Je, IGP Sirro tuyaamini Maelekezo yako au tuuamini Utendaji wa Kiushahidi wa RPC Muroto wa Dodoma?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,681
109,092
Nakumbuka ni Wiki mbili tu ulisema tena kwa Hasira zako za Kwetu ‘ Uzanakini ‘ Mkoani Mara kuwa hupendi tabia ya Wakuu wako wa Polisi wa Mikoa ( RPC’s ) ya Kuwakamata Watu ambao hata bado Mahakama haijawahukumu na Kuwaonyesha hovyo mbele ya Vyombo vya Habari huku ukisema kuwa huko ni Kutafuta tu Sifa au Kujiingiza katika Siasa za Kipuuzi na ukasema kuwa Kisijirudie tena.

Lakini leo hii tena kwa Jeuri kabisa huku akionekana akijiamini na pengine kudhihirisha kuwa Yeye analijua vyema Jeshi la Polisi kuliko Wewe RPC wa Dodoma Afande Muroto amekirudia Kitendo kile kile ambacho Bosi wake IGP Sirro alikipinga na Kukikataa cha Kuonyesha Wahalifu wa Pesa mbele za Vyombo vya Habari.

Kwa aina tu ya ‘ Body Language ‘ ya RPC Muroto sasa GENTAMYCINE naanza kupata Hisia kuwa Wawili hawa IGP Sirro na RPC Muroto wana ‘ Bifu ‘ moja matata na la hatari mno ambalo nahisi linaweza Kuondoka na Mmoja wao Siku si nyingi.

Hapa kuna mambo makubwa mawili ama IGP Sirro hapendi Sifa na Umaarufu alionao na anaoendelea Kuupata RPC Muroto au RPC Muroto haamini na hapendezwi na Sirro kuwa IGP pengine kutokana na sababu za Kipolisi anazozijua Yeye ila kuna ' Fukuto ' kubwa baina ya Mandata ( Mapolisi ) hawa Wawili Waandamizi kabisa nchini Tanzania.
 
Kwa lile povu la Sirro siku ile, na hizo sifa na jeuri ya huyo Muroto, hakika lolote linaweza kutokea. Huenda anapongezwa kwa kazi nzuri na mamlaka za juu zaidi pasipo Sirro mwenyewe kufahamu.

Hatutashangaa balozi mpya mteule (Sirro) akiteuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na huyo mzee wa sifa! maana ndiyo awamu ya wapenda sifa hii.
 
Nami naliona hili kwa mbali Mkuu na huenda Siku moja likaja kuwa kweli. Hawa Wawili lazima tu watakuwa hawaivi kabisa.
 
Kwa lile povu la Sirro siku ile, na hizo sifa na jeuri ya huyo Muroto, hakika lolote linaweza kutokea. Huenda anapongezwa kwa kazi nzuri na mamlaka za juu zaidi pasipo Sirro mwenyewe kufahamu.

Hatutashangaa balozi mpya mteule (Sirro) akiteuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na huyo mzee wa sifa! maana ndiyo awamu ya wapenda sifa hii.
CV yake ndogo sana yule alitakiwa hadi sasa awe OCS tu huko hombolo
 
IGP anao uwezo mkubwa sana tu kumtia adabu huyo Muha. Mfano akamuweka ndani n.k na Rais asimaindi na uzuri Rais ana idea kidogo na adhabu/discipline za kijeshi
 
IGP anao uwezo mkubwa sana tu kumtia adabu huyo Muha. Mfano akamuweka ndani n.k na Rais asimaindi na uzuri Rais ana idea kidogo na adhabu/discipline za kijeshi
Hawezi maana kuna ma RPC wengine wanakua na sauti kuliko IGP mfano Kamanda Kova alivyokua na sauti kuliko IGP Ernest Mangu na hii sijui inasababishwa na nini maana IGP atabaki kulalamika tu mpaka anapelekwa huko ubalozini kuiwakilisha Tz!!
 
IGP alikuwa sahihi ni Mtuhumiwa sio kwamba ndio katibitika ana kosa, Ni makosa makubwa kumuonyesha kwenye Vyombo vya habari tena kwa maneno ya kejeli kwamba " huyu ndio mwizi/kibaka/jambazi/ ....nk" . Askari Polisi na Wakubwa zao wote wafuate Sheria
 
Tukumbuke ni mahakama ndio iliwahi kukemea na kuzuia hili jambo LA kuwaonyesha watuhumiwa hadharani na kuwahukumu katika matelevisheni. IGP ni kama alikuwa anakumbushia tu!!!. Na huyu RPC hakukiuka maagizo ya IGP aliyatii kabisa hakumuanika mtuhumiwa hadharani alionyesha manoti tu!!!
 
Ni kweli Mkuu, hata mimi nimeona RPC Gilles Muroto akionyesha mabulungutu ya fedha, lakini hakumuonyesha mtuhumiwa kama wengine wanavyosema.Bila shaka RPC amezingatia maelekezo ya kutokuonyesha watuhumiwa kwenye media yaliyotolewa na IGP Afande Simon Nyakoro Sirro.
 
IGP alikuwa sahihi ni Mtuhumiwa sio kwamba ndio katibitika ana kosa, Ni makosa makubwa kumuonyesha kwenye Vyombo vya habari tena kwa maneno ya kejeli kwamba " huyu ndio mwizi/kibaka/jambazi/ ....nk" . Askari Polisi na Wakubwa zao wote wafuate Sheria
Nimekumbuka hii "WAMAKONDE WANAJUA I LOVE YOU"-Muroto
 
Back
Top Bottom