewe ungefanyeje?

Ufunguo:
Mchuda - Binti
Msupuu - Mzuri
Kinoma - sana
Sela - Rafiki
Dogolasi - Mdogo mtu


Mapendo
TANMO.
 
mmhhh mpaka kiroho madogo walimsahau hadi muumba wao hii soo usije ukarudia tena umesikia
 
Back
Top Bottom