DODOMA: Rais Samia kuunda Kamati Maalumu kufuatilia mwendo wa Majeshi yote nchini

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuunda kamati ya watu 12 na sekretarieti ya watu watano kwa ajili ya kufuatilia utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini humo.

Rais Samia ametangaza kuunda kamati hiyo Jumatano Juali 20, 2022 mara baada ya kumuapisha Camillus Wambura kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Kabla ya uteuzi huo, Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nafasi ambayo ameteuliwa Ramadhan Kingai ambaye awali alikuwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kigoma.

Rais Samia amesema kamati hiyo itakayooongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Othumani Chande na makamu wake atakuwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambayo itakuwa ikimshauri njia bora ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi wenye matokeo bora kwenye vyombo vya haki jinai.

“Kwa hiyo tutaanza na polisi, wakimaliza wakileta ripoti tutafanya marekebisho, tunakwenda majeshi mengine, tunakwenda magereza, hivyoo mpaka tumalize,” amesema Rais Samia

Amesema kwa ufupi serikali inakuja na jicho jingine ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama na kubainisha kamati hiyo itakuwa ikimpelekea mrejesho kila Jeshi linapomalizwa kuchunguzwa na kufanyiwa maboresho.

“Tutakuja na miundo inayofaa sasa hivi ili kuja na jeshi linalofaa na bora kutumikia Watanzania,” amesema Rais Samia

Mbali na IGP Wambura kuapishwa, wengine walioapishwa ni, aliyekuwa IGP Simon Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Luteni Jenerali, Mathew Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia na Dk. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi.
 
Jeshi la Uhamiaji linakula sana Rushwa.

Wanafuatiwa na jeshi la Mgambo kazi yao ni kula Chakula cha Mama lishe na kupiga Machinga.

Jeshi la CCM AKA Polisi Tanzania hao ni wasaidizi kwenye Ballot Box
 
Pendekezo langu kwa kamati:
1. Majeshi yote ya invest kwenye High-Technology. Tafiti zote nzr na Sustainable USA. Source of idea ni jeshini. Hii ita tokea iwapo tu Majeshi yetu ya ajiri ma genius.
2. Waka some huko Russia, China, Turkey, Germany, Israel, nk. Majeshi yawe mbele ya waarifu.
3. Zima moto. kila Secondary ya Bweni, chuo na Halmshauri ziwe na Gari za zima moto. Naona NEMC wamepanga kuchoma nchi siyo kwa utitiri huu wa Petrol station kila uchochoro. NEMC hawana Master plan ni rushwa tu.
 
Welldone my President Samia, so far so good upande wangu na ninaamini chini ya utawala wako,utawala bora utatamalaki na mimi kuanza kuwaona polisi wangu wakifanya kazi zao kwa uadilifu, pls unda kitu kinaitwa IPID, hawa ni police wa police ni kama MPs wa TPDF, siku women's &men's in uniform watakapofikia entry level ya utendaji kazi wa police wa Botswana, nitafurahi mno!!!
 
Pendekezo langu kwa kamati:
1. Majeshi yote ya invest kwenye High-Technology.
2. Waka some huko Russia, China, Turkey, Germany, Israel, nk. Majeshi yawe mbele ya waarifu.
3. Zima moto. kila Secondary ya Bweni, chuo na Halmshauri ziwe na Gari za zima moto. Naona NEMC wamepanga kuchoma nchi siyo kwa utitiri huu wa Petrol station kila uchochoro. NEMC hawana Master plan ni rushwa tu.
Safi sana ingawa tunatofautiana mno kwenye no 3 yako,mimi ningeliondoa kijeshi kikosi cha uokoaji na zimamoto na kuweka vikosi hivi chini ya metros, municipalities, uaskari wao utaondolewa na technology ya utendaji kazi utaongezwa including using drones
 
Pendekezo langu kwa kamati:
1. Majeshi yote ya invest kwenye High-Technology. Tafiti zote nzr na Sustainable USA. Source of idea ni jeshini. Hii ita tokea iwapo tu Majeshi yetu ya ajiri ma genius.
2. Waka some huko Russia, China, Turkey, Germany, Israel, nk. Majeshi yawe mbele ya waarifu.
3. Zima moto. kila Secondary ya Bweni, chuo na Halmshauri ziwe na Gari za zima moto. Naona NEMC wamepanga kuchoma nchi siyo kwa utitiri huu wa Petrol station kila uchochoro. NEMC hawana Master plan ni rushwa tu.
Upo ndotoni
 
1 na 2 ni idea nzuri sana, inapaswa kuanza kutumika kwa haraka JWTZ.
 
Hii dunia ya teknojia,
Polisi watumie camera na voice recorder, itasaidia ku-record kila tukio linalo fanywa na polisi.

Kwa nchi za wakubwa wanatumia , ningumu mchunguza polisi mmoja mmoja
 
Wananchi hawalalamikii miundo, wanalalamikia watendaji ambao wanatumiwa na wanasiasa na ambao wanashindwa kuwa wabunifu

Unapelekwa Central police pananuka,Kuna Chawa na kunguni, jela mnapangiwa muda wa kunya😁
 
Sijui atatumia maajabu gani kuliondoa jeshi la polisi na vitendo vya rushwa iliyokithiri (hasa kwa wale jamaa zetu wa barabarani), matumizi makubwa ya nguvu kuliko akili, na kutumiwa na ccm nyakati za uchaguzi.

Hayo ya miundo ya vyeo vyao, kwa kweli watajuana wenyewe.
 
Uharibifu wa pesa, hakuna asiyejua makando kando ya jeshi la polisi hadi yeye mwenyewe alishawahi kuadithia mikasa aliyofanyiwa na polisi.
Kwahiyo afanye maamuzi kienyeji bila taarifa inayojitosheleza? Rais Samia yuko sawa, uchunguzi ufanyike
 
Sisi wanaichi tunataka kisikia Ile TUME YA WAZIRI MKUU MAJALIWA DHIDI YA MAUJI YA MFANYABIASHARA WA MADINI KULE MTWARA ILIISHIA WAPI?
HIZI NGONJERA ZENU HAZINA FAIDA KWA MTANZANIA WA KAWAIDA....HAO POLISI KAZI YAO NI KUUWA RAIA TU
 
Back
Top Bottom