Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 79,037
- 168,688
Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1900 huko Urusi kulikuwapo na jamaa mmoja aliyeaminika kuwa na nguvu za miujiza katika kuponya wagonjwa. Lakini vilevile alionekana kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kutabiri.
Uwepo wa jamaa huyo katika falme ya urusi, ulisababisha migogoro kwenye uongozi wa dola hiyo, kitu kilichochochea kupinduliwa kwa aliyekuwa mfalme wa urusi, Tsar Nicholas II
Unajua ilikuwaje?
Jamaa huyo alikuja kupata Umaarufu mkubwa mnamo mwaka 1903, pale alipoingia mjini st Petersburg Na kukutana na familia ya mfalme Tsar Nicholaus II na mkewe Aliyeitwa Alexandra.
Mtoto wa mfalme aliyeitwa Alexei alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa uliyejulikana kama Haemopholia ambao alikuwa akitokwa na damu na damu mfululizo hali iliyomfanya akaribie kufa.
Sasa kwakuwa huyo jamaa alisifika kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuponesha watu kimiujiza ndipo akskutanishwa na familia ya mfalme ili kujaribu kumponesha Alexei..Na kwa bahati mtoto yule alipona mara baada ya kukutana na huyu jamaa.
Mara baada ya tukio hilo, Ikatokea kwamba mke wa mfalme Nicholas II, Aliyeitwa Alexandra alitokea kumshukuru sana na kumthamini jamaa huyo kwa kitendo chake cha kuokoa uhai wa mwanae. Na Hivyo walimwambia aanze kuishi hapo (kwenye makazi ya mfalme) kama shukrani.
Ndipo hapo ukawa mwanzo wa jamaa huyu kuishi 'palace' na familia ya mfalme.
***
Kipindi cha vita ya kwanza ya dunia, Mfalme nicholaus aliondoka urusi na kwenda kwenye viwanja vya mapambano kuvisimamia vikosi vyake vilivyokuwa vinapigana vita.
Sasa huku nyuma, alimuacha mkewe pamoja na jamaa huyo...(kilichotokea sitakielezea hapa, utatafuta mwenyewe kwa muda wako)
Ila kilichochea viongozi wengine wa serikali kuja juu na kupanga njama za kumuua, njia waliyoitumia kujaribu kumuua ni kumuwekea sumu kwenye kinywaji, lakini cha ajabu jamaa huyo sumu ilikuwa haina madhara mwilini kwake...hahah.
Lakini mwisho wa siku walimuua tu kwa njia nyingine, na baadae tukaona Tsar nicholaus na mkewe wanauwawa na kufanya mwisho wa utawala wa kifalme urusi. Na kujulikana kama Mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917.
Je, huyu jamaa ni Nani?
Uzi huu ni kwa HISANI ya Kichwa kikuu
0621002295.
Attachments
Last edited by a moderator: