Matumizi yanazidi kutokana na hasara wanazoleta kwa makusudi. Pia mwingine hajithamini mwenyewe anakaribishwa kwenye chumba cha watoto kitanda shuka na godoro safi lakini haogi mchafu ukimfundisha ni ugomvi tuu. Wangekuwa wanajithamini na kufanya kazi kwa uaminifu wangependwa tu. Mbona wengine wanasomeshwa kabisa
Ninachokiona wako unatembea na ile kanuni ya kwamba jibebe nikubebe.
Swala la upendo kwa mtu ama unapoamua kujitolea kumfanyia jambo fulani sio mpaka umwangalie yuko vipi au mpaka afanye kitakacho kufurahisha wewe ndiyo umuoneshe upendo.
Hapo kinachokosekana kwa mabwana wengi ni upendo nakutokuuthamini utu wa mtu, wengi wanajichukulia wao kama wao na kujiona wathamani kuliko hao wanao watumikisha.
Mkuu Tized nashukuru sn kwa Hoja yako! Tena umetanua mada mpk kwa madreva! Ni Kweli Mkuu mdreva Na wao wanapata shida sn! Unakuta wanawapeka maboss zao ktk mambo Yao binafsi wanabaki kulala Na kusinzia kwenye Gari weeee huku boss akijilewea mipombe Na vimada au akifanya michepuko Na bila kuja Driver amekula au amekunywa chochote Na wakati huo huo Hawa madriver ndio wanaotunza siri nyingi za maboss wao!
Si uungwana ata kidogo!
Unajua mkuu haya mambo yana pande mbili house girl anapothamini kazi yake hata mwajiri atamthamini lakini kuna wengine akiingia kwako tu matumizi utadhani umenunua magari 4 yanayokunywa mafuta hasa kwa uharibifu wa makusudi kukosa uaminifu kazi zenyewe hazifanyiki vizuri. House girl wa namna hii hata mwajiri hatamthamini.lakini kuna wengine huwezi jua kama ni house girl
Unakuta mtu ana wafanyakazi wa ndani yani (House girls) wawili na watoto wake. Anatoka nao kwenda kwenye mgahawa kupata chakula na kinywaji kidogo!
Kwanza anapofika ktk mgahawa haongozani na hao wafanyakazi wake! Anatangulia yeye na mke wake na watoto wake wa kuzaa then hao wafanya kz wanakuja wanachungulia chungulia kwa woga na kukaa pembeni umbali wa hatua 30 kutoka meza ya mabwana zao! Na hawaruhusiwi kuagiza chochote mpaka agizo litoke kwa Bwana.
Na wanakaa wametulia na kujalibu kuwatuliza watoto wa Boss wao ambao wanaonekana ni watundu na wanaokimbiakimbia hovyo ktk mgahawa!
Then baada ya hapo Bwana na bibi wanaagiza chakula na kinywaji na kula wao tu peke yao huku wale wafanyakazi wamekaa pembeni tena ktk viti vya wageni ktk mgahawa huku hawatumii chochote!
Je huu ni uungwana kweli kwa mtu anaekutunzia na kukuangalizia watoto wako wakati wewe ukiwa ktk mapilika ya maisha yako? Na hii mpaka nje km kwenye migahawa mtu anaweza kuwafanyia hivi wafanyakazi wake wazi wazi, je huko ktk familia yake majumbani si ndio balaa kabisa?!!
Maana huko inaonekana ni marufuku mfanyakazi kula chakula km anachokula bwana! Bwana km anakula chips kuku, mfanyakazi anakula ugali Dagaa au maharagwe. Boss km anakunywa maji ya kwenye Fridge yaliyopowa basi mfanyakazi anakunywa ya kwenye ndoo! Na huenda ni marufuku kukaa sebuleni kuangalia Tv au kuwasha tv na redio!
Nauliza jee huu ni UUNGWANA KWELI?
mwallu Karucee miss neddy tian Ennie Annie charminglady Heaven on Earth Mr Rocky Mndengereko Mentor Kaizer Eiyer OLESAIDIMU Tized kiwatengu watu8 Arushaone Samaritan Mashaxizo etc all. Nauliza Je, huu ni uungwana Kweli?
Mimi sikukuzwa na housegirl..sina experience hapo!!!
si uungwana kwani walikuwa na uwezo.wa kuwaacha nyumbani wao wakaenda wenyewe au na watoto wao.
kitendo hicho kinaonyesha jinsi watu hawa walivyo na upeo mdogo. lakini pia kuwaacha hawa mabint kwenye viti vya wageni ni kueadhalilisha kiaina wamewaona hawajui chochote na hawaezi kusema chochote.
natoa angalizo hawa mabinti huwa hawajibu kwa mdomo ila wao huwa wanajibu kwa vitendo mama/baba unawatendea isivyo majibu watapewa wanao muda ambao haupo!!!
....Limbukeni wa maisha tu huyo mtu na mkewe. Ustaarabu gani huo? utasema hakufunzwa kuishi na watu.
Pia sina shaka familia ya namna hiyo wana upungufu mkubwa wa kiimani.
Maisha ni mtihani tu, hao anaowaona ni #Watumwa wake, ndio hao hao anaoamini 24/7
wakae vizuri na wanawe, akili kweli hiyo?
KARMA will catch up na familia ya aina hiyo.
What goes around comes around.
Nakushukuru Mkuu Ntuzu, umesema vizuri sana apo... Hata maandiko yanasema .. Kwa kadiri mlivyowatendea wadogo hawa, Mlinitendea Mimi (Mungu) na pendine maandiko yanasema ...Amsaidiaye MASIKINI humkopesha Mungu, naye anamlipa kwa matendo yake mema. Mithali 19:17