Je, huu utaratibu utapunguza ajali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, huu utaratibu utapunguza ajali?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tisa desemba, Dec 1, 2011.

 1. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wadau, leo asubuhi nikiwa mtwara stendi kwenye bus la sumry kabla ya safari ya kuja dar kuanza, aliingia ndani ya bus askari (trafiki) mwenye cheo cha koplo akajitambulisha na kuanza kutoa maelekezo kwa abiria kama umuhimu wa kufunga mikanda, umuhimu wa kuandika majina halali kwenye tiketi, namba za dharura endapo kutakuwepo na ukiukwaji wa sheria za barabarani n.k

  ghafla
  , akasema sasa ni wakati wa dereva kula kiapo mbele yangu na ninyi abiria.

  dereva akaanza, mimi ..................(akataja jina) dereva wa bus la sumry lenye namba T......ABD, naapa kwamba nitaendesha bus kwa kufuata sheria na taratibu zote za usalama barabarani na ninaahidi kutoa ushirikiano na msaada kwa abiria wangu wakati wote wa safari, safari yangu itapitia mikoa ya mtwara, lindi, pwani na dar es salaam, eeh Mwenyezi Mungu naomba nisaidie.

  JE, HII MBINU ITAPUNGUZA AJALI,tujadili.
   
Loading...