Je huu ni wakati muafaka kwa CHADEMA kutangaza sera ya majimbo?

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Katika siku za hivi karibuni baadhi ya viongozi wa kitaifa wa CHADEMA wamenukuliwa wakitangaza sera ya majimbo ambayo miaka ya nyuma iliwahi kufanya CHADEMA isiwe na mvuto na taswira njema mbele ya jamii kutokana na wepesi wa sera yenyewe kupigwa propaganda za upotoshaji kuhusu udini, kuvunja nchi n.k kutoka kwa wahasimu wao wakubwa yaani CCM.

baada ya viongozi hao kuanza kutangaza sera hiyo tayari wahasimu wao wakubwa yaani CCM ambao walikuwa kimya kabisa kutokana na kushindwa kuhimili vishindo vya tuhuma za ufisadi wameanza kupata ujasiri na pumzi za kuanzisha upya propaganda chafu dhidi ya CHADEMA. Hivyo natoa tahadhari kwa viongozi wa CDM kutafakari upya kuhusu kutangaza sera hiyo hivi sasa.

Ni vyema wangeendelea na kupambana na ufisadi na kutetea raslimali za taifa hadi pale watakapokamata dola watekeleza hiyo sera kama ambavyo CCM wamekuwa wakitekeleza sera mbali mbali badala ya kuanza kuliweka jahazi letu pancha kwa mikono yetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom